Portion 22:
.....Siku mbili tokea niondoke kwa kina Katrina, nilipokea msg kutoka kwake:
Katrina: "Mambo?'
Mimi: "Poa tu, unaendeleaje?"
Katrina: "Hivyo hivyo tu"
Mimi: "Changamoto ni nini sasa hivi? Bado maumivu ni makali?"
Katrina: "Hapana, now ni kama period ya kawaida"
Mimi: "Hongera unaendelea vizuri. Sasa shida ni nini?"
Katrina: "Home bado wanaongea sana, hasa Mzee"
Mimi: "Wape muda, watakuwa sawa tu. Jamaa yako yeye anasemaje?"
Katrina: "Huyo bado sijakwambia, nasubiria tuonane ana kwa ana. Sijui nae atachukuliaje"
Mimi: "Kwani alikuwa anajua kama una mimba?"
Katrina: "Hapana"
Mimi: "As long as hakuna complication yoyote kwa upande wako, sioni haja ya kumwambia. Inaweza kuibua mengine"
Katrina: "Nisipomwambia alafu ikatokea akajua, itaniletea sana shida mbeleni"
Mimi: "Kwani kuna mtu yeyote tofauti na familia yako uliowaambia ili jambo?"
Katrina: "Hakuna"
Mimi: "Kama upo serious na mtu wako na unahitaji uendelee kuwa nae, basi hii ifanye kuwa siri yako. Hata best yako unayemuamini sana usimwambie. In short kufa nayo tu"
Katrina: "Okay sawa. Ratiba yako ipoje leo?. Niko bored, sitaki kushinda home leo"
Mimi: "Kuna vitu vya kusafiri navyo nataka nikanunue. Hivyo nitakuwa busy kidogo leo na kupack"
Katrina: "Unasafiri kwenda wapi?"
Mimi: "Naanza likizo, so naelekea kijijini mara moja"
Katrina: "Okay best, likizo njema".
Convo ikaishia hapo, nikaendelea na ratiba zangu.
***** ***** ****** ***** ***** ******
Baada kadhaa mbele nikaanza safari ya kwenda nyumbani kijijini. Mpaka ufike kwetu, mwendo si haba maana ni parefu.
Ila hatimaye nikafika.
Kwavile nazijua akili za Mshua, ikabidi niwe na taadhari hasa wakati nakaribia home. Nikasukuma geti lao la mbao, huku naangalia pande zote kuona kama Mshua yupo karibu. Kipindi Mimi nimekazana kuangalia mbele, kumbe Mshua alikuwa nje ya geti. Nilivyoingia, na yeye akaanza kunifata mdogo mdogo kwa nyuma huku ameinama kidogo, mikono kaitanguliza mbele kama vile anataka kurukia kitu. Kabla sijageuka vizuri akanirukia na kunivamia maeneo ya kiuno, wote tukaenda chini.
Nataka kugeuka ili tuangaliane uso kwa uso, akawahi kunipiga kabali. Nashindwa hata kujibu mashambulizi, maana Mshua ameshakuwa mtu mzima sana. Ila kipindi Mimi najitahidi kuepusha shari ila yeye yupo serious, ndio kwanza anakaza mikono.
Mara nikamsikia Bi Mkubwa anapiga kelele kutokea ndani: "Hivi nyie huwa mnashida gani?"
Hatujakaa sawa, akatumwagia ndoo nzima ya maji. Maji yalikuwa ya baridi, ukiongezea na baridi la kule kijijini, nilihisi mwili una ganda. Japo mwili ulikuwa unatetemeka kwa baridi, ila nilishukuru kwa kile kitendo, maana kiliniepushia dhahama.
Bi Mkubwa akawa analalamika pale peke yake, Mimi na Mshua kila mmoja akaingia ndani kivyake. Baada ya kubadili nguo, tulivyokuwa sebleni Bi Mkubwa akatufata:
Bi Mkubwa: "Hivi haya mambo yenu mtaacha lini lakini? Kwanini kila ukija lazima amani itoweke kwa muda hapa nyumbani?"
Mimi: "Sasa hapo kosa langu nini? Mimi nimekuja kwetu, ila nimepokewa kwa vurugu"
Mshua: "Muhuni anapokelewa kihuni"
Bi Mkubwa: "Sasa mkiumia itakuwaje? Au ndio mnajitafutia gharama za matibabu na kutusumbua wengine?"
Mshua: "Wewe si ndio ulimwambia aje?"
Bi Mkubwa: "Kwani haruhusiwi kuja?. Hapa ni kwao"
Mshua akaondoka sebleni na kutuacha wenyewe.
Bi Mkubwa: "Hebu jaribu kumuelewa Baba yako, mbona unamfanyia hivi lakini?"
Mimi: "Hivi kwani yeye alilazimishwa kuoa? Muda ukifika nitaoa"
Bi Mkubwa: "Muda upi unaousubiria? Kazi unayo, kipato unacho, afya unayo, kipi kingine unachosubiria?"
Mimi: "Mwanamke ninae Mama na nitamleta, ila nipeni muda kwanza"
Bi Mkubwa: "Hebu jitahidi umlete, inabidi uwe na familia sasa. Hivi hujachoka kuishi peke yako?
Mimi: "Sawa nitamleta, ila hii namna mliyonipokea nayo wala sio nzuri"
Bi Mkubwa: "Binadamu wote huwa tunapenda, ila tunatofautiana kwenye namna tunavyoonesha upendo wetu kwa wale tuwapendao. Niamini mimi, Baba yako anakupenda sana."
Mimi: "Hata kama, ila hii namna yake ya kuonesha upendo Mimi sijaridhika nayo"
Bi Mkubwa: "Kuna siku utamuelewa tu, ngoja na wewe uwe na familia yako"
Mimi: "Ila alichofanya sio sawa. Sijui kwanini unasimama upande wake kwenye ili"
Bi Mkubwa: "Yeye ni mume wangu, hivyo katika jambo lolote inabidi nisimame upande wake"
Mimi: "Ila na Mimi ni mwanao"
Bi Mkubwa: "Wala sijakataa, wewe ni mwanangu".
Mimi: "Pia usisahau nimekaa kwenye ilo tumbo miezi 9"
Bi Mkubwa: "Na hata baada ya miezi 9, uliendelea kuwa chini yangu mpaka ulipopata akili. Ila baada ya hapo ukaondoka, na ndani ya mwaka naweza nikakuona mara moja au nisikuone kabisa. Ila Baba yako hajawahi kuwa mbali na Mimi kwa zaidi ya mwezi, siwezi kutema big g kwasababu ya punje moja ya karanga, hivyo lazima niwe upande wake tu"
Mimi: "Ila Mama....."
Bi Mkubwa: "Hebu kapumzike kwanza basi, mengine tutaongea baadae"
Nikageuka ili nitoke sebuleni, nakutana na Mshua uso kwa uso anachungulia tulipokuwa na bi mkubwa. Mshua alikuwa anatabasamu, tulivyokutanisha macho akakunja sura. Inaonekana yale maneno ya Bi Mkubwa ni kama vile yalimkosha, ila alivyoniona akajifanya kuvunga. Mshua soon anatimiza miaka 70, ila mbele ya Bi Mkubwa utadhani ndio penzi jipya, maana anapenda sana attention yake. Nikaishia kucheka tu.
Bi Mkubwa akaenda zake jikoni, nikaingia chumbani kwangu.
****** ****** ****** *********
Wiki ile ile ambayo nilifika kijijini, kuna siku Katrina alinipigia simu:
Katrina: "Mambo best"
Mimi: "Poa tu, niaje?"
Katrina: "Safi tu, likizo inaendaje?"
Mimi: "Huku utulivu mwingi. Vipi mjini huko?"
Katrina: "Huku panazidi kuwaka moto tu"
Mimi: "Mpaka leo Mzee hajapoa tu?"
Katrina: "Anataka bf wangu aje home"
Mimi: "Sasa hapo shida iko wapi?"
Katrina: "Mzee namjua, lazima atataka kujua kwanini ameruhusu nikatoa mimba"
Mimi: "Jamaa kwani si hajui?"
Katrina: "Hajui, na ndio maana nahofia yataibuka mengine"
Mimi: "Ila sidhani kama Mzee anaweza kumuuliza ilo jambo, maana si atakuwa na ndugu wengine?"
Katrina: "Mzee anataka kuonana nae kwanza kabla ya kuja rasmi"
Mimi: "Mzee wako kumbe nae mkuda kiasi hicho?"
Katrina: "Acha tu"
Mimi: "Tokea nimefika huku sijawasiliana nae, ngoja nitampiga. Pia nitajaribu kuingizia na issue yako, akieleweka nitamuweka sawa"
Katrina: "Mmh sawa, ila sidhani maana nimejaribu kuongea nae sana"
Mimi: "Okay sawa".
Tukaishiana hivyo.
Ila kiukweli kibarua nilichojipa kilikuwa ni kikubwa sana. Niliangalia namna ninayoweza kutumia kumuingia Mr. B ila nikakosa. Jambo nililichukulia kirahisi, ila halikuwa rahisi.
Nakumbuka nilipompigia Mr. B tuliongea vitu kadhaa, ikiwemo yeye kuniomba radhi maana ile siku ya mwisho tunaonana hakuwa sawa. Mwisho wa maongezi nikajaribu kumuingizia na issue ya Katrina. Alinisikiliza kwa muda mrefu bila kuongea kitu, na kadiri alivyokuwa kimya nikajikuta nazidi kubwabwaja. Maana ukimya wake uliniondolea utulivu. Baada ya ukimya wake, jibu alilotoa ndio lilinikata moto:
Mr. B: "Hii ni familia yangu, hakuna mtu anayeweza kuniambia namna gani ya kuiendesha".
Mimi: "Nisamehe kama hiyo ndio tafsiri uliyoipata Mzee, ila nilikuwa najaribu kumsaidia tu. Mimi na yeye hatuna mazoea, ila mpaka ameniambia ili jambo maana yake hakuwa na option. Na ndio maana nikalipa uzito"
Mr. B: "Ukiweza kutambua mipaka yako, life will be easier sana"
Mimi: "Nisamehe sana Mzee wan...."
Mr. B: "Leave my family out of our conversation Amphibian"
Sikuona kama ni busara kuendelea na haya mazungumzo. Ikabidi nimuage, kisha nikakata simu.
Lakini pamoja na yote, ila kwa namna fulani nilochoongea alikitilia maanani. Maana kwa maelezo aliyokuja kunipa Katrina ni kwamba Mr. B alipotezea swala la kuonana na bf wa Trina peke yake. Badala yake aliruhusu waje rasmi, hivyo siri ya Trina iliendelea kutunzwa.
Kwa upande wangu likizo iliendelea vizuri bila purukushani zozote.
Nikiwa naianza wiki ya pili tokea niwe pale nyumbani siku moja mida ya saa tano natoka shamba kuangalia migomba na mazao mengine, nikakuta missed calls mbili toka kwa Mzee wa Kongowe, na msg moja toka Mr. B.
Msg ya Mr. B ilisema hivi : "Habari za asubuhi Amphian, call me once you're free"
Nikabaki najiuliza, kuna nini?. Mzee wa Kongowe ndiye aliyeniunganisha na Mr. B. Sijawasiliana nae muda mrefu, alafu leo nakuta missed zake, na muda huo huo kuna msg ya Mr. B akitaka nimpigie. Je, wanataka kuniambia kitu moja? Mbona wamenitafuta wakati sawa?
Nianze kumtafuta yupi kati yao? Nikaona hakuna haja ya kufanya jambo jepesi lionekane gumu, nikaamua kumpigia Mzee wa Kongowe
Mimi: "Mzee Shikamoo"
Mzee: "Marahaba, habari za siku kijana?"
Mimi: "Safi tu"
Mzee: "Uko wapi sasa hivi?"
Mimi: "Nimekuja kijijini, nipo likizo"
Mzee: "Aisee, mjini unarudi lini?
Mimi: "Baada ya wiki mbili. Vipi Kuna jambo lolote Mzee?"
Mzee: "Yeah, ila ingependeza sana kama ungekuwa mjini"
Mimi: "Jambo gani Mzee?"
Hakunijibu swali langu, badala yake akaniuliza kitu kingine:
Mzee: "Bado una mawasiliano mazuri na Mr. B?"
Mimi: "Ndio, na kabla sijakupigia wewe nimekuta msg yake akisema nimpigie nikiwa free"
Mzee wa Kongowe akaniambia kwa sauti ya ukali kidogo:
"Sasa unapoteza muda wa nini kuongea na Mimi?. Hebu mpigie sasa hivi"
Kisha akakata simu ili kunipa nafasi ya kuongea na Mr. B.
Akazidi kuniacha na maswali mengi zaidi. Maana tafsiri niliyoipata ni kwamba kitu alichotaka kuniambia yeye kwa namna fulani kinawiana na anachotaka kuniambia Mr. B.
Pale pale nikampigia simu Mr. B:
Mimi: "Mzee Shikamoo"
Mr. B: "Marahaba. Nilishindwa kukupigia, sikutaka kukuharibia mapumziko yako"
Mimi: "Usijali Mzee."
Mr. B: "Likizo yako inaisha lini?"
Mimi: "Baada ya wiki mbili"
Akawa kimya kidogo kama mtu anayetafakari jambo. Kisha akaongea:
Mr. B: "Nataka tuonane kwa ajili ya jambo fulani. Unaweza kuwahi kidogo?"
Mimi: "Yeah naweza, lini unahitaji tuonane?"
Mr. B: "As soon as you can"
Mimi: "Hakuna shida Mzee. Baada ya wiki nitakuwa huko"
Tukamalizana hivyo, nikakata simu.
Waliniacha na maswali mengi sana yasiyo na majibu.
** **** ***** ***** ***** *****
Mida ya jioni nikiwa nimekaa na Mshua, ikabidi nimshirikishe hii habari walau nipate mtazamo wake.
Mshua: "Hebu nione hiyo msg aliyokutumia"
Alivyoisoma ile msg akaniuliza:
"Mbona sijaelewa. Huyu Amphibian ni nani?"
Mimi: "Amezoea tu kuniita hivyo"
Mshua: "Kwamba halijui jina lako mpaka akupe jina jingine?"
Ikabidi nimuelezee jinsi ilivyokuwa kuhusu lile jina. Akabaki ameniangalia kana kwamba ni kijana niliyepotea.
Mshua: "Kuna haja ya kuja huko unapoishi nikae hata wiki. Una mambo mengi yanayotia mashaka"
Mimi: "Ilo ni jina tu halina maana yoyote Mzee"
Mshua: "Hivi kuna siku itafika uwe na mke wewe?"
Yani Mshua kwenye kila mada lazima atafute namna ya kuingizia ishu za kuwa na mke.
Mimi: "Sasa hayo yametokea wapi?"
Mshua: "Kwahiyo hayana maana? Nilikupeleka kanisani ukabatizwa, ila umefika mjini unajipa majina ya ajabu ajabu"
Ikabidi nikae kimya kwanza, maana kadiri nitakavyomjibu na yeye ndivyo atavyopandisha hasira. Baada ya kuona nipo kimya, akarudi kwenye mada yetu:
Mshua: "Kwahiyo lini unaenda kuonana nae?"
Mimi: "Wiki ijayo itabidi niende, mapumziko yangu nitamalizia kule"
Mshua: "Umeachiev vitu gani kwenye maisha yako hadi unajihisi unahitaji mapumziko?"
Mimi: "Haya ni mapumziko ya kawaida tu kwa kila mtumishi Mzee. Hayahusiani na kuachiev chochote"
Mshua: "Mnapewa likizo ili mkaitumie kufanya mambo yenu mengine na sio kuja kujificha kijijini. Kesho fanya urudi town. Nenda kaonane nae haraka"
Mimi: "Ila nimeshaongea nae, tumekubaliana baada ya wiki"
Mshua: "Yule sio ndugu yako, huwezi jua anakuitia nini. Kama kuna opportunity usidhani akitokea mtu wake wa karibu ataendelea kukusubiria wewe utoke mafichoni. Huna unachofanya huku, fanya uende"
Mimi: "Huku ni kwetu Mzee, sijaja kujificha"
Kipindi tupo kwenye hayo mazungumzo, Bi Mkubwa nae akawa amaengia. Mshua akamuelezea tulichokuwa tunajadili na maamuzi tuliyofikia ya Mimi kuondoka.
Mama hakuwa na hiyana, aliridhia. Akaanza kunipa mawaidha yake kama siku zote.
Bi Mkubwa: "Ila usiache kusali mwanangu, kuna nguvu kubwa sana kwenye maombi "
Mshua: "Mjini anajiita Amphibian, unategemea atakumbuka kusali?"
Mimi: "Nasali sana Mama, ni vile Mungu bado hajaamua kutupa. Muda ukifika naamini kila kitu kitakuwa sawa"
Bi Mkubwa: "Yawezekana unasali, ila unasali inavyotakiwa?"
Kabla hata sijajibu, Mshua akaingilia tena:
Mshua: Midomo hii hii wanayoitumia kunyonyeana sehemu za siri ndio wanaitumia kumuomba Mungu?"
Hii kauli ilinikata sana. Haikuwa mara ya kwanza kumsikia mtu akisema hivi, na mara zote imekuwa ikinigusa.
Sikutaka kujibu chochote. Kulikuwa na uzito kwenye alichosema.
** * **
Kesho yake mapema asubuhi nilikuwa ndani ya bus narudi mjini. Nilikuwa tayari kwenda kuonana na Mr. B.
Sikuwa najua kwanini yeye na Mzee wa Kongowe walitaka nirudi haraka mjini.
Ila nilijifunza jambo moja kubwa sana, fursa inapogonga hodi mlangoni kwako. Usijifikirie mara mbili. Opportunities never knock the same door twice. Ukiacha fursa zikupite, kuna wengine watazipokea na kuzikumbatia kiasi kwamba hutoziona tena.
Mpaka muda huu ninaoandika maneno haya, namshukuru sana Mshua kwa kuniambia niwahi kwenda mjini. Alikuwa sahihi sana. Mungu aliposema alimuumba binadamu kwa mfano wake, naamini binadamu aliyekuwa anazungumziwa ni Mshua wangu, live long Mzee.
Huu ulikuwa ni wito ambao ulienda kufungua ukurasa mwingine mpya kwangu.
Fursa iliyonipa tumaini jipya.
Uzuri ni kwamba ilinikuta nikiwa tayari. Tayari kwa New Life Chapter.
Chapter ambayo panapo majaaliwa, pengine naweza kuja kuandika humu jukwaani. Ila kwasasa, naomba niishie hapa.
** *** ***** ***** ***** *****
Kufikia hapo, naomba nihitimishe usimuliaji. Ila ningependa kuwaacha na msemo mmoja:
"Njia sahihi ya kutabiri mafanikio yako yajayo, ni kujiandaa vizuri. Mafanikio yako ni zaidi ya cheti".
Mpaka wakati mwingine.
Regards,
Analyse.