Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
Kuna siku ndo nimetoka kireport kazini kama siku mbili 3 hivi nmebaki ofisini mwenyewe si nikaachia hewa chafu pale mara paap Boss huyu hapa ofisi inanuka balaa hakika nilipata fedhehea ya kufa mtu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
Aisee noma sana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Bora alifukua tope
 
Nakumbuka mwaka 2004 Mimi bishoo kinoma sasa kipindi kile zilikuwa zimetoka jinsi Fulani tulikuwa tunaita mikasi,maana zilikuwa nyeupe mixed mikasi mikasi rangi nyeusi!,sasa bana dukani zilikuwa bei juu kinoma,Mara kuna mshkaji wangu mmoja hivi nilikuwa na rap nae kipindi hicho akaniambia anauza jinsi hiyo mikasi kwa 7000tsh nikaona kama ndoto vile sikuamini ,nikachomoa fasta pesa ya ada ambayo nilikuwa natakiwe nilipe kesho yake nikampa jamaa 7000tsh akaniletea ukali,fasta Mzee mzima nikaingia kuoga kwanza nikatupia vitu vikali na ile jinsi nikaanza kunesa kitaani sikufika hata mbali ni kama mita 200 tu kutoka home mama mmoja alikuwa na wanae kama wa nne hivi wakubwa kimtindo akanisimamisha,nilivyosimama baada ya salamu akaniambia mwanangu samahani Nina wasiwasi na jinsi uliyovaa ni ya mwanangu huwa anaibiwa sana jinsi kwahiyo nikaamua nikimnunulia mpya huwa kuna sehemu naweka alama,kwahiyo kama huamini alama ni Fulani na nimeweka sehemu Fulani tukikuta sio usijali mwanangu nakurudishia jeans yako!
Kwa vile home ilikuwa ni mita 200 tu kutoka pale hao mpaka ghetto nikavua suruali tukakuta ni kweli zile alama zipo,nikamwambia mama Mimi nimeuziwa na MTU Fulani na bahati nzuri ni jirani yake alikuwa anamjua vizuri, Mzee nikaachia jeans kesho yake nikamtokea mshkaji aliyeniuzia kimya kimya ghettoni kwake nikamweleza kisanga jamaa kumbe ndio ilikuwa ndio zake bila hiyana akanipa jinsi nyingine sikuipenda sana lkn nilikuwa sina namna na akanisisitizia hiyo sio ya wizi Mimi nikasepa zangu na urafiki ukaishia hapo
 
nakuja PM unipe number yake
 
Nikiwa form 2 kwenye miaka ya 2000 kuendelea..nikiwa kama kijana sharp kabisa kwenye extended family yetu hapa Dar..Mshua akanipa pesa shilingi milioni moja za ujenzi nipeleke moshi kwa bibi yangu mlokole asilimia (100%)Basi laki tano nikaweka mguu wa kushoto tano nyingine mguu wa kulia...
Nikapewa ticket ya Bus moja nakumbuka likiitwa Amazon na fedha taslimu elfu 70 nauli ya kurudi na pesa ya kijikimu na zawadi za njiani kupeleka kwa bibi na simu ndogo ya kufunua aina ya Bird kwa ajili ya mawasiliano.
Nikatoka zangu kinondoni studio mpaka ubungo terminal, bus nikaliona nikaenda kwenye kibanda nikanunua pombe pakti 3 aina ya Tyson nakumbuka walikua wanauza 650 kwa pakti moja nikaipiga pale pale mbili nikapanda nazo kwenye bus...Nilikua nimekaa kwenye siti ya 2 by 2 dirishani ghafla wakapanda wadada wawili na mkaka mmoja ...dada mmoja mweupe mwenye shepu.. yani ni mkubwa kabisa kuliko mimi akaja akakaa akanisalimu wenzake wakakaa siti ya mbele yetu...Sasa mm nina pombe yangu nilikua napenda apande hata msela akae na mm ili niwe huru kukata na kunywa pombe yangu[emoji23]Basi nimejikaza mpaka maili moja kibaha nikasema hapana wakati nafikiria nn cha kufanya wale wa mbele wakampa mwenzao katoni ya castle lager za kopo akatoa moja akafungua akaanza kunywa akaniambia karibu kaka nikachukua kopo ...zikaisha tokaongeza...mara nimetoa kisimu nijifanye kumbeep bibi ilimradi vurugu nikatoa na yale mapomve makali ya viroba nakumbuka tuliwaka sana...To make the long story short nilitakiwa kushuka Kiboriloni nikajikuta niko hoteli moja arusha inaitwa Seven Eleven kama sikosei....niko uchi niko na yule dada[emoji23][emoji23] kumbe nilikata moto simu nimezima sipatikani yule demu kumbe kwenye milioni akadai eti nilinwambia tutumie laki tu zinazobaki tutaenda ngorongoro pakikucha akawa anezihifadhi..kweli kuhesabu nina laki 9[emoji23][emoji23]Nikawasha simu nikapiga kwa bibi nikamwambia nimejikuta asubuhi nyuma ya bus nililotoka nalo dar nimelala na kwenye pesa baba alizonipa imechukuliwa laki moja akapiga vigelegele kanisa lao lina branch arusha akawaelekeza wakaja kunichukua nikapewa shemasi anirudishe Moshi kama shujaaa.....Sijahi muhadithia mtu...yani hapa kwenyewe nlikua naandika nafuta naandika nafuta....kama yule dada yupo humu hata anipM jamaniii[emoji23][emoji23]
 
Pole mzee
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1487][emoji1487]
 

Hivi kuna mama mkwe analipaga deni?
 
Mimi na mke wangu tulienda kusalimia kwao(ukweni) sasa tukarudi nyumbani nikaona bora niwajurishe kuwa tumefika salama daaaa nikajikuta nimetype haraka haraka na kisimu changu cha tochi kuwa "TUNASHUKURU TUMEFI.LA SALAMA" Then nisend faster kwa mama mkwe aisee alienistua mke wangu kwa sababu ya upekuzi (u spy) wake inbox
 
Hahahahaa we mse.nge unakismati kichizi[emoji23][emoji4][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Iyo kitu naomba isije nitokea kwa kwel
 
Hili nalo tukio aiseee. Pole
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…