Lililoitwa Sakata la Bandari: Pumba zimeanza kujitenga na Mchele

Umeamua kuandika upumbafu hui kwasababu ya Zitto Kabwe kuunga mkono uuzwaji wa bandari?? Ili sakata la bandari linazidi kukudhalilisha sana
 
Tafuta hoja aliweka hapo kaongea hisià zake za tumbo lake hawa ndo walewale wachumia tumbo
 
Umeshachumbiwa, mahari imeshatolewa kabisa na kupokelewa na wazazi wako, kilichobakia ni mumeo kuja kukuchukua ili uhamie nyumbani kwake kama mke rasmi.

Tahadhari kuhusu sifa mbaya za mumeo mtarajiwa na ulaghai wake kuhusu taarifa zake binafsi, ambazo ndizo zitawekwa katika cheti chenu cha ndoa kama mkataba wala hazikusumbui. Wewe unachokitaka ni kuondoka mara moja katika maisha yako ya kuganga.

Watu kama wewe ni sikio la kufa.
 
Sasa kijana mbona unajidhalilisha. Kuna ukweli upi wa Bandari kuuzwa? Au niambie wewe hapa Bandari ipi imeuzwa? Imeuzwaje?
Mimi siyo kijana.

Tatizo akili yako umeifunga ndani ya mipaka ya nyumba yako.

Kuuza kampuni siyo sawasawa na kuuza tenga la nyanya.

Kuuza uhuru wako au kuuza mamlaka ya nchi siyo sawa na kuuza suti.

Umewahi kusikia kuwa Taifa fulani limeuza uhuru wake? Umewahi kusikia nchi fulani imeuza mamlaka yake?

Kwa fikra zako, nchi ikiuza uhuru wake, ni sawa ilibeba bidhaa inayoitwa uhuru, sawa na unavyopeleka samaki ferry, halafu uhuru ukapigwa mnada kwa bei ya ushindani?

Ukipewa rushwa, na rushwa hiyo ikakufanya upoteze uwezo au utashi wa maamuzi, umeuza uhuru na mamlaka yako. Walioenda Dubai, wakapokea hongo mbalimbali ili wafanye maamuzi ya kuegemea upande wa DP, wameuza bandari zetu na mamlaka ya Taifa letu kwa malipo ya hongo waliyokula kwa sababu uhuru na uwezo wa maamuzi yao umefubazwa na rushwa walizokula.

Nikiwa Canada, kampuni ilikuwa na mwongozo hata wa kupokea zawadi. Kampuni yoyote au mtu binafsi ikikupa zawadi, ilikuwa ni lazima zawadi hiyo uipeleke kampuni ili ikaangaliwe thamani yake, na aliyekupa ana uhusiano gani wa kibiashara na kampuni yenu. Lengo ni kuangalia kama zawadi hiyo inaweza kuathiri maamuzi yako katika utendaji kazi. Ni vitu vidogo tu kama vile Tshirts, caps au mashati yenye nembo za kampuni, ambavyo vipo kwaajili ya kuitangaza kampuni au biashara ndivyo hukustahili kuvitolea taarifa.
 
CHAWA kama CHAWA!
 
Kwann Zanzibar haipo kwenye mkataba Kwani wao hawataki utamu wa uwekezaji
 
TEC tumemaliza kazi yetu. Na kanuni yetu ni moja, UKIMALIZA KAZI VITANI NA UKAMSHINDA ADUI HAUTAKIWI TENA KUJIELEZA (Post bellum non explicet)
 
Jana eti wanasema sasa wataongelea katiba mpya! Wameona la bandari limebuma.
Ndiyo maana tunasema wewe akili yako ni kibaba. Huelewi hata kinachoongelewa wala kulengwa.

Mkataba wa kishenzi wa DP, umeonesha umuhimu wa uharaka wa katiba mpya. Kama katiba ingekuwa nzuri, huu mkataba wa kishenzi usingesainiwa wala kuoitishwa na lile genge la wahuni wa Tulia, watu ambao hawakuchaguliwa na yeyote.
 
Tangazo kwa umma mabafiliko na TEUZI
Mweshimiwa rais hii leo Tarehe 6/9/2023,Amefanya teuzi mbali mbali na amemteua Lord denning kuwa mkuu wa wilaya ya Jukwaa la siasa,

Mheshimiwa Lord denning anachukua nafasi ya FaizaFoxy ambaye amehamishiwa katika wizara ya Utetezi wa bandari..

Zuhura Yunus
Ikulu maelezo
 
Poleni sana. Ukweli umeshafika. Uzandiki wenu hautafanikiwa kamwe
Sasa mbona husemi huo ukweli na wala huweki huo Ushahidi wa kisema watu wameelewa?? Na Je TPA wamendagaza geti zipi na DPW wanachukuwa Zipi??
Hoja hata Moja za Wananchi wanaokataa IGA hujazij8bu??!
CHAWA2
 
Urawekaje ukomo kwenye IGA wakati kuna HGA?

Ni suala la uelewa tu ndugu. Polee sana kwa kuwa kilaza
Wewe inaonekana una kichwa kizito sana.

Kwanza hiyo inayoitwa IGA ni batili. Na mahakama imetamka hivyo, na imelishauri Bunge kurekebisha hiyo kasoro. Hakuna IGA kati ya Nchi na jimbo.

Pili hicho kinachoitwa IGA, imezungumzia ukomo wa mkataba na kusema kuwa ukomo wake ni ukomo wa miradi ya HIGA. Kwa hiyo miradi ya HIGA isipokoma, hiyo IGA batili inaendelea kusimama. Upande wa pili unabanwa kuwa fursa zote za uwekezaji wa bandari kwenye bahari, maziwa na mito unalazimika kuwajulisha wao na huna mamlaka ya kuingia mikataba na wengine. Sasa hapo ukomo upo wapi? Tatizo mnasoma halafu mnatoka watupu. Halafu mnakuwa wajinga kuwazidi ambao hawana hata diploma.
 
Jifunze kusikiliza na kuelewa hata vile usivyopenda kusikia. Hiyo ndo maturity
Sasa nikisikiliza ujinga na kusema huu ni ujinga, siupendi, utanilaumu kwa kuwa nimeelewa huu ni ujinga nikasema siupendi?

Katika enzi hizi za uwajibikaji wa viongozi kwa umma uliowachagua unaweza vipi kumtetea rais anayesema hataki kujibu hoja za wananchi wake wengi wanaotaka zijibiwe?

Huoni kumtetea rais huyo ni ujinga?
 
Poleni sana. Ukweli umeshafika. Uzandiki wenu hautafanikiwa kamwe
KKKT wasema wanaunga mkono uwekezaji wenye tija kama wanavyoshauri TEC na akina Mwabukusi. Shida iko wapi?! Wamewakumbusha nyie mafisadi kuwa mkarejee hiyo IGA ina tija?; Kama siyo achaneni kama wananchi wanavyolalamika. Mbona hamtaki kujiuliza kama huo uwekezaji unatija kwa Taifa?!
IGA inaelekeza haki ya DPw kumiliki Bandari zote za Tanganyika kutoka Tanga hadi Mtwara, maziwa makuu na za nchi kavu na huwezi kuendeleza maeneo hayo bila kibali chao. Mbona unaficha haya badala yake unadanganya ati gati namba 1? Tena umiliki Wa milele. Kama issue ni ushirikiano kwanini IGA ije namna dispute resolution tena nje ya nchi yetu? Tangu lini mashirikiano ya kirafiki yakawa na kipengele cha dispute?! Urafiki ukifikaga mwisho si kila moja anakamata njia yake?!
ACT-wazalendo haiwezi kuwa rejea hata kidogo, ni chama ambacho mrengo wake inajulikana. Inaongozwa na Ayatola Kabwe ni sehemu ya Serikali ambayo ambayo unasukumwa agenda ya kuuza Bandari zote za Tanzania Bara huku Bandari ya zote za Zanzibar zikiwa excluded. Kikundi cha namna hii ni ya kusikiliza kama rejea?! Haiwezekani hata kidogo.
 
https://www.facebook.com/
View: https://fb.watch/mTLTQUYlL6/?mibextid=NnVzG8&startTimeMs=204921
 
https://www.facebook.com/
View: https://fb.watch/mTLTQUYlL6/?mibextid=NnVzG8&startTimeMs=204921
 
Kwa ufupi tu
Nina Masters ya Sheria- Westminster University
Sasa uneshindwa kujua wanaonufaika na bandari ndio haohao wanaoitaka dpw!
Bandari haikuwa inaendeshwa na wahuni. Ni wateule wa serikali hii hii..
Wanaotaka dpw ni wateule pia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…