Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri

Portion 05.

....Kitendo cha Ester kuniruhusu niende kilinipa nguvu kubwa sana. Nilijiapia kwamba tukishasuluhisha mambo yetu, sitokaa nifanye ujinga tena. Nitajitahidi kadiri niwezavyo kumfanya awe na amani. Safari hii nilidhamiria kubadilika haswa.

Haikuwa mara ya kwanza Mimi kwenda kwao, hivyo nilikuwa napajua. Nilibeba mazaga zaga kama kawaida, sikutaka kwenda mikono mitupu.

Wakati nikiwa njiani niliblock namba zote za mashangazi na wale wote niliohisi wanaweza kuniharibia. Msg na ushahidi wote ambao ungeweza kuleta kizaa zaa nikafuta. Ila bado nikawa sina amani kabisa, ikabidi nizime simu. Sikutaka surprise ya aina yoyote siku ile.

***** ***** ***** ***** ***** ******

Nikaenda moja kwa moja mpaka kwakina Ester. Nikapokelewa vizuri tu. Ester anashangaa mbona sijampigia hata simu aje kunipokea stand. Mama ake akamwambia asiniulize maswali mengi, wanashukuru nimeshafika salama.

Ikabidi nimwambie Ester kuwa simu yangu ilikata chaji ndio maana sikuweza kumpigia pindi nilipofika.

Tukiwa sebleni pale, nikampa Ester simu yangu akaenda kunichajia chumbani kwake. Baada ya kuwa tumemaliza kula, kikao chetu kikaanza.

Mama akatusema pale, alafu mwisho wa siku akasema anatuacha tuwekane sawa, yeye anaenda kufanya shugulli zingine. Nikaona endapo bi mkubwa ataondoka, basi Ester atanikazia tu maana namjua vizuri sana. Ikabidi nimuombe Mama aendelee kuwa na sisi hadi tufikie muafaka.

Muda wote ambao tulikuwa pale sebleni, simu ya Ester ilikuwa inaita sana, na msg zikawa zinaingia mara kwa mara. Akili yangu ikaniambia atakuwa ameshapata mtu mwingine na ndio maana inakuwa ngumu kwake kunirudia.

Nikajikuta napatwa na wivu.

Pia nikataka kuitumia ile iwe kama sababu ya kumuonesha kwanini hataki turudiane.

Mimi: "Mbona hupokei simu? Maana inaita muda mrefu".

Ester: "Hapa tupo kwenye kujadili mambo yetu, tukianza kuruhusu simu , hatutomaliza leo"

Mimi: "Pokea kwanza simu ili tuweze kuendelea kwa amani"

Ester: "Simu haihusiani na sisi, tuongee yetu"

Mimi: "Nilijua tu kuna mtu ndio anakuzuzua. Hata hii kuachana kwetu nilijua lazima kuna mtu ndio anakushawishi. Ulikuwa unanitafutia sababu tu"

Ester: "Nakuheshimu sana, na sijawahi kukuvunjia heshima. Ila naona umefika mbali sasa"

Mimi: "Wewe ndio unayetaka tufike mbali. Mbona hutaki kupokea hiyo? Pokea alafu weka loud speaker wote tusikie. Mama siunaona Ester alivyo?"

Mama: "Hebu tulieni basi, tuongee kwa utaratibu kama tulivyoanza ili tuelewane"

Ester: "Mama naomba utupishe kidogo tuongee wenyewe"

Mimi: "Mama naomba usiondoke maana wewe ndio umeitisha Iki kikao, inabidi ujue yote yanayondelea mpaka mwisho"

Ester alinikata jicho kali sana. Nikaona nimemshika pabaya.

Ester: "Mama naomba utupe dakika tano tu, alafu utarudi. Nakuomba sana Mama angu"

Bi mkubwa hakuwa na hiyana, akatupisha. Tulivyobaki wenyewe, Ester akaniambia kwa sauti ya chini ila iliyojaa hasira:

Ester: "Uliniambia simu yako imezima chaji ila nilivyoichomeka imeonesha ina 44%. Maana yake haikuzima, bali ilizimwa. Simu yako nimekuwekea kwenye chaji, ila laini zako nimeziweka kwenye simu yangu. Hivyo hizi msg zote na simu unazozisikia ni za kwako, upo tayari nipokee na kuweka loud speaker au hizi msg tuzisome wote?"

Moyo ukalia Pa!. Niliganda kwa muda bila kujua niongee nini. Alafu muda huo Ester kanikazia macho ananiangalia ninavyobabaika. Hatukukaa muda, simu ikaita tena. Ester akaipokea na kuweka loud kweli.

Aliyepiga: "We mtoto siku hizi unaringa sana utadhani una mbo.o ya almasi. Leo unakuja au mpaka nikufate kama jana?"

Ester akamkatia simu, Mimi nikabaki nimejiinamia tu kwa aibu.

Ester: "Yani jana umetoka kulala na mwanamke mwingine, alafu leo unakuja kuniomba msamaha. Hivi huna aibu wewe? Una uhakika hujarogwa?"

Nikabaki kimya!

Ester: "Vipi tusome na msg kwa sauti kama ulivyotaka?"

Nikaendelea kubaki kimya tu.

Ester: "Mama yangu anakupenda sana , Yani kuliko kawaida, nisingependa ajue kila kitu kuhusu migogoro yetu maana itamvunja sana moyo, na hatoweza kukuchukulia tena kama mwanzo. Yeye anaamini tunaweza kusuluhisha na kuendelea kuwa pamoja, ila ni Mimi ndiye nitakayetakiwa kuishi na wewe, na Wala sio yeye. Hivyo maamuzi bado yanabaki kwangu. Jana umetoka kulala na mwanamke mwingine, leo umekuja kuomba msamaha. Iko wazi kwamba it won't work between us, kwanini usikubaliane na hali tu?".

Nilikuwa kwenye situation kama ya Steven Gerrard alivyoteleza na kubaki anamuangalia Demba Ba anaenda kufunga goli lililowanyima ubingwa Liverpool. Sikuwa na utetezi wowote, kila kiungo cha mwili wangu kikakubaliana na ukweli kwamba Ester sio wangu tena. Hakuna namna ya kuweza kumrudisha.

Sikuona haja ya kuendelea kuongea tena, hapakuwa na cha kuongea. Ameshanipa countless chances ila zote nazingua.Nikaamua nimuache pengine atakuja mtu anayemfaa, Mimi nilishashindwa.

Nikamuaga Bi mkubwa kwamba naondoka. Bi Mkubwa ananiuliza "Mmefikia muafaka mwanangu?" . Jibu nililompa "Amesema nimpe muda kidogo atanitafuta akishatulia"

Bi Mkubwa: "Sawa mwanangu, kila kitu kitakuwa sawa"

Nikaaga kisha nikatoka.

Safari ya kutoka kijijini kwao mpaka Dar niliiona ndefu kuliko route ya Songea - Kigoma. Nilikuwa stressed kuliko kawaida yani. Njia nzima mpaka nafika Dar nilikuwa na sikiliza wimbo mmoja tu, Let Her Go wa Passenger. Kiasi kwamba sasa hivi nikisikia chorus ya ule wimbo, nakua nishajua verse inayofuatia ni ipi hata kama niliukutia kati.

Siku zote nilikuwa najitahidi kumtoa Ester kwenye maisha yangu, sasa hivi ameamua kutoka najikuta nabaki na maumivu makali kuliko kawaida. Sikuwahi kumpa umuhimu kama alionipa yeye. Nimeanza kumpenda kipindi ambacho yeye ameshazichoka tabia zangu.

Ujio wake kwenye maisha yangu ulileta mabadiliko mengi sana mazuri ila sikutaka kuyaona. Sasa hivi hayupo ndio nakumbuka kila kitu kuhusu yeye.

Niliwaza mengi sana wakati nipo ndani ya bus.

Kufika Dar, nakuta napo hakujapoa. Hazikupita siku mbili nikashikwa tena na polisi. Nikajikuta nakosa amani.

Nikaanza mtindo wa kila siku naenda zangu beach kupoteza time na kutuliza akili. Nilizunguka beach zote za Dar, mpaka ile siku nakutana na Evervess pale Rongoni na kunisimulia mkasa wake (hii ni ile story iliyoondelewa jukwaani).

Siku niliyoachana na Evervess, usiku sikupata usingizi kabisa. Niliwaza mambo mengi sana kuhusu maisha yangu. Nilijaribu kuangalia faida na hasara zilizotokana na mashangazi, nikakuta hasara ni nyingi mno kuliko faida. Nimepoteza hela nyingi sana, nguvu na muda kwa hawa wamama, ila sina cha maana zaidi ya kuzunguka kwenye restaurant za kishua au kupanda magari makali na shopping. Kinyume na hapo ni hasara tu.

Imagine mfano nilifunga safari toka Dar mpaka Kijiji kimoja kipo Mbulu kinaitwa Masieda kumfata Mwahija. Na kule isingekuwa busara za yule mwenyekiti wa kile kijiji pengine ningefia kule. Wambulu sio poa wale watu.

Ukiachana na huyo, nishapoteza deals nyingi sababu ya wamama. Huyu mkurya anayeniwinda, nae kisa ni mwanamke.

Hapa ndio kwa moyo wa dhati nikaona Mimi na mashangazi basi sasa. Nahitaji kufocus kisha nijijenge upya. Nikaanza kumuomba Mungu kwamba endapo nitatoka kwenye huu msala niliopo sasa salama, basi sitochezea tena nafasi yoyote nitakayoipata.

Wanasema pombe inarudisha nyuma maendeleo ya mnywaji, ila nadhani mapenzi yanashika namba moja. K inatia sana hasara, hasa ukijifanya wewe ni msingi kiuno.

Akili ikaanza kuniambia nibadilishe simu na laini kabisa, ili nianze upya. Lakini imekuwaje mpaka nikawa kwenye huu msala wa sasa na polisi kiasi cha kufikiria kubadilisha laini ya simu?

Turudi nyuma kidogo uone jinsi mashangazi walivyoniharibia sana mipango yangu na kuniweka kwenye hii situation. Pengine unaweza kuelewa kwanini niliamua kuachana na mambo ya mashangazi. Maana ilifikia hatua nikahama Jiji la Dar.....

****** *******

Soma next portion hapa:

Niltaka nkaoge,,ila wacha ikae kuoga sio lazma
 
Na wewe ulipaka mafuta ya nazi ukatulia tuli kumsubiri virgin kama mtoa uzi?
Hapana, manzi alikuwa anajielewa sana, ni aina flani ya wale mamanzi wajuaji, yupo abroad sasa.

Yeye ndiye alipanga mwenyewe, hivyo mi nilikua mfuata maelekezo, just imagine it took two days, ilikuwa ni taratibu sana...
 
Tatizo raia mnakuwaga na jazba sana majukwaani, hamtaki story ichelewe au dharura isitokee.
Labda kwa wasiokufahamu ila wengi huwa tunajua Aposto ni mtu wa maneno yako na huwa unarusha kwa interval ulizodhamiria siku zote. Labda itokee lishangazi limekufuata inbox likakubembeleza ukalainika na kutupatia bonus portion 😀 😀 (kidding).

Wewe tupia story kwa muda na nafasi yako mengine tuachie wasomaji tutafsiri wenyewe.
Story zako huwa nazirudia mara kwa mara kila nipatapo muda sababu zinafurahisha na kufundisha vile vile.
 
Pamoja sana mkuu 👊👊
 
Back
Top Bottom