Lile fupa lililowashinda marais wanaume 4, rais mwanamke 1 aligegeda kama mlenda!. Miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa letu yatua bungeni asubuhi hii

Wanabodi

Soma bandiko hili kwa utangulizi huu Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza? na Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo na ... na Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.

Leo tarehe 10 November, 2023 ni siku ya ukombozi fulani kwa taifa letu la Tanzania, Lile Fupa Lililowashinda Marais Wanaume kwa kipindi cha miaka 40!, Rais Samia, ambaye ni rais Mwanamke shujaa wa awamu ya sita, leo ameanza kuli gegeda fupa hili lililowashinda marais madume wanne!, tena mgegedo wenyewe wa fupa hili, Mwanamke shujaa huyu, ameanza kuligegeda akiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili tuu na miezi kadhaa, kwa miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa Letu, inatua Bungeni Dodoma asubuhi hii kwa hati ya dharura!

Miswada hiyo ni Mswada wa mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, Muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kuondoa dhulma kubwa kwenye sheria yetu ya uchaguzi na muswada wa kurekebisha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.

Japo bado sijafanikiwa kuona contents za miswada hiyo, lakini kitendo cha serikali ya awamu ya sita kuwasilisha tuu miswada hii ni uthibitisho wa nia njema na dhamira ya dhati ambapo Rais Samia anastahili pongezi za dhati na kuthibitisha Wanawake wana uwezo mkubwa kuliko wanaume kwenye baadhi ya maeneo,

Kwa wenye access na TBC, macho na masikio yetu tuyaelekeze Bungeni Dodoma milango ya saa 4:30 asubuhi hii, hizi ngoma 3 zitashuka!.

NB: Pamoja na mabadiliko haya kutua Bungeni, ile hoja yangu Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa? is still valid!.

Karibuni

Paskali
Huyu Poti bana.
 
Inawezekana mkuu,kwa kuwa prides za Shetani ni pamoja na Gay Pride,Women Pride, Abortion Pride,Pornography Pride na Euthanasia Pride,hizi zote zinakuja,na tayari zimeshaana kupigiwa chapuo sana!For full blown Women Pride,Abortion Pride, Euthanasia Pride and Pornography Pride kama ilivyo Gay Pride, they are just waiting for the right time.Kwa sasa wamesema Wanadamu hawapo tayari.
Fact.
 
Wanabodi

Soma bandiko hili kwa utangulizi huu Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza? na Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo na ... na Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.

Leo tarehe 10 November, 2023 ni siku ya ukombozi fulani kwa taifa letu la Tanzania, Lile Fupa Lililowashinda Marais Wanaume kwa kipindi cha miaka 40!, Rais Samia, ambaye ni rais Mwanamke shujaa wa awamu ya sita, leo ameanza kuli gegeda fupa hili lililowashinda marais madume wanne!, tena mgegedo wenyewe wa fupa hili, Mwanamke shujaa huyu, ameanza kuligegeda akiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili tuu na miezi kadhaa, kwa miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa Letu, inatua Bungeni Dodoma asubuhi hii kwa hati ya dharura!

Miswada hiyo ni Mswada wa mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, Muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kuondoa dhulma kubwa kwenye sheria yetu ya uchaguzi na muswada wa kurekebisha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.

Japo bado sijafanikiwa kuona contents za miswada hiyo, lakini kitendo cha serikali ya awamu ya sita kuwasilisha tuu miswada hii ni uthibitisho wa nia njema na dhamira ya dhati ambapo Rais Samia anastahili pongezi za dhati na kuthibitisha Wanawake wana uwezo mkubwa kuliko wanaume kwenye baadhi ya maeneo,

Kwa wenye access na TBC, macho na masikio yetu tuyaelekeze Bungeni Dodoma milango ya saa 4:30 asubuhi hii, hizi ngoma 3 zitashuka!.

NB: Pamoja na mabadiliko haya kutua Bungeni, ile hoja yangu Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa? is still valid!.

Karibuni

Paskali
Ndo ndo ndo si chururu !
Something always is better than nothing !
Siku hizi tunaweza kula bila kunawa zipo sanitizer ! 😅🙏🙏
 
Lissu, mbowe na wapinzani wengine critical wampe mama maua yake, na wao pia tuwape maua yao kwa ku mobilize hayo. Mama anaenda kuweka historia kubwa iliyotukuka nchini
Akiamua anaweza !!
Na atakumbukwa milele kwa mazuri sio kwa mabaya !
Hata Jk angetaka angetupatia Katiba mpya lakini hakutaka tu kujiwekea legacy iliyotukuka. !!
Rais ana madaraka makubwa sana Nchi hii na pia Mwenyekiti wa Chama pia ana madaraka makubwa sana ndani ya Chama !!
Kwa mintarafu hizo nani mwenye ubavu wa kuzuia jambo jema akiamua lifanyike ??!! Tusidanganyane eti kuna wahafidhina wala nini !
Locuta causa finita kwa kilatini 😅🙏🙏
 
Wanabodi

Soma bandiko hili kwa utangulizi huu Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza? na Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo na ... na Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.

Leo tarehe 10 November, 2023 ni siku ya ukombozi fulani kwa taifa letu la Tanzania, Lile Fupa Lililowashinda Marais Wanaume kwa kipindi cha miaka 40!, Rais Samia, ambaye ni rais Mwanamke shujaa wa awamu ya sita, leo ameanza kuli gegeda fupa hili lililowashinda marais madume wanne!, tena mgegedo wenyewe wa fupa hili, Mwanamke shujaa huyu, ameanza kuligegeda akiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili tuu na miezi kadhaa, kwa miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa Letu, inatua Bungeni Dodoma asubuhi hii kwa hati ya dharura!

Miswada hiyo ni Mswada wa mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, Muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kuondoa dhulma kubwa kwenye sheria yetu ya uchaguzi na muswada wa kurekebisha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.

Japo bado sijafanikiwa kuona contents za miswada hiyo, lakini kitendo cha serikali ya awamu ya sita kuwasilisha tuu miswada hii ni uthibitisho wa nia njema na dhamira ya dhati ambapo Rais Samia anastahili pongezi za dhati na kuthibitisha Wanawake wana uwezo mkubwa kuliko wanaume kwenye baadhi ya maeneo,

Kwa wenye access na TBC, macho na masikio yetu tuyaelekeze Bungeni Dodoma milango ya saa 4:30 asubuhi hii, hizi ngoma 3 zitashuka!.

NB: Pamoja na mabadiliko haya kutua Bungeni, ile hoja yangu Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa? is still valid!.

Karibuni

Paskali
Nadhani ni response ya mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya siasa kuhusu namna ya kuendesha chaguzi zetu bila makelele. Imekaa vizuri
 
Eti "rais shupavu kabisa".... Dah kweli paskali huyu ana mission maalum humu na si nyingine bali na kumtengenezea mazingira ya kuaminika huyo anayemwita ni shupavu... Hongera mkuu kwa kuwa undercover.
 
Akiamua anaweza !!
Na atakumbukwa milele kwa mazuri sio kwa mabaya !
Hata Jk angetaka angetupatia Katiba mpya lakini hakutaka tu kujiwekea legacy iliyotukuka. !!
Rais ana madaraka makubwa sana Nchi hii na pia Mwenyekiti wa Chama pia ana madaraka makubwa sana ndani ya Chama !!
Kwa mintarafu hizo nani mwenye ubavu wa kuzuia jambo jema akiamua lifanyike ??!! Tusidanganyane eti kuna wahafidhina wala nini !
Locuta causa finita kwa kilatini
 
Paskal,

Hatujawahi kuwa na shida na uwepo wa sheria za uchaguzi, tume na ofisi ya msajili. Ila shida ipo kwenye content zake. Sasa sheria hizo zimepelekwa bungeni hata hujaona mapendezo ya mabadiliko yanalenga kuboresha au kuleta kichefuchefu zaidi.

Wewe tayari umeshaanza kusifia hata hujui unasifia nini. Magufuli alipeleka sheria nyingi bungeni lakini nyingi tumeona zilivyokuwa za hovyo.

Umekosa subira, ungesubiri ujue kilichopo na kama ndio kilio cha wananchi basi usifie.

Kuwa chawa promax unahitaji akili kubwa sio kuropoka na kusifia hata usichokijua
Pascal licha yakwamba ni sehemu ya CCM Lakini amekuw a akikwazwa na mwenendo wa namna chama hicho kinavyo ongoza nchi yetu .

Kuna kesi zisizo na idadi namna ambavyo chaguzi zetu za serikli za mitaa na chaguzi kuu , wagombea wa vyama mbadala (Upinzani) wakinyanyasika na kudhurumiwa hakizao za kuwa viongozi wa wananchi katika maeneo mbalimbali.

Kwa mda mrefu wananchi wamekuwa wakinyimwa baadhi ya viongozi wanao wataka kutoka vyama mbada na kusababisha kuchelewa Kwa maendeleo halisi.

Kwahiyo pengine furaha ya ndugu na kaka yetu Pascal Mayala ni kuona kile ambacho kumekuwa kikimuumiza mda mrefu madadiliko yana chungulia licha yakwamba bado uhalisia kuonekana content za miswaada hiyo.
 
Back
Top Bottom