Kwanza niwapongeze watani kwa ushindi waleo ila pia nikili kwamba kama shabiki wa yanga nisingeweza kusema kwamba tutafungwa japo moyoni nilikuwa nafahamu tutafungwa kuanzia goli tatu nakuendelea.
Nipende kuwapongeza wachezaji na benchi la ufundi la timu yangu kwa kuipigania nembo ya timu kwa moyo mkubwa sana licha ya magumu tunayopitia kama timu, niwaombe mashabiki wenzangu wa yanga tuendelee kuchangia timu yetu kwa moyo mkunjufu kabisa, nivile tu uwezo wa kipesa sina kwa kiasi hicho ila ningekuwa nazo zakutosha nafikili leo ningewapa posho ya kutosha achilia mbali matokeo ya leo. Mungu ibariki yanga mungu tubariki wanayanga.