Kapeace
JF-Expert Member
- May 26, 2017
- 24,514
- 65,521
Sahihi kabisaKuna makosa inabidi yatokee ili tupate kujifunza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sahihi kabisaKuna makosa inabidi yatokee ili tupate kujifunza
Haya 🤝Nilishaiuza, kwahiyo sitoweza kuiweka tena jukwaani.
freeeesh tu!Vijana wa mjini wanasema uwe tayari kwa kila hali, ukiitwa madame sawaaa, shangazi sawaaa mwengine anamalizia na kukuita mama kabisaaa😆😆😆
ila esther!
AH SUBUTHUUUU!Kwamba mume alikurudisha kwenu? 😅

Miss u...Shukrani Analyse nipo apaa [emoji6] vitu anavyopenda shunie hiviii
😇😇😇😇🤣🤣🤣🤣🤣🤣Portion 05.
....Kitendo cha Ester kuniruhusu niende kilinipa nguvu kubwa sana. Nilijiapia kwamba tukishasuluhisha mambo yetu, sitokaa nifanye ujinga tena. Nitajitahidi kadiri niwezavyo kumfanya awe na amani. Safari hii nilidhamiria kubadilika haswa.
Haikuwa mara ya kwanza Mimi kwenda kwao, hivyo nilikuwa napajua. Nilibeba mazaga zaga kama kawaida, sikutaka kwenda mikono mitupu.
Wakati nikiwa njiani niliblock namba zote za mashangazi na wale wote niliohisi wanaweza kuniharibia. Msg na ushahidi wote ambao ungeweza kuleta kizaa zaa nikafuta. Ila bado nikawa sina amani kabisa, ikabidi nizime simu. Sikutaka surprise ya aina yoyote siku ile.
***** ***** ***** ***** ***** ******
Nikaenda moja kwa moja mpaka kwakina Ester. Nikapokelewa vizuri tu. Ester anashangaa mbona sijampigia hata simu aje kunipokea stand. Mama ake akamwambia asiniulize maswali mengi, wanashukuru nimeshafika salama.
Ikabidi nimwambie Ester kuwa simu yangu ilikata chaji ndio maana sikuweza kumpigia pindi nilipofika.
Tukiwa sebleni pale, nikampa Ester simu yangu akaenda kunichajia chumbani kwake. Baada ya kuwa tumemaliza kula, kikao chetu kikaanza.
Mama akatusema pale, alafu mwisho wa siku akasema anatuacha tuwekane sawa, yeye anaenda kufanya shugulli zingine. Nikaona endapo bi mkubwa ataondoka, basi Ester atanikazia tu maana namjua vizuri sana. Ikabidi nimuombe Mama aendelee kuwa na sisi hadi tufikie muafaka.
Muda wote ambao tulikuwa pale sebleni, simu ya Ester ilikuwa inaita sana, na msg zikawa zinaingia mara kwa mara. Akili yangu ikaniambia atakuwa ameshapata mtu mwingine na ndio maana inakuwa ngumu kwake kunirudia.
Nikajikuta napatwa na wivu.
Pia nikataka kuitumia ile iwe kama sababu ya kumuonesha kwanini hataki turudiane.
Mimi: "Mbona hupokei simu? Maana inaita muda mrefu".
Ester: "Hapa tupo kwenye kujadili mambo yetu, tukianza kuruhusu simu , hatutomaliza leo"
Mimi: "Pokea kwanza simu ili tuweze kuendelea kwa amani"
Ester: "Simu haihusiani na sisi, tuongee yetu"
Mimi: "Nilijua tu kuna mtu ndio anakuzuzua. Hata hii kuachana kwetu nilijua lazima kuna mtu ndio anakushawishi. Ulikuwa unanitafutia sababu tu"
Ester: "Nakuheshimu sana, na sijawahi kukuvunjia heshima. Ila naona umefika mbali sasa"
Mimi: "Wewe ndio unayetaka tufike mbali. Mbona hutaki kupokea hiyo? Pokea alafu weka loud speaker wote tusikie. Mama siunaona Ester alivyo?"
Mama: "Hebu tulieni basi, tuongee kwa utaratibu kama tulivyoanza ili tuelewane"
Ester: "Mama naomba utupishe kidogo tuongee wenyewe"
Mimi: "Mama naomba usiondoke maana wewe ndio umeitisha Iki kikao, inabidi ujue yote yanayondelea mpaka mwisho"
Ester alinikata jicho kali sana. Nikaona nimemshika pabaya.
Ester: "Mama naomba utupe dakika tano tu, alafu utarudi. Nakuomba sana Mama angu"
Bi mkubwa hakuwa na hiyana, akatupisha. Tulivyobaki wenyewe, Ester akaniambia kwa sauti ya chini ila iliyojaa hasira:
Ester: "Uliniambia simu yako imezima chaji ila nilivyoichomeka imeonesha ina 44%. Maana yake haikuzima, bali ilizimwa. Simu yako nimekuwekea kwenye chaji, ila laini zako nimeziweka kwenye simu yangu. Hivyo hizi msg zote na simu unazozisikia ni za kwako, upo tayari nipokee na kuweka loud speaker au hizi msg tuzisome wote?"
Moyo ukalia Pa!. Niliganda kwa muda bila kujua niongee nini. Alafu muda huo Ester kanikazia macho ananiangalia ninavyobabaika. Hatukukaa muda, simu ikaita tena. Ester akaipokea na kuweka loud kweli.
Aliyepiga: "We mtoto siku hizi unaringa sana utadhani una mbo.o ya almasi. Leo unakuja au mpaka nikufate kama jana?"
Ester akamkatia simu, Mimi nikabaki nimejiinamia tu kwa aibu.
Ester: "Yani jana umetoka kulala na mwanamke mwingine, alafu leo unakuja kuniomba msamaha. Hivi huna aibu wewe? Una uhakika hujarogwa?"
Nikabaki kimya!
Ester: "Vipi tusome na msg kwa sauti kama ulivyotaka?"
Nikaendelea kubaki kimya tu.
Ester: "Mama yangu anakupenda sana , Yani kuliko kawaida, nisingependa ajue kila kitu kuhusu migogoro yetu maana itamvunja sana moyo, na hatoweza kukuchukulia tena kama mwanzo. Yeye anaamini tunaweza kusuluhisha na kuendelea kuwa pamoja, ila ni Mimi ndiye nitakayetakiwa kuishi na wewe, na Wala sio yeye. Hivyo maamuzi bado yanabaki kwangu. Jana umetoka kulala na mwanamke mwingine, leo umekuja kuomba msamaha. Iko wazi kwamba it won't work between us, kwanini usikubaliane na hali tu?".
Nilikuwa kwenye situation kama ya Steven Gerrard alivyoteleza na kubaki anamuangalia Demba Ba anaenda kufunga goli lililowanyima ubingwa Liverpool. Sikuwa na utetezi wowote, kila kiungo cha mwili wangu kikakubaliana na ukweli kwamba Ester sio wangu tena. Hakuna namna ya kuweza kumrudisha.
Sikuona haja ya kuendelea kuongea tena, hapakuwa na cha kuongea. Ameshanipa countless chances ila zote nazingua.Nikaamua nimuache pengine atakuja mtu anayemfaa, Mimi nilishashindwa.
Nikamuaga Bi mkubwa kwamba naondoka. Bi Mkubwa ananiuliza "Mmefikia muafaka mwanangu?" . Jibu nililompa "Amesema nimpe muda kidogo atanitafuta akishatulia"
Bi Mkubwa: "Sawa mwanangu, kila kitu kitakuwa sawa"
Nikaaga kisha nikatoka.
Safari ya kutoka kijijini kwao mpaka Dar niliiona ndefu kuliko route ya Songea - Kigoma. Nilikuwa stressed kuliko kawaida yani. Njia nzima mpaka nafika Dar nilikuwa na sikiliza wimbo mmoja tu, Let Her Go wa Passenger. Kiasi kwamba sasa hivi nikisikia chorus ya ule wimbo, nakua nishajua verse inayofuatia ni ipi hata kama niliukutia kati.
Siku zote nilikuwa najitahidi kumtoa Ester kwenye maisha yangu, sasa hivi ameamua kutoka najikuta nabaki na maumivu makali kuliko kawaida. Sikuwahi kumpa umuhimu kama alionipa yeye. Nimeanza kumpenda kipindi ambacho yeye ameshazichoka tabia zangu.
Ujio wake kwenye maisha yangu ulileta mabadiliko mengi sana mazuri ila sikutaka kuyaona. Sasa hivi hayupo ndio nakumbuka kila kitu kuhusu yeye.
Niliwaza mengi sana wakati nipo ndani ya bus.
Kufika Dar, nakuta napo hakujapoa. Hazikupita siku mbili nikashikwa tena na polisi. Nikajikuta nakosa amani.
Nikaanza mtindo wa kila siku naenda zangu beach kupoteza time na kutuliza akili. Nilizunguka beach zote za Dar, mpaka ile siku nakutana na Evervess pale Rongoni na kunisimulia mkasa wake (hii ni ile story iliyoondelewa jukwaani).
Siku niliyoachana na Evervess, usiku sikupata usingizi kabisa. Niliwaza mambo mengi sana kuhusu maisha yangu. Nilijaribu kuangalia faida na hasara zilizotokana na mashangazi, nikakuta hasara ni nyingi mno kuliko faida. Nimepoteza hela nyingi sana, nguvu na muda kwa hawa wamama, ila sina cha maana zaidi ya kuzunguka kwenye restaurant za kishua au kupanda magari makali na shopping. Kinyume na hapo ni hasara tu.
Imagine mfano nilifunga safari toka Dar mpaka Kijiji kimoja kipo Mbulu kinaitwa Masieda kumfata Mwahija. Na kule isingekuwa busara za yule mwenyekiti wa kile kijiji pengine ningefia kule. Wambulu sio poa wale watu.
Ukiachana na huyo, nishapoteza deals nyingi sababu ya wamama. Huyu mkurya anayeniwinda, nae kisa ni mwanamke.
Hapa ndio kwa moyo wa dhati nikaona Mimi na mashangazi basi sasa. Nahitaji kufocus kisha nijijenge upya. Nikaanza kumuomba Mungu kwamba endapo nitatoka kwenye huu msala niliopo sasa salama, basi sitochezea tena nafasi yoyote nitakayoipata.
Wanasema pombe inarudisha nyuma maendeleo ya mnywaji, ila nadhani mapenzi yanashika namba moja. K inatia sana hasara, hasa ukijifanya wewe ni msingi kiuno.
Akili ikaanza kuniambia nibadilishe simu na laini kabisa, ili nianze upya. Lakini imekuwaje mpaka nikawa kwenye huu msala wa sasa na polisi kiasi cha kufikiria kubadilisha laini ya simu?
Turudi nyuma kidogo uone jinsi mashangazi walivyoniharibia sana mipango yangu na kuniweka kwenye hii situation. Pengine unaweza kuelewa kwanini niliamua kuachana na mambo ya mashangazi. Maana ilifikia hatua nikahama Jiji la Dar.....
Umepotea mwana lunyasi...😀😀Aiseee naanza kuamini ule msemo kwamba mwanamke atakuvumilia ila siku akiamua kwamba imetosha ndio basi tena harudi nyuma, wanaume wengi sijui kwanini wanashindwa kuliona hili halafu mwisho wa siku wakija kuangukia kwa magumegume wanaanza kutukana wanawake wote, kumbe wanasahau kuwa walishapata wanawake wazuri ili wakachezea nafasi kwa kudhani wanapendwa hivyo watavumiliwa milele
Unashangaa nini dada akee?😂Umepotea mwana lunyasi...😀😀
Mkuu hili lilishapangwa kwa wote hawa yani yeye na ester liwe funzo kwao, naamini Analyse kipo alichojifunza kwa alichopitia life is full of lessons everyday untill we die.Sasa na wewe unajua kabisa simu haijaisha chaji, na akiiweka chaji itasoma chaji iliopo, ulikua unatumia akil gani wewe?? Kwel kabisa unakwenda kutafuta suluhu kwa akil ya kizembe namna hii mkuu? Ya kwel haya au??
huo ndo ukweli.Aiseee naanza kuamini ule msemo kwamba mwanamke atakuvumilia ila siku akiamua kwamba imetosha ndio basi tena harudi nyuma, wanaume wengi sijui kwanini wanashindwa kuliona hili halafu mwisho wa siku wakija kuangukia kwa magumegume wanaanza kutukana wanawake wote, kumbe wanasahau kuwa walishapata wanawake wazuri ili wakachezea nafasi kwa kudhani wanapendwa hivyo watavumiliwa milele
ahahahhaah ila Esther ana akili sanaYeye ndio aliomba simu aniwekee chaji, na Mimi sikutaka kuresist ili asije hisi chochote. Ila mambo ndio yakaenda kunigeuka
hata kama mimi Analyse sikutajiii.After portion 05. Nadhani utaanza na visa vya mashangazi. Ningependa kuuliza kuhusu Ester , where is her? Is she married or not?
Mkuu Analyse
Kilikuja kwa ndege mkuu😆where is her?
where is she?
Asante mkuu.Sijui anapoishi kwasasa. Ila kuna kipindi baada ya kuwa nimetoka kule aliniomba tuonane maana nilikuwa namsumbua sumbua. Dhumuni la yeye kutaka tuonane ilikuwa ni kuniambia kwamba yupo kwenye harakati za kuchumbiwa.
From there tulionana mara kadhaa, na baada ya hapo sijawahi kujua alipo. Ile namba yake inapatikana endapo akitaka kunijulia hali tu, kinyume na hapo haipatikani.