Lile "jicho ona", limeona si vema Jeshi la Polisi kuwa sponsored! Sponsors wakifanya makosa, polisi atapat kigugumizi! Vipi sisi media na sponsors?

Lile "jicho ona", limeona si vema Jeshi la Polisi kuwa sponsored! Sponsors wakifanya makosa, polisi atapat kigugumizi! Vipi sisi media na sponsors?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kitu kipya humu kinachoitwa "Jicho Ona".

Jicho Ona ni vile vitu ambavyo kwa jicho la kawaida vinaonekana kama ni vitu vizuri jambo jema, jambo zuri, jambo la kawaida, ila jicho ona linaona kuliko jicho la kawaida, linaona visivyo onekana na jicho la kawaida, jicho ona linaviona na kuviibua.

ikitokea kuna mtu ana jicho ona na unamkubali sana, kila jicho ona lake likiona kile unachokiona wewe wengine hawakioni, kila ukimpongeza unanyooshewa vidole na kuitwa chawa!, unafikia mahali unaamua hata ukiona jicho ona limeona kitu, unapongeza kimoyo moyo tuy ili kuepuka usiitwe "chawa", unajizuia mwisho unashindwa!

Leo nimeingia jf nikakutana na bandiko hili Watanzania ile Kesi ya kupinga matokeo ya Rais nchi Jirani sasa inarushwa mubashara na Citizen tv siyo hapa tunamtegemea MMM. Hivyo nikaamua kuwasha TV niangalie hii kesi.

Naifuatilia kwa shauku kubwa kwasababu sisi Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, The Common Laws of England, ambapo kamera haziruhusiwi mahakamani wala kesi hazitangazwi live, lakini kwa vile hii kesi ya uchaguzi ni high profile case, na ina the biggest public interest, then watakuwa wamekubali hii kesi iwe live ili kutoa fursa kwa public kuona kinachoendelea.

Nilipowasha TV, nikajikuta nasukumwa na uzalendo wa kichungulia kwanza hapa nyumbani kuna nini kabla ya kwenda Kenya. Ile kuwasha tuu TBC, macho kwa macho nakutana na jicho hilo!, baada tuu ya kuona jicho, mimi kwisha habari yangu, hakuna tena cha kwenda Kenya wala cha nini, ni nimeganda hapo hapo kwenye TV kukodolea macho jicho!

Nikamkuta mzungumzaji? Wa jicho ona yuko mubashara on TBC kwenye event fulani Jeshi la Polisi inayofanyika CCP Moshi. Mzungumzaji ametoa shukrani kwa wafadhili mbali mbali waliojitolea kulidhamini jeshi la polisi kufanikisha tukio hilo.

Mzungumzaji akasema wazi kuna taasisi za kudhaminiwa na wafadhili mbalimbali na kuna wafadhili na wadhamini, akasema wazi kuna baadhi ya shughuli jeshi la polisi halipaswi kuomba ufadhili wala udhamini, lifanye kwa uwezo wake wenyewe wa ndani, kwasababu hao wafadhili ni binadamu, wanapo lifadhili jeshi la polisi, siku wakifanya makosa, jeshi litakumbwa na kigugumizi namna ya kumwajibisha sponsor!

Hili limefurahisha sana na kunigusa sana, kwasababu hata sisi media, kuna mambo huwezi kufanya bila kumtegemea sponsor, sasa siku sponsors akiharibu, je media tutaweza kumuwajibisha kwa kumuandika vibaya?

Ukiisha dhaminiwa ni lazima umripoti vizuri sponsor!

Kiukweli kabisa lile jicho ona, linaona sana na litalisaidia sana taifa hili kwa kuona visivyo onekanika!

At this jancture jamani na mimi naomba mnipe pongezi zangu kwà kulibaini hili jicho ona kitambo sana!

Angalia tarehe ya bandiko hili Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu?

Pia nina kijiswali katika mambo haya haya ya udhamini, kwa vile Ikulu ni mahala patakatifu akitokea mfadhili yoyote kudhamini kitu chochote au jambo lolote la pale patakatifu petu, kuwepo na maximum transparency, mdhamini huyo ni nani, the motive behind udhamini huo, how much is involved?, and if it's huge sums of money, pia tumfanyie due diligence mdhamini huyo, his source of fund and what is trying to gain kwa kuifadhili Ikulu yetu, isije kuwa sio ufadhili as ufadhili bali uwekezaji kwa kutoa advance ya kitu fulani mainly some lucrative government tenders mkakuta mfadhili anapewa kwa single source!.

Hii live ya CCP imemalizika sasa ndio nakwenda Citizen TV Kenya kuangalia kesi ya uchaguzi, nimekuta patupu!
Kuna live ya Sheikh Sharrif Nassir wa ODM kushinda Ugavana wa Mombasa.

Nawatakia siku njema.
Paskali
 
Hili limefurahisha sana na kunigusa sana, kwasababu hata sisi media, kuna mambo huwezi kufanya bila kumtegemea sponsor, sasa siku sponsors akiharibu, je media tutaweza kumuwajibisha kwa kumuandika vibaya?.
Ukiisha dhaminiwa ni lazima umripoti vizuri sponsor!.
Hapa ndio vijana wa CCM wanatambaa na beat enzi za JPM walidance na mziki wake saivi maza kaja wamebadili gia angani wanatambaa na biti la maza maana ni "sponsor"

"Jicho ona" limefumbua jicho langu
 
Wafadhili vs Wadhamini, kwani hawa wote sio watu wanaoweza kutenda uhalifu pia?

Sioni sababu kwanini jeshi letu la polisi lijiweke rehani kwa sababu ya hizo njaa, wana maeneo ya kutosha, watengeneze miradi itakayowafanya wajihudumie kwa vyote ili waondokane na hii aibu.

Hii biashara ya kutafuta visingizio kwa tofauti za majina, nayo ni aibu pia.
 
Mambo mengine tunakwenda mbele na kurudi nyuma.

JKT waliambiwa wasitoke kwenye majukumu yao ya msingi.

Magereza nao vile vile.

Wote wanafanya miradi ya uzalishaji.

Sasa polisi wanaambiwa waondokane na utegemezi.

Watumie njia gani ambazo wengine wamekatazwa??

Wakikaa njiani kupiga mabao nako wanaambiwa wapungue.

Aisee haya mambo haya.
 
Moja ya super mada kutoka kwako Adv.Mayala, umeongea facts tupu na mimi ninaafiki kabisa jeshi letu la police lifanye kazi zake totally independent kutoka kwa politicians, ningepewa urais wa 24hrs,ningevunja hii wizara ya home affairs na kutengeneza wizara mbili, ministry of police na home affairs (immigrations &uraia),ingependeza mno jeshi langu la police pia lingekua linatoa crime statistics za nchi ili raia wajue kuwa hali ya uhalifu ipo vipi na jeshi la police limejipanga vipi kukabiliana nalo, otherwise jeshi langu la police kuwa sponsored na top dogs 🐕 sio vema kabisa
 
Mambo mengine tunakwenda mbele na kurudi nyuma.

JKT waliambiwa wasitoke kwenye majukumu yao ya msingi.

Magereza nao vile vile.

Wote wanafanya miradi ya uzalishaji.

Sasa polisi wanaambiwa waondokane na utegemezi.

Watumie njia gani ambazo wengine wamekatazwa??

Wakikaa njiani kupiga mabao nako wanaambiwa wapungue.

Aisee haya mambo haya.
Polisi ni watoa huduma siyo wazalishaji
 
Wanahabari ninyi tatizo lenu ni kubwa Sana. Tatizo lenu lina mzizi wa tatizo wenye tatizo kubwa.

Kitendo cha vyombo vya habari kutegemea zaidi matangazo toka serikalini, pamoja na ofa za kuandamana na rais ama viongozi wengine kwenye safari nje, huu ndiyo mzizi wa tatizo lenu kubwa.

Wanahabari ili vyombo vyenu viwe huru ni lazima vijitegemee kwanza kifedha. Ndipo kaI uenu kama mhimili wa nne wa nchi itafanikiwa.
 
Pascal usisahau hata royal tour ni pesa ya wadhamini na sterling aliyecheza anafahamu fika. Hata usiku wa chakula cha royal tour jumamosi kuna wadhamini.
 
Pascal usisahau hata royal tour ni pesa ya wadhamini na sterling aliyecheza anafahamu fika. Hata usiku wa chakula cha royal tour jumamosi kuna wadhamini.
Sina problem yoyote na udhamini wowote popote katika jambo la kheri kama Royal Tour,
Kitu muhimu ni maximum transparency kwenye udhamini wowote wa Ikulu yetu au rais wetu,
Mdhamini ni nani
Shughuli zake ni nini
Udhamini huo ni kiasi gani?
Mdhamini ku declare interest kuwa udhamini huo ni CSR na sio lobbying and advocacy ya kumendea tenda yoyote ya serekali ili apewe kwa SS.

Mfano Royal Tour yote toka shooting hadi uzinduzi imegharimiwa na mdhamini fulani, who is he, how much did he spend?, and what for?.
P
 
Pascal ni mmoja tu, nilianza kufuatilia mada zako kwa umakini zaidi kuanzia siku hii ulipombana kwa maswali mh aliyetangulia mbele ya haki.
 

Attachments

  • Swali_gumu_lililojibiwa_kirahisi_na_Magufuli(240p).mp4
    9 MB
Back
Top Bottom