Tatizo kubwa sio mfumo wa vyama vingi, bali ni chama tawala kulazimisha kuwepo madarakani bila ridhaa ya wengi. Inaonekana chama tawala kulikubali kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila chenyewe kuwa tayari kwa hilo. Matokeo yake wananchi wengi wamesharidhia hali hiyo, huku chama tawala kikilazimisha kubaki chenyewe au madarakani kwa njia ya kunajisi box la kura. Hali hiyo inachangia mvutano na mgawanyiko usio wa lazima hasa anapotokea rais asiyeheshimu kutofautiana kimitazamo.
Wengi wanatafuta sababu zisizotoa jawabu. Vyama vingi vilikuwepo miongo dahari
Rais Mkapa kuna wakati alikerwa sana na vyama vingi.
Aliwajibu kwa hoja na mantiki.Aliwapiga kwa hoja na kuanzia hapo wakawa kimya.
Rais Kikwete, tofauti na Mkapa yeye alionekana kutojali sana wapinzani wanasema nini.
Viongozi hao walikuwa katika zama za mitandao na vyama vingi.
Nakumbuka hotuba ya Mw Nyerere pale Jangwani wakati akina Mrema wakiwa juu kisiasa.
Mwl aliona tatizo linaloweza kutokana na mgawanyiko wa mambo madogo ya siasa.
Mwl alijua kuna umuhimu wa watu kutofautiana kimitazamo bila kuhasimiana
Hilo litawezekana watu wakiridhiana bila chuki au vinyongo
Pengine kuna kitu sielewi au ninakiona ''upside down''.Uvumi sioni kama ni hoja
Ninachokiona ni picha ya uvumi huo, na kujiuliza kwanini uvumi umepewa nafasi kiasi hiki?
Kwanini haya yanatokea? Nini tofauti na nini kifanyike?Je, hizi si dalili njema za Taifa?
Kama siyo tumefikaje hapa Watanzania wenye upendo hata ''kushabikia'' uvumi na mabaya?
Hivi tukiondoa mitandao, tukafuta vyama vingi, tutawezaje kufuta ''hizi roho za kutakiana mabaya'' Kumbuka hizi ni ''intrinsic'', hujitokeza tu zenyewe, hatuna uwezo nazo
Kuna mzee hapa Kicheba alitueleza,mgonjwa wa akili akiongeza msikilize, utapata kitu
Hawa mashabiki na wazua uvumi wadharauliwe , lakini pia kuna kujitazama kupitia uvumi na uzushi wao iwapo kuna cha kujifunza , kama hakuna, tuwadharau
Tukiwaacha kama ''wagonjwa'' kwa hoja za vyama vingi na mitandao hatujitendei haki!
Tutakuwa tunalaumu jinsi wanavyosambaza uvumi wao(mitandao) kwa itakadi zao(vyama vingi) na kuacha hoja ya '' nini msukumo ulio nyuma ' hadi wanafikia kuzusha uvumi na uongo wa mabaya! tusiyoyataka wala kuyaombea!