Lighter Touch: Ule uvumi ungenoga hivi leo

Chadema tu ndio walifurahi, ila nina amini JPM atawafurahisha zaidi! Subiri
Haya ni makosa yanayojirudia. Huwezi kujua nani Chadema nani CCM na nani hayupo miongoni mwao. Unachotakiwa kujua ni kuwa kuna ''ufa''.

Ukianza kusema hawa ni CDM wale ni Uvccm hawa ni Jucuf tayari unaligawa Taifa
Taifa linajengwa na muunganiko wa wote, ukianza kutenga unajenga ufa

Hili ni kosa sijui kwanini watu hawajifunzi.
 
Nakubaliana nawe, naondoa hilo neno ''kila mtu'' kwa kuwa hakuna kigezo wala takwimu. Badala yake natumia ''hali iliyopo''. Swali linabaki pale pale, nini kimebadilika hadi hali ikawa kama ilivyo leo?
Ninakushukuru kwa kuondoa neno KILA MTU.

Hali haijabadilika bali kilichobadilika ni njia/fursa za kufikisha ujumbe. Zamani ilikuwa lazima uwe na Laptop au PC kama unataka kufikisha ujumbe kupitia internet. Leo hii simu ya kiganjani inafanya mambo yote lakini kikubwa zaidi hata gharama yake kwa sasa iko chini.

Kama nilivyosema, zamani kabla ya mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Instagram haijawa maarufu na kupata watumiaji wengi, watu walikuwa wanategemea forums ambazo zilikuwa na moderators ambao walikuwa wanafuta message hasi kwa jamii. Mfano Jamboforums/Jamiiforums na yahoo forums.

Wewe kama mkongwe hapa umekuwa mtu ambaye unasema taifa limegawanyika hata kabla Rais Magufuli hajaingia madarakani. Nakumbuka ulikuwa unamlaumu sana Rais Kikwete kwa kuligawa taifa halafu leo unahoji kama vile tatizo hili limeanza kwenye awamu ya tano!
 
Hakuna muunganiko wa chadema, usitegemee watu wenye akili ya kunguni wakaunganika! Walimtukana kila aina ya tusi kikwete, leo wanamlilia
Chadema sio watu wa kuwa entertain hata kidogo, ni kubana na kuwakanyaga kwa kadri utavyoweza!
Na namuomba mh. Raisi afanye jambo kwa wajinga hawa
 
Bado sikubaliani nawe kwasababu una hoja mbili. Kwanza, vyama vingi ambayo sasa unaiacha na kuingilia mitandao. Mitandao ipo zaidi ya miaka 20 sasa na awamu zote!

Pili, sijasema kugawanyika kwa taifa kumeanza na awamu hii.
Huko nyuma tuligawanyika hasa baada ya Mkapa kuondoka madarakani. Kukawa na Wanamtandao, Original n.k. Tukaona taifa linagawanyika katika masuala muhimu kama katiba
Tulisema, kugawanyika huko hakukuwa jambo zuri kwani ni mwanzo wa mmomonyoko wa umoja wetu wa kitaifa.

Tulipofikia sasa nadhani utakubaliana nami ni hatua mpya. Hii hatua ya kutakiana mabaya kwa pande zote, kuhasimiana katika misiba, matibabu na hali za kibinadamu kama ilivyotokea katika uzushi na uvumi ni mwendelezo lakini hatua ya juu zaidi isiyohitaji microscope kubaini tatizo.

Ndiyo maana nilikuuliza, tumefikaje hapa? Tunaondokaje hapa?
Hoja yangu imejengwa juu ya nini kifanyike turudi katika upendo na umoja wa kitaifa na si uvumi ambao tunajua hauna maana

Tofauti na wengine wanaolaumu uvumi kama tatizo, mimi naona uvumi kama dalili tu ''symptoms' picha kubwa ya uvumi ndilo tatizo na tunapaswa kulijadili wala si kutafuta namna ya kufukia vichwa mchangani mwili nje kwa hoja za vyama vingi au mitandao.
 
OK! kama hiyo ndiyo njia ya kuliunganisha Taifa, naiwe hivyo!
 
Yote 9 ..kumi playlist ya Msigwa ilinifurahisha

Hauwezii kushindanaaa na wanadamu wenye kinywa
 
Ujumbe ni huu tu ama kuna kitu cha ziada umekiweka?
 
Nakubaliana nawe, naondoa hilo neno ''kila mtu'' kwa kuwa hakuna kigezo wala takwimu. Badala yake natumia ''hali iliyopo''. Swali linabaki pale pale, nini kimebadilika hadi hali ikawa kama ilivyo leo?

Kilichobadilika ni uwepo wa mitandao ya kijamii na upatikanaji mrahisi wa simu janja [ aka mitambo ya kuzalisha na kueneza ujinga na ujuha].
 

Si ajabu ndege hiyo yenye kasi ya ajabu iliyompeleka kote huko, imetoka kwa wazee wa Gamboshi.
 

mkuu


nisingeweza kumjibu vizuri na kwa ustaarabu kama hivi

ningemtukana tu
 
Zitto, Maria Tsehai Sarungi, Ansbert Ngurumo, Evarist Chahali, Godbless Lema, Vincent Mashinji na ndugu yao Kigogo...watu Wa ajabu sana
Umemsahau fatuma na mdude.
 

kwanini haumlaumu mzushi?
 
Wengi wanatafuta sababu zisizotoa jawabu. Vyama vingi vilikuwepo miongo dahari

Rais Mkapa kuna wakati alikerwa sana na vyama vingi.
Aliwajibu kwa hoja na mantiki.Aliwapiga kwa hoja na kuanzia hapo wakawa kimya.

Rais Kikwete, tofauti na Mkapa yeye alionekana kutojali sana wapinzani wanasema nini.

Viongozi hao walikuwa katika zama za mitandao na vyama vingi.

Nakumbuka hotuba ya Mw Nyerere pale Jangwani wakati akina Mrema wakiwa juu kisiasa.

Mwl aliona tatizo linaloweza kutokana na mgawanyiko wa mambo madogo ya siasa.
Mwl alijua kuna umuhimu wa watu kutofautiana kimitazamo bila kuhasimiana
Hilo litawezekana watu wakiridhiana bila chuki au vinyongo

Pengine kuna kitu sielewi au ninakiona ''upside down''.Uvumi sioni kama ni hoja

Ninachokiona ni picha ya uvumi huo, na kujiuliza kwanini uvumi umepewa nafasi kiasi hiki?

Kwanini haya yanatokea? Nini tofauti na nini kifanyike?Je, hizi si dalili njema za Taifa?
Kama siyo tumefikaje hapa Watanzania wenye upendo hata ''kushabikia'' uvumi na mabaya?

Hivi tukiondoa mitandao, tukafuta vyama vingi, tutawezaje kufuta ''hizi roho za kutakiana mabaya'' Kumbuka hizi ni ''intrinsic'', hujitokeza tu zenyewe, hatuna uwezo nazo

Kuna mzee hapa Kicheba alitueleza,mgonjwa wa akili akiongeza msikilize, utapata kitu

Hawa mashabiki na wazua uvumi wadharauliwe , lakini pia kuna kujitazama kupitia uvumi na uzushi wao iwapo kuna cha kujifunza , kama hakuna, tuwadharau

Tukiwaacha kama ''wagonjwa'' kwa hoja za vyama vingi na mitandao hatujitendei haki!

Tutakuwa tunalaumu jinsi wanavyosambaza uvumi wao(mitandao) kwa itakadi zao(vyama vingi) na kuacha hoja ya '' nini msukumo ulio nyuma ' hadi wanafikia kuzusha uvumi na uongo wa mabaya! tusiyoyataka wala kuyaombea!
 

Uko too emotional mpaka unakosa hoja ya msingi zaidi ya kuja na mitazamo ya kujipendekeza ili utoke kimaisha. Kikwete hakutukanwa bali aliambiwa ukweli wake, na hata sasa hakuna anayemlilia, bali anapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa ili kumnanga Magufuli. Kila siku rais anasifiwa hasafiri kama sehemu ya kujibu tuhuma za awali kuwa JK alikuwa anasafiri sana. Hii vita yenye double standard ya ufisadi ni kilio cha upinzani. Uwepo wa katiba mpya ni jambo lililopata msukumo sana kutoka hao cdm.

Ni hivi usimuombe rais afanye kitu kuhusu cdm, bali muagize achukue hatua yoyote atakayo dhidi ya cdm, kwani ni hujuma ipi hajafanya kuhusu cdm useme hivi sasa ndio atakuwa amefanya jambo jipya? Ana mwaka wa nne huu, katumia madaraka yake awezavyo kuwafanyia kila hujuma na bado cdm ipo, mshauri aifute kabisa ili uridhike. Maoni ya kujipendekeza kwa umri ulio nao yatakupa maisha ya kiwango fulani, ila cdm ikifa kipi kitapeleka tena familia yako chooni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…