Ligi ya Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 2 - 1 AS Club Vita | Simba yafuzu kucheza hatua ya mtoano 2019

Nimependa hapo ulipo tia signature MPIRA SI UADUI, well said, hii inaonyesha una ukomavu katika nyanja za soka, keep it up lady, wana simba tunakupenda sana tunatamani uhamie upande huu maana huku ndiko kwenye furaha na mikakati, una kila sababu za kuwa shabiki namba 1 simba sc

Happiness is a lifestyle
 
Msiwalaumu Vita, km hali ilikuwa hivi wangepita wapi ???😳
 
Utani muhimu sana, ila jana mpaka nimewaonea huruma, bora hata mngedroo na Lipuli, maana mmeumia mara mbili.

Ngoja tuanze kula viporo Mtani, na kama unavyojua, viporo vya tajiri havichachi, freezer ni za kumwaga.
Acha tu niliumia nikijua furaha tutaipata kwa Mkapa mwishowe ikawa kinyume.

Ila ndio mpira huo japo hakuna kukata tamaa mpaka tone la mwisho ndio nitaamini kweli tumeukosa ubingwa.
 
Nakazia hapo kwenye kuhamia
 
Ahsante Mtani. Kuhama timu sisi kina YANGA lialia ni ngumu mno Mtani kama Ngamia kupita kwenye tundu la Sindano. Hivyo nakomaa na Yanga yangu tu mpaka mwisho.

Nauliza tu jana ulipata usingizi kweli Mtani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…