Lift ya Jengo la Millenium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu kwatajwa kuwa chanzo

Lift ya Jengo la Millenium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu kwatajwa kuwa chanzo

Tz ni nchi hovyo Sana! Kuna mwaka fulani walikata tiketi za ndege kuzidi siti, watz wakasema tunasimama! Mpk waliposhushwa kwa nguvu!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah
 
Kuna Floor za jengo refu pale posta ni kama gari za mbagala zinajaa mpaka kingora kinalia watu ndio wanapungua.. afu watu wapunguze uvivu floor 1 & 2 sio ya kupanda lift.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila nyie watu.
 
Mission completed but not totally completed.
Msikae kusema et lift imefanyiwa maintenance hivi karibuni au kilienda kikarudi. Fuatilieni huko millennium tower kuna huduma gani na effect kwa taifa, fuatilieni ni wakina nani hao majeruhi na nafasi zao katika serikali na jamii.

#Letsusthinkindeep

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Kuna Uwezekano Lift ilikuwa mbovu au Maintanance hazifanyiwi kwa wakati...

Ninachofahamu mimi....Lift uzito ukizidi haiwezi kuondoka... Mlango utafunga kama kawaida ila Inasimama Floor hiyo hiyo hadi Uzito upungue.. Tena hasa hizi lift za Kisasa..

Niwape pole Majeruhi..
Dada uniitage nije kupanda lift huko bas.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sawa Mdogo wangu

Tutaanzia zile Opposite na kwenu...PSSSF commercial Complex...Tena bado mpya mpya zile...

Halafu twende na pengine tena[emoji28]
 
Kuna Floor za jengo refu pale posta ni kama gari za mbagala zinajaa mpaka kingora kinalia watu ndio wanapungua.. afu watu wapunguze uvivu floor 1 & 2 sio ya kupanda lift.
Jengo la Ushirika Mnazi mmoja kulikuwa na Babu kaajiriwa kukubonyezea unaposhuka

lilikuwa linajaza haswa na yeye ndio ataamua pa kubonyeza
 
Watu saba wamejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Kairuki kwa ajili ya matibabu baada ya lifti kuporomoka kutoka ghorofa ya 10 katika jengo la Millenium Tower lililopo Kijitonyama Jijini Dar es salaam.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema chanzo ni lifti hiyo iliyokuwa imebeba zaidi ya Watu kumi kuzidiwa uzito ——— “lifti ilizidiwa uzito na ilikuwa imefanyiwa matengenezo hivi karibuni ambapo leo ilikuwa inajaribiwa na kulikuwa na Fundi ndani”

Askari wa Zimamoto na Uokoaji Assintant Inspector Mohammed kutoka Kinondoni amesema kilichofanywa na Uongozi wa jengo hilo lenye ghorofa 25 ni makosa kwa kuwa hawakupaswa kufanya majaribio ya lift kukiwa na Watu ndani bali walitakiwa kuweka kitu chochote chenye uzito ndani ya lifti ndio waifanyie marekebisho.
 
Hiyo mitaa kuna shetani mtoa roho anatembea, jana mtu kajirusha na leo lift imeporomoka
Daaah mimi naona shetani apumzishwe kila kitu shetani😂😂, unachepuka shetani, ukijikwaa kidogo shetani, mtu kajitupa shetani, ukifukuzwa KAZI KWA KUIBA shetani aseee awe tu na yeye anaenda kushtaki KWA MUNGU 🤣🤣🤣
 
Sema yale madude yanaogopesha sana, nikipanda huwa sina amani nawaza kamba ikikatika na hapo unaenda upo 11th floor itakuwaje? 😄 ila kutoka 10th floor mpaka ground hao watu wamepona? Aise wakatoe sadaka kanisani
 
Back
Top Bottom