Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri

Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri

Ila Ester mjanja sana nmependa akili yake...kitendo cha kuweka line zako kwenye simu yake alijua kukushika pabaya🤣🤣🤣🤣
Apo jamaa alizingua me singipata ujasir uwo wa kumpa cm yng akaweke chaj hata siku mmoja akili yng ingenambia angewasha cm na kupekura japo blcok list ila mdada alienda mbali zaidi akachomoa line na kueke kwenye cm yake kbs yaaan daah🤣
 
Tafiti zinasema mara nyingi mahusiano yetu ya kwanza ndio yana determine preference ya mahusiano yetu yatakoyofatia na mengine na mengine

Yaani unakuwa more free and comfortable kwa Aina hiyo ya watu

Swali kwako Mkuu, mahusiano yako ya kwanza yalikuwa na mtu ambaye amekuzidi umri.???
 
Tafiti zinasema mara nyingi mahusiano yetu ya kwanza ndio yana determine preference ya mahusiano yetu yatakoyofatia na mengine na mengine

Yaani unakuwa more free and comfortable kwa Aina hiyo ya watu

Swali kwako Mkuu, mahusiano yako ya kwanza yalikuwa na mtu ambaye amekuzidi umri.???
aliwahi eleza hapa kipindi fulani.
Huyu alianza harakati za maisha akiwa mdogo sana, very likely watu walikuwa wanamuona mkubwa so wakawa wanampa. Kumbe bw mdogo.
Ndo mana anapita mule mule

Comment yako imenikumbusha kitu niliambiwa na mama mmoja alisema wanaume wengi wakiwa vijana hujifunza ngono kwa wasichana wa kazi.
Kitu ambacho wanawake wengi hawakijui, wanaume wengi hawawadharau wadada wa kazi kwa ujumla wao kwa kuwa most of them ndiko walikojifunzia ngono.
Sasa mama mjengo we mtukane dada weeee, mwenzio anaona unatukana Mwalimu wake.
Mtese weeeee, mwenzio anaona unatesa mtu muhimu sana kwenye maisha yake

Na ndo mana hawaaaachi kuwala!
Nilifikiria vitu ving sana, nikaishia tu kucheka!
 
Ambacho sikujua ni kwamba yeye aliona vitu ambavyo Mimi sikuviona hapo kabla. Tena aliviona kwa namna ambayo Mimi sikuwahi kuvifikiria, japo Mimi ndio nilikuwa mkubwa kwake kwa miaka 6+
Mkuu hii sentensi haujaitolea maelezo kabisa hadi portion iliyoisha. Ni kitu gani alikiona kwako Esther halafu mwishowe akakubali kukipoteza tu.
Please, kabla haujaenda kwa story za mashangazi.
 
Portion 06.

..... Ipo hivi. Kuna kipindi nilipanga maeneo ya Tabata barakuda kwa chini, panaitwa "Kiwanjani". Ni ndani ndani kidogo, ukitokea barabarani. Sikuwa na marafiki wengi pale mtaani, na hii ilitokana na aina ya maisha niliyokuwa naishi. Naondoka asubuhi, narudi jioni au usiku, wik end sikuwa natembea tembea pia. Japo mara moja moja, siku za wik end au hata katikati ya wiki, kama sina ratiba maalum ya kutoka, basi mida ya jioni nilikuwa napenda kwenda kuangalia mpira maeneo ya Tabata Sigara.

Mara nyingi nikiwa narudi, kituo cha kushukia ilikuwa ni barakuda kisha nateremesha bondeni kuelekea ghetto kwangu. Nikiwa na kama wiki na nusu tokea nihamie kwenye ule mtaa, jioni moja wakati natembea mdogo mdogo nikiwa narudi home, mbele yangu alikuwa Mama mmoja wa makamo, kabeba ndoo kubwa kichwani, alafu mkononi kabeba kikapu.

Wote tulikuwa tunaelekea uelekeo mmoja. Tunashusha kile kilima.

Kwa mwendo wake, nikiangalia na vile vitu alivyokuwa kabeba. Nilijikuta namuonea huruma, ikabidi niombe kumsaidia kile kikapu cha mkononi.

Baada ya kuwa tumeumaliza ule mteremko, akaniomba nimpatie ule mzigo wake huku akinishukuru. Kwa maelezo aliyonipa, hakuwa anakaa mbali tokea pale tulipokuwa. Alijaribu kunielekeza japo sikutilia maanani, nikamuachia mzigo wake, nikaondoka.

Zikapita kama siku tatu bila kumuona tena yule bi mkubwa, na hata kwenye fikra zangu alishatoka. Ila kuna siku nyingine asubuhi nawahi zangu job, nikakutana nae kituoni akiwa anasubiria daladala. Yeye ndio alikuwa wa kwanza kuniona, akanipungia mkono, tukasalimiana ile kimbalimbali. Gari ilivyofika wote tukawa tumepanda, na hapo ndio tuliweza kujuliana hali kwa ukaribu na kuongea kidogo.

Baada ya mwendo kadhaa, alipata siti akawa amekaa, kila mmoja akawa busy na mambo yake na hatukuongea tena, zaidi ya kunipungia mkono wakati anashuka, maana alianza kushuka kabla yangu. Hii siku ndio nilipata wasaa wa kumuangalia kwa ukaribu, hakuwa mkubwa kivile, nyama za kutosha, muda wote akiongea anapenda kutabasamu. Hata baada ya kuwa ameshuka ndani ya lile gari, bado tabasam lake liliendelea kubakia kwenye fikra zangu. Pole pole akili yangu ikaanza kumchukulia tofauti.

Ilikata wiki bila kumuona tena. Nakumbuka hiyo
siku ilikuwa jumapili, mida ya jioni napandisha zangu Tabata Sigara kwenda kuangalia mpira. Nikiwa njiani nikamuona tena yule bi Mkubwa. Safari hii Mimi ndio nilianza kumuona, nikampungia mkono, akaacha kutembea ikawa kama vile anataka salamu ziishe ndio aendelee na safari yake. Ikabidi nisogee upande aliokuwepo ;

Bi Mkubwa: "Yani wewe kila mara tunakutana kwenye hiki kilima tu. Hujambo?"

Analyse: "Sijambo Mama, labda kwavile wote hatukai mbali na hiki kilima"

Bi Mkubwa: "Hivi unakaa maeneo gani"

(Nikajaribu kumuelekeza elekeza pale, aliishia kuutambua mtaa wangu, japo nyumba hakuifahamu vizuri)

Bi Mkubwa: "Kumbe sio mbali sana"

Analyse: "Sio mbali kabisa"

Bi Mkubwa: "Haya kijana wangu nisikucheleweshe unapoenda"

Analyse: "Sawa Mama"

Bi Mkubwa: "Haya jioni njema"

Muda wote tunaongea pale, akili yangu inajaribu kuchekecha ni Kwa namna gani naweza kumuomba namba yake ya simu. Na mpaka anaamua kuniaga, sikuwa nimepata trick ya kumuomba ya simu. Iko wazi Mimi na yeye hatukuwa na sababu kubadilishana namba za simu, ila kwa upande wangu nilijiona ninasababu kibao. Nilishachoshwa na ile hali ya kuwa tunakutana kwa bahati mbaya tu, akili yangu ilishaanza kunipush nitengeneze mazingira ya kuwa tunaonana. Kwahiyo baada ya yeye kuwa amenitakia jioni njema, ikabidi nimjibu tu,

Analyse: "Asante mama, na wewe naomba nikutakie usiku mwema"

Lengo la kumwambia hivi ilikuwa nikujaribu kurefusha maongezi yetu maana nilijua angeshangaa, walau niendelee kufikiria sababu ya kumpa ili nimuombe namba, japo sikuwa na uhakika nini kitafatia baada kuwa nimemwambia vile;

Bi Mkubwa (akashangaa): "Unan'takia usiku mwema kweupe hivi? Uko sawa kijana wangu, au ushaonja kidogo?"

Analyse (nikatabasamu kidogo): "Mimi niko sawa Mama angu, ni vile tu baada ya hapa hatutoweza kuonana tena pengine mpaka baada ya wiki, nisipokutakia usiku mwema sasa hivi, nitakutakia saa ngapi?"

Bi Mkubwa: "Yani kumbe ndio unavituko hivi? Sasa kama tumeweza kuonana sasa, ndio itashindikana baadae? Maana jua halijazama bado ili. Hata hivyo kwangu unapajua, unaweza pita"

Analyse: "Yani nifunge safari mpaka kwako kwa ajili ya kukutakia usiku mwema tu?"

Bi Mkubwa: "Sasa shida iko wapi?"

Analyse: "Hakuna shida, basi leo nitajaribu kufika kwako"

Bi Mkubwa: "Karibu sana, kwani unapakumbuka tokea nimekuelekeza siku ile?"

Analyse: "Hata sipakumbuki, naomba uniachie namba yako nikitaka kuja nikupigie, maana dalili za kupotea ni nyingi"

Bi Mkubwa: "Kuzunguka kote kumbe ulikuwa unataka namba ya simu?"

Analyse: "Unajua tumekuwa tukikutana mara kadhaa kwa bahati mbaya, nadhani imefika wakati inabidi tuanza kukutana kwa makusudi"

Bi Mkubwa: "Una maneno wewe, haya andika nataka niwahi kwangu nikapumzike"

Akanitajia, nikambeep, kisha kila mmoja akaendelea na safari yake.

Kama kuna sehemu nilishawahi kuingia choo cha kike, basi ni kwenye mahusiano na huyu Mama aisee. Alijua sana kuninyoosha, kiasi kwamba ilifikia wakati nikiona calls yake mwili unaniishia nguvu.

Hapa ndio niliamini kwamba, haijalishi ni mahusiano ya muda mrefu au mfupi, sometime inabidi kufanya background check, maana kuna sehem zingine hazifai hata kuzisogelea.

Mimi ni miongoni mwa wale wenye mioyo migumu sana, hasa wanapohubiriwa neno la Mungu. Ila kuna kipindi nilishikika, ilifikia hatua kama mara tatu hivi nilianza kupatwa na msukumo wa kutaka kuokoka.

Kati ya hizo mara 3, moja wapo ni kipindi nipo na huyu Mama. Aisee kuna wanawake ukitaka kuingia kwenye maisha yao unabembeleza, na ukitaka kutoka bado unabembeleza vile vile.

Kwangu, huu ulikuwa ni kama nimedandia mtumbwi wa vibwengo tu.

Anyways, tuachane na hayo kwanza.

Tulivyoachana pale baada ya kupeana namba, ratiba ya kwenda kuangalia mpira niliendelea nayo. Ila muda wote wakati nipo pale Sigara, akili yangu yote inajaribu kuchakata nini kifanyike pindi nikitoka kuangalia mpira.

Kuna upande unaniambia nimkaushie kwanza, lakini sauti nyingine inaniambia niende japo kumsalimia na kupajua kwake. Hii sauti ya pili niliipotezea maana sikuwa nafahamu mazingira ya kwake, unaweza kwenda kichwa kichwa ukakutana na mumewe kule, alafu ikawa balaa.

Baada ya kujifikiria sana, nikaadhimia mpira ukiisha nirudi zangu ghetto tu. Mida ya saa nne kasoro usiku nikiwa ghetto nikaona acha walau nimtumie msg:

Analyse: "Usiku mwema Mama"

Msg haikujibiwa!

Muda ulivyoenda bila majibu, nikaanza kuhisi atakuwa kalala, au labda ni mke wa mtu yupo na mumewe huko. Nikaamua nikaushe tu. Kuna muda natamani ningekausha mazima tu, au nisingemcheki kabisa, maana sipendagi nitume msg alafu isijibiwe. Ila ndio hivyo sikuwa najua, hivyo siwezi kujilaumu sana.

****** ****** ******* *******

Asubuhi nilitarajia kukuta msg yake, lakini hola. Nikawa naamini atanitafuta baada ya kuona msg yangu, lakini pia ikawa hola.

Nikawa najiuliza mbona kimya? Au hana vocha?Nilivyoona muda unasonga bila yeye kunitafuta, nikaamua kumpigia. Sikutaka kutuma msg. Safari hii simu nayo ikaita hadi ikakata, nikaamua niendelee na mambo yangu tu, nikampotezea.

Baada ya ukimya wa takribani siku nzima, mida ya jioni akanitumia msg;

Bi Mkubwa: "Umeshindaje?"

Analyse: "Salama tu, vipi wewe?"

Bi Mkubwa: "Mungu mkubwa, huku kwema tu"

Analyse: "Ulikuwa kimya tokea jana, hadi nikahisi labda ulinipa namba ya uongo"

Bi Mkubwa: "Namba ya uongo kivipi wakati jana ulinidipu ikaita?"

Analyse: "Ukimya wako ulinikosesha bahati ya kupajua kwako"

Bi Mkubwa: "Ungepiga tu maana mambo ni mengi, hadi nafasi ya kusoma msg haipo"

Analyse: "Nipige simu muda ule alafu hapokee mumeo, nitamwambia nini?"

Bi Mkubwa: "Kama lengo lako ni kutaka kujua kama nipo na mume au la, uliza tu. Mbona unazunguka sana?"

Analyse: "Vipi mumeo yuko wapi? Maana Kwa umri huo siamini kama huna mume"

Bi Mkubwa: "Kama Unahisi nina mume, namba yangu uliniomba ya nini?"

(Nikahisi kama ameanza kupoteza hali ya utulivu, maana ni kama alikuwa anaboreka na conversation yetu).

Analyse: "Nilitaka walau niwe na watu ninaofahamiana nao hapa mtaani, maana siunajua Mimi bado mgeni mgeni?"

Bi Mkubwa: "Mgeni? Mbona sijakuona na kamba mguuni?. Mbona una maneno mengi yasiyo na msingi?"

Analyse: "Yaliyo na msingi ni yapi?"

Bi Mkubwa: "We mtoto naona maswali yamekuwa mengi sasa, hebu ngoja nilale kidogo"

Analyse: "Sawa, baadae tunaweza kuonana?"

Bi Mkubwa: "Una jipya gani?"

Analyse: "Mapya yapo mengi tu, nahitaji muda wako tu ili niweze kuyaweka wazi"

Bi Mkubwa: "Baadae nitakuwepo kama unajiamini, karibu"

Analyse: "Asante"

Nilidhamiria baadae niende kweli pale kwake, ila Kuna kitu kimoja kikawa kinanipa wasiwasi. Huyu bi mkubwa wakati tunachat, alikuwa ananijibu dry sana tofauti na tunavyoongeaga tukiwa njiani. Akili ikaanza kuniambia isijekuwa nilikuwa nachat na dume mwenzangu au naenda kuingia mtegoni.

Nikaanza kujiuliza, niende au nisiende? Pale mtaani bado sifahamiki, pakitokea lolote nani atakuwa mtetezi wangu?

Baada ya kujiuliza sana, nikaamua acha niende tu, lakini nikajiambia inabidi niwe na taadhari.

Nikaendelea na mishe zangu,huku navuta muda...

** ****

Soma next portion hapa:
Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri
 
Back
Top Bottom