Likizo na Pasi Zasitishwa JWTZ. Waliokuwa likizo waitwa warudi kambini

Likizo na Pasi Zasitishwa JWTZ. Waliokuwa likizo waitwa warudi kambini

Status
Not open for further replies.
ukifa msalimu babayangu aliyefariki sababu ya CCM. Kwangu mimi adui ni CCM na Rwanda ni ndugu zangu.

Every nation has internal and external enemies, domestic and foreign enemies; no surprise!
 
Nashauri kwa upendo kabisa na uzalendo wa hali ya juu kwamba kuna baadhi ya habari si za kuanika humu, maana hujui adui zako nao wakizisoma watafanya nini, suala la vita ni nyeti sana na hivyo tuwe makini na tunayoweka humu.
 
Sipendi NCHI hii iingie vitani,tuna matatizo mengi,Kagame hata akitaka kuchukua Kagera sina tatizo,kama hao watu watapatiwa maendeleo ,Eti uzalendo,wakati manufaa Uhuru yapo katika baadhi Familia tu
 
Sikatai kuandaliwa kwa haya majeshi, ila swali langu najiuliza, hivi kwa mfano Tanzania ikaingia kwenye vita na nchi yoyote kwenye eneo la maziwa mkuu ni kwa FAIDA ya nani? Maana watanzania tusidanganywe kuwa vita yoyote ni kwa faida ya WATANZANIA. Maana mimi hata haya malumbano ya TANZANIA na RWANDA sijui msingi wake ni nini. Raisi wetu alitoa ushauri wa Kagame, well and good, however, yeye kuna mangapi mabaya yanafanyika ndani ya nchi yake na ajachukua hatua? Maana tusitengeneze mazingira ya hatari ya kujitakia halafu baadae yakaonekana na kwa faida ya watanzania. This is totally wrong and unacceptable. Watawala wengi wa Afrika na wakiwemo wengine wa Tanzania kazi yao ni kufanya mambo kwa maslahi yao....Kabla ya hii nchi kupelekwa kwenye vita aidha za maneno au za silaha, watanzania tuambiwe hayo mavita yana faida gani kwa WATANZANIA na WANYARWANDA. Tusipelekwe kichwa kichwa tu. Hawa viongozi wetu wanarushiana maneno ila sisi WATANZANIA na WANYARWANDA bila shaka tunahitaji kuishi kwa umoja na undugu.

Mimi naomba watuambie kwanza hizi vita za maneno au za silaha ni kwa maslahi ya nani?

kudos kaka. Mbona vyombo vya habari havijamuuliza Kagame yeye kwa nini alisema vile?
 
Sipendi NCHI hii iingie vitani,tuna matatizo mengi,Kagame hata akitaka kuchukua Kagera sina tatizo,kama hao watu watapatiwa maendeleo ,Eti uzalendo,wakati manufaa Uhuru yapo katika baadhi Familia tu,
"Vox popoli vox dei"
 
Hizi zote naona ni propaganda tu, inawezekana vipi habari za ndani za kiintelijensia jeshini zije kuanikwa JF, si mnamrahisishia kazi hata adui mwenyewe!
 
Waende wakapigwe kazi yao kubaka dada zetu huko mtwara na kutia hasara kwenye taifa letu bila kazi yoyote wachewende huko
 
Huu ni wakati wa Tanzania kuungana pamoja kuliunga jeshi letu mkono......Mimi nipo tayar kwa kujitolea hili kwa kulinda mipaka yetu ya nchi
 
Ni jambo jema kuwa katika hali ya tahadhari, lakini wakubwa hao Kikwete na Kagame wazungumze haya mambo ya vita si ya kuendekeza. Ndugu zangu tukumbuke kuwa wakati wa Idd Amin na sasa ni nyakati tofauti sana, uzalendo miongoni mwa Watanzania ulikuwa mkubwa sana tofauti na leo ambako watu wako ki-matabaka, leo wengine wataamua kwenda kujitolea wakiwa na malengo maalumu ikiwa ni pamoja na uporaji . Vita si ya kushabikia na ikianza uwanja wa mapambano ni huko mpakani ambako raia wa kawaida wanaishi, hivyo kasheshe ni kwa akina mama na watoto, na hivi je kweli Tanzania kupigana na Rwanda kuna maslahi yoyote, yafanyike mazungumze tu huu upuuzi wa maneno kuhusu vita tuachane nao, tuna raslimali za kutosha bongo zetu zingejikita namna ya kushughulikia matumizi sahihi ya raslimali na kuwezesha watu waishi kwa amani kuliko hii kitu inaitwa vita!
 
Tanzania hatuna usiri wa vitu nyeti kama hivi?.

Usiri wa nini tena? Mficha uchi hazai. Rwanda walipopeleka vikosi mpakani walionyesha kwenye TV ya taifa. Marekani wanajadili kuipiga Syria mbele ya vyombo vya habari kwa hiyo hata sisi hakuna haja ya kuficha ugonjwa. Mambo ya kuvizia ni wakati vita inapiganwa kwa mikuki na siyo kipindi hiki unaweza tuma kitu ukiwa Tabora kikashuka Kigali.
Lazima aelewwe kwamba na sisi tumezinduka na tuko alert kwa lolote tumechoka kutishiwa!!!
 
Hivi kusikia Marekani inatuma meli zake za kivita huko Mashariki ya Kati wakati inasubiri kuishamblia Syria ni kuhatarisha usalama? Kuna siri na hii si siri yenye kuhatarisha jambo lolote. Mtu yeyote aliyesoma vizuri ataona kuwa kuna habari ambazo ningeweza kuziweka lakini kwa makusudi sikuziweka. Lakini katika nchi ya kidemokrasia wananchi hawatakiwi kujua mambo ambayo jeshi linapanga kufanya kwa jina lao - si wao ndio watalipia na wanalipia kodi mambo haya?
 
Ni wakati wa taifa letu kuendeleza mshikamano wengu katika hali yoyote itakayojili kuilenga tanzania,
hatuna nchi nyingine ni hii hii lazima tuitetee kwa nguvu zote.



Pumb mema mule nyie kweny vita mtake ushrikiano nas!!!!
 
Mwanajeshi gani kavujisha siri kamwambia Mwanakijiji mipango ya Jeshi letu.

Wanajeshi wanamna hii ni hatari kwa kutoa siri wanaweza hata kusaidiana na maadui zetu kutuhujumu.

Mkuu wa majeshi kuwa makini na vijana wako.

Aliyosema Mwanakijiji sio siri......viko kwenye public domain.....!

Pamoja na hayo wale makamanda wa RPA waliotekwa pamoja na vijana wao wa M23 bado wananyweshwa supu...!


Source:
Jeshi la Wananchi Tz ‏@JW_TZ 6h Vita imefika Def Con 003, ni ushindi wa 96%, Hii inatokana na kufanikiwa kukamata mateka 2602 ikiwemo maafisa wa juu wa 4 wa Jeshi la Rwanda
 
Hivi kusikia Marekani inatuma meli zake za kivita huko Mashariki ya Kati wakati inasubiri kuishamblia Syria ni kuhatarisha usalama? Kuna siri na hii si siri yenye kuhatarisha jambo lolote. Mtu yeyote aliyesoma vizuri ataona kuwa kuna habari ambazo ningeweza kuziweka lakini kwa makusudi sikuziweka. Lakini katika nchi ya kidemokrasia wananchi hawatakiwi kujua mambo ambayo jeshi linapanga kufanya kwa jina lao - si wao ndio watalipia na wanalipia kodi mambo haya?

Siku hizi mnawatii kweli kweli!!! Kuna MoU nini!!! ha! ha! ha! Alafu nimeiona kule kwenye twita ya JWTZ pia!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom