Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri

Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri

Portion 16:

...... Safari haikuboa. Mpaka tunafika, Mimi na yule Mzee aliyekuwa pembeni yangu tulikuwa tunapiga story kana kwamba tulifahamiana siku nyingi. Nilikuja kufahamu jina lake, anaitwa Mr. B. Alikuwa ni mtu mwenye ufahamu na mambo mengi sana. Japo taaluma yake ilikuwa ni tofauti kabisa na ya kwangu, ila wote tulifanya kazi kwenye taasisi zilizopo chini ya wizara moja. Mtu wa kariba yake ni kama dhahabu endapo ukiwa karibu yake. Nadhani ndio maana hata Mzee wa Kongowe alitaka niwe nae karibu.

Mr. B alikuwa nimpenda kusoma vitabu, na hicho ndio kilisaidia Mimi na yeye kuelewana. Katika vitabu vyote ambavyo nimeshasoma, kila nilichomtajia, alikuwa nae ameshakisoma. Alifurahishwa na tabia yangu ya kupenda kusoma vitabu. Akaniandikia list ya vitabu 10 ambavyo alisema angependa niwe nimevisoma ndani ya mwaka mmoja. Na tokea siku ile, amekuwa na utaratibu wa kunipa list ya vitabu vya kusoma kila tunapouanza mwaka. Tokea nimefahamiana nae, nimejikuta nasoma vitabu vingi sana tofauti na kipindi cha nyuma.

Kwa kiasi kikubwa amenisaidia sana kuibadilisha akili yangu.

Siku moja tukiwa short break wakati wa training, ulikuwa muda wa chakula. Kuna picha moja nilimpiga Mr. B wakati anakula. Ilikuwa ni picha nzuri, hivyo akahitaji nimtumie.

Baada ya kuipata picha, akaamua kusave namba yangu. Whatsap wanamtindo ukitaka kusave namba ya mtu, basi sehemu ya kuandika jina wataweka jina ambalo huyo mtu ndio ameliweka Whatsapp. Mimi Kwa upande wangu niliandika "Amphibian" hivyo Mr. B alivyokuwa anasave namba yangu, likakaa ilo jina.

Mr. B: "Amphibian? Seriously?"

Nilijisikia noma sana, sikuwahi zingatia ile sehemu na sikuona kama ni kitu kikubwa. Ila Kwa mtu wa heshima kama yule, niliona kama ameniona miyeyusho.

Ila na yeye kwenye kuisave namba yangu, akaamua kuisave hivyo hivyo Amphibian. Na ndio jina ambalo amekuwa akiniita tokea siku hiyo. Mpaka kuna muda huwa nahisi akitajiwa jina langu halisi anaweza asinitambue kwa haraka.

Training ilikuwa ni ya siku 30 kisha tukarudi nchini na kutawanyika, maana tulienda watu wa taaluma tofauti tofauti, japo karibia wote tulikuwa chini ya wizara moja.

Ile siku ambayo ndio tulirudi, mida ya usiku Mzee wa Kongowe akanipigia simu:

Mzee: "Vipi mambo yameendaje huko?"

Mimi: "Vizuri tu, hata Mr. B tunaelewana vizuri sasa hivi"

Mzee: "Nimefarijika kuona unaenda vizuri nae"

Analyse: "Ndio Mzee, tunaelewana kwa kiasi fulani"

Mzee: "Ukielewana nae vizuri, ni mtu mzuri sana huyu. Anaweza kukusaidia pakubwa"

Analyse: "Nitajitahidi kuendana nae"

Mzee: "Unajua kwenye maisha kila kitu huwa kina zeeka. Kitu pekee ambacho hakizeeki ni connection na watu. Na hicho ndio kila mtu anapambania. Kwa Mr. B upo sehemu sahihi. Anaweza kukusaidia zile sehemu zote ambazo Mimi sikuweza".

Analyse: "Mzee ni mkarimu na muelewa sana, nina imani nitaenda nae vizuri"

Mzee: "Pamoja na kumuona muelewa, ila hanaga uvumilivu kwenye mambo mawili, mali zake na binti yake wa mwisho. Kuwa mwangalifu na hivyo vitu"

Analyse: "Ilo lisikupe shaka Mzee"

Mzee: "Unajua sisi ambao familia zetu sio popular kwenye siasa, tunatumia nguvu kubwa ili kuweza kukaa level za juu. Na ndio maana tukistaafu ni rahisi kusahaulika. Kesho yako inategemea na mambo utakayofanya leo, jitahidi kila nafasi unayoipata unaitumia vizuri, huwezi jua siku moja itakuweka kwenye level gani"

Analyse: "Nitajitahidi sana kwenye ilo Mzee"

Mzee: "Nakukumbusha tena huyo sio ndugu yako, hivyo jitahidi kumfanya awe karibu nawe. Jitahidi usivuke mipaka"

Baada ya hapo tukaagana, akakata simu.

***** ***** ***** ******

Tokea niondoke Dar kwa kiasi fulani nimekuwa na amani, japo imekuwa ngumu kuzoea life la huku nilipo. Ofisi anayofanyia kazi Mr. B ipo mkoa huu huu niliopo hivyo imekuwa rahisi sana Mimi na yeye kuinteract. Amekuwa ni mtu wa kunishauri na kunipa facts za hapa na pale ambazo zimekuwa msaada kwangu.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikijaribu kubadilisha vitu kwenye maisha yangu , ila nimekuwa nafeli mara zote. Hii inatokana na kwamba nilikuwa najaribu kubadilisha kila kitu, ila nasahau kubadilisha fikra zangu. Tokea nimefahamiana na Mr. B, nimekuwa napigania sana kubadili fikra zangu, na Kwa kiasi fulani nauona mwanga.

Siku zote amekuwa akijaribu kunipa mwongozo kwenye vitu kadha wa kadha. Kawaida huwa nikishatoka kazini kuna sehemu napendaga kwenda kukimbia kimbia na kucheza mpira kidogo. Jioni moja nikiwa natoka mazoezini, nikakuta missed calls za Mr. B, ikabidi nimpigie:

Mr. B: "Amphibian hujambo?"

Analyse: "Sijambo Mzee. Shikamoo"

Mr. B: "Marahaba. Mbona hupokei simu zangu?"

Analyse: "Nilikuwa mazoezini kidogo Mzee, hivyo simu sikuwa nayo"

Mr. B: "Mazoezi gani ya muda huu, mbona unaleta ujanja ujanja kijana?"

Analyse: "Muda huu ndio narudi, ila nilienda mapema tu"

Mr. B: "Wik end ratiba yako ipoje?"

Analyse: "Usafi tu mida ya asubuhi, na jioni ndio kama hivi nakuja kupunguza mafuta ambayo sina"

Mzee akacheka:

Mr. B: "Basi kama utaweza, ukitoka kwenye hayo mazoezi yako, uje nyumbani kwangu"

Analyse: "Siku gani haswa ambayo utahitaji nije?"

Mr. B: "Jumapili itakuwa vizuri zaidi"

Analyse: "Sawa Mzee"

Baada ya kukata simu, nikabaki najiuliza "Huyu Mzee ananiitia nini?". Sikupata jibu, na sikuona haja ya kuendelea kujiuliza maswali mengi wakati nikienda nitajua.

Hiyo siku tuliyokuwa tunaongea ilikuwa ni alhamisi. Ilipofika jumapili, mida ya saa moja nikawa njiani kuelekea kwake. Nilikaribishwa vizuri, nikakuta msosi umeshaandaliwa nikajumuika nao mezani. Nikiangalia mezani, naona mboga ni nyingi kuliko vyakula vingine. Kibaya zaidi nikaambiwa Mimi ndio nianze kupakua. Nikapakua aste aste, lakini nilivyoanza kula nashangaa wali umeisha, nimebaki na mboga tu kwenye sahani. Nilikuwa naona aibua wakati hakuna hata aliyekuwa na muda na Mimi.

Baada ya kula, tukawa tunapiga story na Mr. B pale sebuleni:

Mr. B: "Vipi mambo yako yanaendaje sasa hivi?"

Analyse: "Mungu ni mwema Mzee, yanaenda"

Mr. B: "Nafurahia sana kuona jinsi ulivyosharp. Usipoteteleka, utafika mbali sana"

Analyse: "Mungu anisimamie"

Mr. B: "Hivi ukiachana na hii kazi yako, unajishughurisha na kitu gani kingine?"

Nikataka nimwambie namiliki bodaboda kuna mtu nimempa mkataba, ila nikasita. Maana Mshua wangu mwenyewe nilivyomwambiaga nimenunua bodaboda, aliniambia nitafute kitu kingine maana hiyo sio biashara, muda wowote naweza kupigiwa simu niambiwe chombo kipo chini ya fuso, mtaji na faida vinapotea ndani ya sekunde chache. Hivyo kama Mshua alinikataa, huyu Mzee itakuwaje?

Analyse: "Sina chochote zaidi ya kazi yangu Mzee"

Mr. B: "Seriously?. Una nguvu, una muda, inakuwaje unakubali vyote vipotee hivyo?"

Analyse: "Kitu cha kufanya ndio sikioni"

Mr. B: "Mbona vya kufanya vipo vingi sana?. Anzisha hata kampuni, kuna watu wanakampuni za (....) au (....) mambo yao yanaenda vizuri tu. Commitment na dedication ndio kila kitu"

Analyse: "Ni kweli unachosema, ila mtaji wa kuanzisha hiyo kampuni ndio ugumu ulipo"

Mr. B: "Ugumu? Kwani kampuni ni nini mpaka iwe ngumu kuanzisha?"

Nikamulezea uelewa wangu juu ya kampuni. Akacheka:

Mr. B: "Kuna tofauti kati ya kampuni na ofisi Amphibian. Hapo wewe umeelezea ofisi za kampuni, na sio kampuni yenyewe. Kuna watu wanamiliki kampuni na hawana hata physical office, wana laptop na briefcase tu na mambo yao yanaenda. Acha kuniangusha kijana"

Analyse: "Sikuwahi fikiria hivyo, nitajaribu kuyafanyia kazi mawazo yako"

Mr. B: "Unajua kwa umri ulionao sasa hivi, hiki ndio kipindi cha kujaribu sana uwekezaji. Kuna wakati utafika hela yako itakuwa inaisha kabla hata haijakufikia mkononi. Ukishafika kipindi hicho kama hujawekeza popote, basi sahau kabisa kuhusu uwekezaji wowote wa maana"

Analyse: "Ni kweli Mzee"

Mr. B: "Kwa sisi Watanzania, mpaka kufika hapa tulipo tunakuwa tumepitia kwenye mikono ya watu wengi. Hivyo na sisi tunamadeni ya watu wengi hata kama hawatokuja kutudai. Hivyo ukiona kipato chako kinakutosha wewe tu, basi jua haupo salama. Maana pia kuna dharura ambazo zikija, zinahitaji uwe na uwezo wa kuhudumia hata familia kumi ndio huweze kuzitatua".

Akakaa kimya kidogo, kisha akaniuliza:

"Hivi unawekaga akiba?"

Analyse: "Mara chache chache"

Mr. B: "Ukiwa mwanaume kati ya vitu unavyotakiwa kuviogopa sana, ni kutokuwa na akiba. Otherwise, you're not safe"

Nikabaki kimya kwa muda, maana kulikuwa na uzito mkubwa kwenye vitu alivyoongea. Nilihitaji kufanya maamuzi kutoka kwenye jambo aliloniambia. Nilikaa kimya kwa muda mrefu mpaka pale aliponishtua:

Mr. B: "Naona akili yako ipo mbali sana kwasasa. Take your time, plan kitu kizuri. Alafu nisije nikawa nimekubana hapa, ukitaka kwenda kupumzika niambie tu. Maana najua kesho unahitajika kazini mapema"

Analyse: "Sikuwa nimeangalia saa kabisa, kumbe muda ndio umeenda hivi. Basi acha niwakimbie Mzee"

Mr. B: "Uwe unakuja tunapiga story kama hivi, hapo ni nyumbani pia"

Analyse: "Sawa Mzee, nitajitahidi niwe nakuja. Maana ninavingi sana vya kuchukua toka kwako"

Mr. B: "Anytime Amphibian"

Analyse: "Basi utaniagia kwa Mama ndani"

Mr. B: "Huyo atakuwa ameshaenda kulala, nitakuagia usijali"

Tukatoka nje, akawa ananisindikiza. Wakati tunataka kutoka getini, kuna mdada amevaa tight, raba na vesta akawa ameingia:

Mr. B: "Amphibian, huyu ni Binti yangu anaitwa Katrina, sidhani kama ushawahi kumuona"

Analyse: "Hapana, ndio mara ya kwanza hii"

Mr. B: "Huyu bwana ndio last born wangu, tena na yeye ni mpenda mazoezi kama wewe, hapo alipo anatoka evening walk"

Tukasalimiana na Katrina. Manzi mwenyewe ni ananata kuliko hata gundi, yani super glue ikasome. Maana tulisalimiana lakini alikuwa kama vile hana time na mimi. Kwa muda mchache niliomuona, ni kama aliishika akili yangu. Lakini kwa ule unataji wake, nikayafuta akilini mawazo yoyote juu yake maana sikuwa tayari kurudia makosa yaliyonifanya niondoke Jiji la Chalamila.

Lakini kumbe haikuwa rahisi kama nilivyodhani. Sijui ni Mimi ndio niliingia kwenye kumi na nane zake, au ni yeye ndio aliingia kwenye zangu, maana nilijikuta kwenye mazingira ambayo sikupenda kabisa niingie. Katrina alikuja kuwa kikwazo kwangu. Na hii ni baada ya kushindwa kufuata ushauri wa Mzee wa Kongowe kuhusiana na vitu vya Mr. B ambavyo ni untouchable.

Niliteleza padogo sana.....
Mwanaume ogopa kutokuwa na akiba, hii naishi nayo
 
Portion 17:

.... Nilivyotoka pale, nilienda moja kwa moja ghetto kwangu, ila nikawa nafikiria sana kuhusu vitu nilivyoongea na Mr. B. Unajua kuanzisha biashara sio kitu rahisi, lakini pia kujua ni biashara gani ufanye nao ni mtihani.

Wiki nzima nilikuwa naitumia kuuliza watu, google na kadhalika, ila bado sikuwa na wazo la kueleweka. Kuna siku ikabidi nimpigie Mshua, katika story za hapa na pale nikamgusia kuhusu hiyo issue:

Mshua: "Kwahiyo umefikiria nini mpaka sasa hivi?"

Analyse: "Sina wazo lolote la kueleweka mpaka sasa"

Mshua: "Wakati mnaongea nae, alikwambia nini haswa?"

Analyse: "Alishauri tu kuwa kama itawezekana nifikirie kufanya biashara nje na kazi yangu"

Mshua: "Sawa, basi endelea kufikiri. Pengine utapata cha kufanya"

Tukaagana na Mshua. Nikaendelea na ratiba zangu baada ya siku mbili Mshua akanitumia msg:

Mshua: "Kwanini usiifanyie kazi mifano yake?"

Analyse: "Unamaanisha nini?"

Mshua: "Kati ya mifano aliyokupa, chagua mmoja ndio uufanyie kazi"

Analyse: "Lakini mifano aliyotoa sina kabisa uzoefu wowote na hizo biashara"

Mshua: "Wewe huna, ila yeye atakuwa nao"

Analyse: "Lakini ni Mimi ndio nitakuwa nafanya hiyo biashara, sio yeye"

Mshua: "Utatumia uzoefu wake"

Alichoniambia Mshua, mwanzoni niliona kama hakimake sense. Ila baada ya kukosa option, nikaamua kuchagua mfano wa kwanza kati ya ile miwili aliyonipaga Mr. B. Na ili kufanikisha, ilitakiwa niende Dar. Sikuwa na uhakika kama bado mahasimu wangu wananiwinda au la, hivyo nikaona kwenda haitokuwa wazo zuri kwa wakati ule. Ikabidi nimpigie mdogo wangu, nikampanga kuhusu ile issue. Nikamuachia jukumu la usajili wa kampuni na maswala yote yanayohusu vibali.

Tulifanikiwa kuweka mambo sawa, japo mchakato mzima ulitugharimu. Kufanya biashara sio jambo rahisi, na japo tulitarajia ugumu lakini huu tuliokutana nao ulizidi.

****** ****** ******* ******

Kwa upande wa kazini niliweza kuendelea na majukumu yangu kama kawaida. Kuna siku kuna kampuni ikaja kwa ajili ya kuomba huduma toka ofisini kwetu. Walikuwa wanahitaji mtaalam ambae anaweza kuwasaidia kwenye mradi wao. Ofisi ikanipendekeza Mimi kwenda kutekeleza lile jukumu.

Ni jukumu ambalo nilikuwa nalijua kwa maana ya nadharia (theory) tu, ila sikuwahi kulifanyia kazi kwa vitendo.

Nakumbuka ilikuwa Ijumaa wakati nataka kutoka ofisini, wakati napitia email yangu kuona kama kuna taarifa yoyote. Ndio nikakutana email toka kwa boss, akinipa hint juu ya hiyo kazi. Akanitaka jumatatu nikifika nimcheki ili tujadili.

Dhumuni la yeye kunitaarifu mapema, ni kwavile hata yeye alikuwa anajua kwamba ni kazi itakayokuwa na presha sana, alafu bado sina uzoefu nayo na inatakiwa kufanywa na mtu mmoja. Baada ya kuisoma ile email, nikajikuta natamani jumatatu isifike. Sikuwa tayari kwa lile jukumu.

Wik end nilienda kuonana na Mr. B nyumbani kwake. Katika maongezi akaniambia vitu ambavyo kwa namna fulani vilinipa confidence:

Mr. B: "Unajua kwenye maisha, bahati uwaendea wenye uthubutu. Ukionesha kutojiamini, hutokaa uzipate"

Analyse: "Ilo nalijua, lakini hii ni kazi kubwa Mzee. Naweza kwenda kuharibu"

Mr. B: "Ukimwambia boss wako kuwa huiwezi, hatokaa akupe nafasi nyingine. Na ukiikubali alafu ukaenda kuharibu, hatokaa akuamini tena. Hutakiwi kuikataa, na hutakiwi kuharibu. Mpaka amekupendekeza wewe, basi kuna namna ameona utaiweza. Inakuwaje unashindwa kujiamini, ikiwa wengine wanakuamini?"

Analyse: "Huu mradi ni mkubwa sana, na kampuni ninayoenda kuwasaidia ni kampuni kubwa. Sitaki kuikataa hii kazi, ila nakosa ujasiri "

Mr. B: "Achana na ukubwa wa hiyo kampuni, weka mawazo yako kwenye kazi unayotakiwa kuifanya. Have faith in yourself"

Tuliendelea kuongea mpaka tulivyoona imetosha, nikaaga na kurudi kwangu.

Jumatatu nilionana na Boss na kweli baada ya mazungumzo ile kazi akaiweka kwangu. Baada ya wiki nikatakiwa kuonana na wale wahusika wa ule mradi kwa ajili ya kufanya nao kazi.

Nilienda nikiwa na full energy and confidence, ila nilivyofika field, confidence yote ikabakia ndani ya gari. Na kwasababu nilikuwa nasubiriwa Mimi, hivyo nilivyofika wakubwa wote wakaja kuniona, kuanzia msimamizi wa mradi, mchina, hadi vibarua. Siku ile ndio nilijua kumbe hata asubuhi ya saa mbili mtu unaweza kutoka jasho wakati mazingira uliyopo ni ya baridi, tena bila hata kufanya mazoezi yoyote.

Wakawa wananiuliza maswali ya kiudadisi dadisi walau na wao wapate kupata uelewa wa ninachofanya. Nikawapiga blah blah pale, kisha wakanisubiria nianze kazi. Siwezagi kufanya kazi kwa kusimamiwa, japo wao hawakuwa wakinisimamia, ila walikuwa bampa to bampa na Mimi, nikajikuta kazi inakuwa ngumu. Baridi ilikuwa kali, ila nikajikuta napatwa na kiu. Nikaenda kwenye gari kuchukua chupa ya maji. Nikiwa kwenye gari, kuna kibarua mmoja ambaye alikuwa ni mtu mzima (baadae nilikuja kufahamu anaitwa Mzee Moyo), alisogea hadi pale kwenye gari. Nikahisi itakuwa na yeye anamaswali, hivyo nikajiandaa kumjibu, japo nilikuwa nimekunja sura:

Mzee Moyo: "Vipi dogo, uko poa?"

Analyse: "Niko poa Mzee, Shikamoo"

Mzee Moyo: "Marahaba. Vipi kazi inaendaje?"

Analyse: "Ndio nataka kuianza hapa"

Mzee Moyo: "Una muda gani tokea umeanza hizi kazi?"

Analyse: "Sina muda mrefu sana"

Mzee Moyo: "Hii ni kazi yako ya ngapi?"

Analyse: "Ya kwanza"

Mzee Moyo: "Unaonekana tu. Ila utamudu tu, usiwe na shaka”.

Analyse: "Naamini hivyo pia"

Mzee Moyo: "Mbona kama hujiamini?"

Analyse: "Amna"

Mzee Moyo: "Sikia ni kwambie, hii kazi unayofanya hakuna yeyote hapa kati yetu anayeweza kuifanya, vinginevyo usingekuwa hapa. Unachokosa wewe ni uzoefu tu, ila hao wengine wote wanakosa uzoefu na ujuzi pia. Kwahiyo hakuna utakachowaambia, alafu wakapinga, ilimradi usiongee vitu ambavyo havipo. Ukijiamini hii kazi itakuwa rahisi sana kwako".

Nikabaki kimya namsikiliza tu. Akaendelea:

"Mimi niliishia kidato cha pili, ila kwavile nimefanya kazi sana na hawa wataalam, mpaka kuna baadhi ya mambo ya kitaalam naweza kuyafanya bila shida, na hapo sijawahi ingia darasani kuyasomea".

Haya maneno aliyaongea simple sana, ila yalinipa nguvu sana kuliko hata alivyofikiria. Nikajikuta napatwa na ujasiri, hata kiingereza kikarudi. Maana mwanzo wakati natoa ufafanuzi kwa yule Mchina, nilikuwa na scratch kama CD mbovu. Wakati bado naongea na Mzee Moyo, akaja msimamizi wa ule mradi ambaye ni Mtanzania:

Msimamizi: "Niliongea na boss wako, akaniambia bado hauna uzoefu wa kutosha na hizi kazi?"

Analyse: "Ni kweli"

Msimamizi: "Kwavile ujuzi unao, swala la uzoefu halina shida sana. Utajifunza kadiri siku zinavyoenda. Ila ninachokusisitiza, hii kazi inahitaji matokeo mazuri na haupo hapa kufanya majaribio. Ukiharibu, maana yake umeniharibia na Mimi. Kwahiyo tuliza kichwa"

Analyse: "Usiwe na shaka mkuu"

Akaondoka na kutuacha na Mzee Moyo. Alichonisaidia Mzee Moyo, ni kuchukua jukumu la yeye kuwa ananisaidia Mimi kubeba vifaa, hivyo wale wengine tukawa mbali nao. Ile kazi niliifanya vizuri hadi nikajishangaa. Tokea mradi unaanza hadi unaisha, nilikuwa beneti sana Mzee Moyo. Kama jina lake lilivyo, alikuwa ananitia moyo sana. Na kati ya watu wanathamani kubwa kwenye maisha yangu, basi na huyu Mzee wa Kingoni yupo. Na hata mradi ulipoisha, ameendelea kuwa sehemu ya maisha yangu. Sasa hivi alishaacha zile kazi, amerudi kwao Songea. Na ikitokea nimeenda kule, lazima nipitie pale nyumbani kwake Mshangano. Mungu azidi kumpa maisha marefu.

Majukumu yangu kwenye ile project yalipokamilika, nilirudi ofisini na kuendelea na majukumu mengine.

Mara kwa mara wik end nikawa naenda kumuona Mr. B nyumbani kwake kwa ajili ya kujijenga kimawazo. Katika story za hapa na pale akaniuliza:

Mr. B: "Hivi umefikia wapi katika kuanzisha biashara?"

Analyse: "Nimeshaanzisha tayari Mzee"

Mr. B: "Biashara gani unafanya?"

Analyse: "Kuna mtu nimeanzisha nae kampuni ya maswala ya (.....)"

Baada ya kusema vile, yule Mzee aliniangalia kwa muda kidogo, katika hali kama ya kushangaa hivi, lakini bila kusema chochote. Baada ya hapo akaniambia:

Mr. B: "Kwanini umefikiria kampuni ya mambo hayo?"

Analyse: "Basi tu, baada ya kufikiria, niliona hiyo ni best option kwa wakati huu”.

Mr. B: "Naomba nikiri kwamba uko smart na sharp kuliko nilivyotegemea Amphibian".

Nikasmile tu. Kati ya vitu ambavyo huwa sijivungi, basi nikupokea pongezi, haijalishi kama nazistahili hizo pongezi au la. Kiuhalisia, wazo alinipa Mshua, lakini nisingeweza kumwambia Mr. B kwamba Mshua ndio alinipa ilo wazo. Nikauchuna.

Mr. B: "Mna muda gani tokea ianze kuoperate?"

Analyse: "Miezi kama mitano sasa tokea operations zimeanza kurun"

Mr. B: "Maendeleo yakoje?"

Analyse: "Tunaenda nayo japo ni taratibu taratibu sana. Sikuwahi fikiria kama biashara ni ngumu na zinaumiza kichwa namna hii".

Mr. B: "Ndio maana waliofanikiwa wanakuwaga na uchungu na mali zao. Ukiona mtu anafanya vizuri kwenye biashara, basi jua amepitia mengi"

Analyse: "Sasa ndio nagundua"

Mr. B: "Biashara inapoanza kama hivi, jitahidi walau uifanye ijiendeshe yenyewe, hata kama faida itakuwa ndogo, hayo bado ni mafanikio. Na kama italazimika kutoa hela mfukoni ili kuipa nguvu, basi isiwe kwa muda mrefu. Unajua biashara ni kama mtoto anayejifunza kutembea. Kuna muda unakuwa unamuangalia asijiumize maana huwa anaanguka anguka sana. Lakini kuna point inafika, akishapata akili ya kutanguliza mikono wakati wa kuanguka unamuacha, maana anakuwa anaweza kujilinda.

Nendeni nayo taratibu hiyo biashara yenu. Ndani ya miezi sita mpaka tisa ya kwanza au mwaka kabisa, hakikisheni haifi wala haisimami. Mkifanikiwa ilo, miezi sita inayofatia mnaweza kuongezea mtaji kwenye hii biashara ili kukuza faida. Hakikisheni mnakuwa na mtu anayeweza kusimamia maswala yote yanayohusu kodi, lakini pia kila hela inayotoka au kuingia hakikisheni mnaiandikia itawasaidia sana mbeleni.

Kuna kosa kubwa sana nilifanya wakati nikiwa mdogo kama wewe, nisingependa kuona unalifanya"

Analyse: "Kosa gani Mzee?"

Mr. B: "Nilianzisha biashara kwa ajili ya familia, ila sikuiandaa familia kwa ajili ya biashara"

Analyse: "Unamaanisha nini? "

Mr. B: "Kwa miaka mingi nimekuwa nafanya biashara mpaka zimekuwa kubwa hivi. Nimesomesha wanangu shule nzuri, nimewapa elimu nzuri. Lakini sikuwaweka karibu sana waone ninachofanya. Nimeligundua ilo muda ukiwa umeshaenda sana"

Analyse: "Muda mbona bado upo, hata sasa unaweza kuwaweka karibu na biashara zako"

Mr. B: "Ili waweze kuwa karibu, inabidi wawe na interest. Na interest zinajijenga taratibu, kwa kuona, kushiriki nk. Mtoto wangu wa kwanza, yupo Sweden anafamilia kule na hana mpango wa kuja kuishi Tanzania. Wa pili yupo Canada, tayari ana maisha yake na mipango yake. Huyu Katrina ni mzito kidogo kwenye biashara, japo kwa mbali naona anaelekea. Ni yeye pekee ndio anayenipa tumaini. Mimi sio mtabiri, ila ikitokea nimefariki haitochukua miaka miwili, biashara zangu nazo zitakufa".

Analyse: "Kama ukijaribu kuwashawishi hao wanao wanaweza kurudi Tanzania ili waendeleze biashara zako"

Mr. B: "Sio rahisi kama unavyodhani"

Kabla sijamjibu, akaendelea:

"Unajua zamani tulikuwa tunapenda watoto wa kiume kuliko wa kike. Unajua kwanini?"

Analyse: "Iko wazi, mtoto wa kiume ndio atakayeendeleza ukoo. Wakike yeye akishaolewa sio wako tena"

Mr. B: "Ni kweli usemacho, lakini kuna ukweli mchungu ambao wala hausemwagi"

Analyse: "Ukweli upi"

Mr. B: "Huyo anayeendeleza ukoo pindi akishaoa mwili unabaki kwenye ukoo, ila moyo na akili yake havitokuwa na ukoo tena. Na yule ambaye umesema akishaolewa anakuwa sio wa ukoo tena, moyo wake utaendelea kuwa na familia"

Analyse: "Unajaribu kusema nini?"

Mr. B: "Ukiwa na watoto wakike kwenye familia ni Baraka kubwa sana tofauti na tulivyokuwa tukiamini. Watoto wangu wakiume wote hakuna anayetaka kurudi Tanzania, ila sio kwa mapenzi yao. Bali ni ushawishi toka kwa wanawake zao. Hivi kuna faida gani mtu kuendeleza ukoo alafu yuko maili nyingi sana kutokea ulipo?"

Akaendelea:

"Nina watoto watatu, ila hao wawili sijawaona kwa miaka mingi sasa, na sioni dalili za wao kurudi hivi karibuni. Natamani ningekuwa na wakike mwingine wakusaidiana mawazo na Katrina, ila ndio hivyo kwa umri huu siwezi ongeza mtoto mwingine. Ndio maana nampenda sana huyu last born wangu"

Nilibaki kimya maana nilikosa cha kusema, aliongea kwa uchungu sana kuonesha namna gani ilo jambo linamtatiza.

Sikuendelea kukaa sana pale, niliamua kumuacha maana nilihisi anahitaji muda wa peke yake.

Nikamuaga kwamba nataka kuondoka, akaniruhusu niende. Tofauti na siku zingine, hii siku hakutaka kabisa kunisindikiza. Na Mimi nilimuelewa.

Ila aliniacha na maswali mengi sana kichwani mwangu..

***** ***** ***** *****

Soma muendelezo hapa: Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri
 
Ni leo tu asubuhi kuna sehemu tulikuwa tunajadili utofauti wa watoto wa kike na wa kiume, basi tu wengine tulishaleta hiyo midume ila watoto wa kike ni mali sana hauadhiriki, Mzee kaongea kitu muhimu, muendeleza ukoo kimwili ila moyo uko kwingine, huyu moyo uko karibu ila mwili uko mbali yupo bora!
 
Bro I am learning a great deal from your experience in life. I want to say your actions will shape the next phase of my life. Life is calling me to act now. Thou, I got no experience in my own bussiness and don't have an ideal what it will be but I will try. I will learn along the way.
Umekua na life experience kama ya INSIDER MAN. We are learning through your experience bro.
 
Back
Top Bottom