Walio thubutu kumhoji Nyerere walifia jela au walikimbia nchi. Alitawala kidikteta yule mchonga meno.
Waliofia jela au kuikimbia nchi ni waliotaka kuulipia mlango bila kujali maisha ya waliokuwa ndani.
View attachment 2389895
Umuhimu wa kudai haki kwa amani kistaarabu lazima kuzingatiwa.
Nyerere aliwajengea wananchi wake uthubutu na Hilo si jambo dogo.
Mimi majibu yangu kwako ndugu yangu Ni kuwa je Nani amewahi kukuzuia kutoa maoni na hoja zenye kusaidia kujenga Taifa letu? Huamini hoja zako zinaweza kusaidia na kuleta Tija katika eneo fulani?Nikupe dokezo ya yaliyopo kwenye mada:
View attachment 2389889
Ninazungumzia uthubutu wa kuhoji uliouwawa ambao leo haupo tena. Mengine ni matokeo tu.
Hakuna mahali ninapopinga members JF kupigwa ban, nyuzi kufutwa au kufungwa lakini bila sababu kuwekwa hadharani?
Labda unifahamishe kwa nini Uzi huu kumwulizia member BAK ulifungwa?
Mimi majibu yangu kwako ndugu yangu Ni kuwa je Nani amewahi kukuzuia kutoa maoni na hoja zenye kusaidia kujenga Taifa letu? Huamini hoja zako zinaweza kusaidia na kuleta Tija katika eneo fulani?
Hakujenga huo uthubutu. Alitawala kidikteta. Ushahidi huu
Baada ya Nyerere, walau huyu alikuwa na misimamo inayoeleweka.View attachment 2389875
Mzee Mwinyi is my favourite President wakati wote when it comes to democracy, sawa na Ahmed Salim kama mtendaji mwenye weledi...JPM mtendaji mzuri kwenye utekelezaji alkini asiyeshaurika...Wengine siku nyingine...Kama Ma rais wangekuwa wanajifunza basi wange blend hizi tabia kuja na moja nzuri itakayosaidia nchi...Kila nabii na kitabu chake. Ukitaka kujua namaanisha nini kuhusu msemo huo, basi muulize Oscar Kambona, bibi Titi Mohammed na viongozi wengine walioonja joto la jiwe la mwl Nyerere. Kidogo uniambie Mwinyi ndo hakutumia nguvu kubwa kuwaadhibu waliompinga.
Kuna kijana (jina simtaji) huko chuo kikuu fulan aliwahi kumchora raisi Mwinyi picha ya kudhalilisha, kijana akashukiwa na wanausalama ili wakamuadabishe, lkn Mwinyi akawapigia sim fasta wana usalama na kuamrisha wamuachie kijana huyo haraka iwezekanavyo aendelee na masomo yake bila kujali matusi na kejeli zake alizozionesha kwake, kwa familia yake na nafasi yake kama raisi wa nchi.
Huyu kijana angefanya hivyo enzi za Nyerere pengine leo tusingekuwa nae tena.
Nyerere aliruhusu au alishauri viruhusiwe?Nyerere alifuta vipi vyama vya upinzani wakati ni 👉 yeye ndie aliruhusu vianze kuwepo'| licha ya kupingwa na wengi kwenye chama chake?
Usichanganye Nyerere kuvifuta vyama vya upinzani wakati wa kupigania Uhuru na baada ya hapo, wakati wa kupigania Uhuru ilikuwa ni vyema kwake kufanya alivyofanya ili kuwaunganisha watanzania kwa muda mfupi, wawe na lengo moja, ili kufikia matarajio waliyojiwekea.
Kuruhusu vyama vya upinzani kabla ya uhuru kungekuwa ni kuvurugana wenyewe kwa wenyewe hapa ndani, hivyo mkoloni angetumia mvurugano wetu kuendelea kututawala kirahisi, mimi niko na Nyerere kwenye hilo.
Nyerere aliruhusu au alishauri viruhusiwe?
Tena walioshauri ni wengi sio Nyerere peke yake.
Yani raisi wa nchi awe Mwinyi afu ruhusa atoe Nyerere?
Unataka kutuambia kwamba Nyerere alikuwa na cheo cha ayatollah Khomen wa Iran ambae maamuzi yake ndio ya mwisho mbele ya raisi?
Kama alikuwa na cheo cha ayatollah mbona alishindwa kutumia cheo hicho kurudisha azimio la Arusha na badala yake akawa analalamika tu kwenye vyombo vya habari kama tunavyoweza kulalamika mimi na wewe hapa JF bila kuwa na uwezo wa kumfanya lolote tunaemlalamikia?
Kama alikuwa na cheo hicho mbona alishindwa kumzuia Kambona na wengine waliokimbia utawala wake wasirudi nchini kama alivyowazuia kabla hajatoka kwenye uraisi?
Mbona alishindwa kuzuia mfumo wa biashara huru aliokuwa anaupinga wakati na kuukataza enzi za utawala wake na badala yake akawa analalamika tu kwenye vyombo vya habari kama kawaida yake?
Ukweli ni kwamba watu wengi (sio wote) wamekuwa wakipindisha ukweli wa baadhi ya mambo kwa lengo la kumpa sifa mtu ambae sifa hizo hazimstahili ili yule ambae zinamstahili aonekane hakuna la maana lolote alilofanya au analofanya.
Mwinyi ataendelea kuwa baba wa demokrasia ya nchi yetu maana katika utawala wake ndio watu walikuwa huru kuikosoa serikali yake na yeye mwenyewe bila mkosoaji yeyote kufungwa, kukimbia nchi, kufukuzwa chama, kuuwawa nk.
Mengine ni propaganda tu kama zilivyo propaganda zingine.
Hata kama alishauri viruhusiwe, basi kama viliruhusiwa kweli, inaonesha nguvu ya ushawishi aliyokuwa nayo kwa wale aliokuwa akiwaongoza, na hata baada ya kuwaongoza.Nyerere aliruhusu au alishauri viruhusiwe?
Tena walioshauri ni wengi sio Nyerere peke yake.
Yani raisi wa nchi awe Mwinyi afu ruhusa atoe Nyerere?
Unataka kutuambia kwamba Nyerere alikuwa na cheo cha ayatollah Khomen wa Iran ambae maamuzi yake ndio ya mwisho mbele ya raisi?
Kama alikuwa na cheo cha ayatollah mbona alishindwa kutumia cheo hicho kurudisha azimio la Arusha na badala yake akawa analalamika tu kwenye vyombo vya habari kama tunavyoweza kulalamika mimi na wewe hapa JF bila kuwa na uwezo wa kumfanya lolote tunaemlalamikia?
Kama alikuwa na cheo hicho mbona alishindwa kumzuia Kambona na wengine waliokimbia utawala wake wasirudi nchini kama alivyowazuia kabla hajatoka kwenye uraisi?
Mbona alishindwa kuzuia mfumo wa biashara huria aliokuwa anaupinga wakati na kuukataza enzi za utawala wake na badala yake akawa analalamika tu kwenye vyombo vya habari kama kawaida yake?
Ukweli ni kwamba watu wengi (sio wote) wamekuwa wakipindisha ukweli wa baadhi ya mambo kwa lengo la kumpa sifa mtu ambae sifa hizo hazimstahili ili yule ambae zinamstahili aonekane hakuna la maana lolote alilofanya au analofanya.
Ni kawaida kukuta watu hao wakichukua mazuri ya Mwinyi kumpa Nyerere au Mkapa, na kuchukua baadhi ya mabaya ya hao niliwataja kumpa Mwinyi.
Mwinyi ataendelea kuwa baba wa demokrasia ya nchi yetu maana katika utawala wake ndio watu walikuwa huru kuikosoa serikali yake na yeye mwenyewe bila mkosoaji yeyote kufungwa, kukimbia nchi, kufukuzwa chama, kuuwawa nk.
Nyerere angekuwa anapenda demokrasia asingewahenyesha waliokuwa wanampinga.
Angewasikiliza na kuwavumilia.
Mengine ni propaganda tu kama zilivyo propaganda zingine.
By the way namheshimu Nyerere kama baba wa taifa letu, ndio maana avatar yangu inaongozwa na picha yake kitambo sana.
Jf ilikuwa zamani, siku hizi imejiunga na waimba mapambioTanzania ya enzi za Nyerere ikiheshimika kila pembe ya dunia haipo tena. Tanzania hiyo ilikuwa na misimamo yake iliyojulikana na isiyotetereka.
Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote bila Afrika yote kuwa huru. Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote kama kulikuwa na ukiukwaji haki popote duniani Ukweli huo ulifahamika hivyo na kila rafiki na hata kila adui.
Kama taifa tulikuwa wamoja na nchi ilikuwa yetu sote. Nguvu ya hoja ilitamalaki na uthubutu wa kuhoji ulisisitizwa katika nyanja zote kutokea shule za misingi.
Leo baadhi ya watu kwa nafasi na ubinafsi wao wametumia nguvu kuuuwa uthubutu wa kuhoji. Yote hiyo ikiwa kwa nia ya kujimilikisha nchi wao na familia zao. Wasijue kuwa nchi wanaiuwa pia
Leo hatushindani kwa hoja. Hoja hazijibiwi kwa hoja, bali kejeli au kwa marungu. Watu wenye hoja tofauti wanatakiwa kuufyata. Tumelazimishwa kuwa taifa la makondoo.
Matokeo yake yamekuwa watu kulia lia yanapowakuta bila kuwa na uthubutu wa kuchukua hatua. Watu wamelazimika kuwa wenye kuangalia maslahi yao binafsi yanayowagusa wao moja kwa moja. Kwa maana jitihada za kuhoji lolote zimegeuzwa kuwa ni kujichumia majanga.
Uwezo wa kujenga, kutetea au kupinga hoja haupo tena. Utanzania wetu tuliojulikana nao umeparaganyika. Kila mtu imekuwa yupo yupo tu. Leo bila aibu tunajinasibu kama mashabiki wa Man U au Arsenal.
Ni muhimu kwa Kila mmoja kujihoji amefanya nini kuifikisha hii nchi hapa.
Anasema Prof Shivji:
“Pasipo mijadala au ubunifu huwezi kuendeleza fikra, na hii inakwenda moja kwa moja kuathiri usomaji na ufundishaji.”
Kwanini kuwaziba watu midomo? Kwanini hoja kupigwa marungu? Kwanini kuitana majina? Kwanini kujikita kupambana na mleta hoja badala ya kupambana na hoja? Nk, nk.
Kwanini JF hupiga wajumbe ban, kufuta au kufunga nyuzi bila kutoa sababu zikajulikana hadharani?
"Kwanini," huhitaji majibu si marungu.
Jf ilikuwa zamani, siku hizi imejiunga na waimba mapambio
Mtu mwenye nguvu na ushawishi anakoswa koswaje kupinduliwa hadi anaomba msaada nje ya nchi (Uingereza)?Hata kama alishauri viruhusiwe, basi kama viliruhusiwa kweli, inaonesha nguvu ya ushawishi aliyokuwa nayo kwa wale aliokuwa akiwaongoza, na hata baada ya kuwaongoza.
Mengine uliyoandika kama la biashara huria, suala la Kambona kurudi nk hayo yalikuwa mambo ya kifalsafa, hayo aliyaacha yatokee kwasababu alikuwa ameshaondoka madarakani, ndipo wenye mawazo tofauti wakaja kufanya waliyoona wao yanafaa, hapa Nyerere asingeweza kuingilia, alionesha ustaarabu wa hali ya juu, hakutaka udikteta.
Zaidi, unaposema Nyerere alipewa sifa nzuri asizostahili kutoka kwa Mwinyi, na Mwinyi kupewa sifa mbaya toka kwa Nyerere na Mkapa, hapa ndipo nimekuona una ajenda ya siri, na hiyo ajenda yako ya siri uliyonayo dhidi ya Nyerere ndio inakufanya usione mazuri yake, nimejua reasoning yako iko influenced na kitu gani, sitakushangaa tena.
Huyu Nyerere wenu ndiyo alituachia katiba hii mbovu pamoja na hawa viongozi wa hovyo
Kwa hili la intimidation, baba wa taifa tumwombee msamaha kwa Mungu...Hii tabia ya ukuu wa bila kuulizwa swali ila yeye akiongea ndiyo point hata kama haipo ni urithi aliotuachia ambao unatutafuna mpaka leo kama cancer...Akatuachia pia taifa lenye watu wenyeuthubutu wakuhoji.
Leo tumesheni chawa, makondoo, wapenda starehena mashabiki wa timu za arsenal na Man City. Wabinafsi wasiokuwa na lililola maana isipokuwa lao.
"Wapenda ngono na wachawi siyo kwenu tu, hata kwetu wapo."
Kama taifa tuna agenda ipi?
Sema ukipewa fursa ya kuiba mali za umma utaongea?Akatuachia pia taifa lenye watu wenyeuthubutu wakuhoji.
Leo tumesheni chawa, makondoo, wapenda starehe na mashabiki wa timu za arsenal na Man City. Wabinafsi wasiokuwa na lililola maana isipokuwa lao.
"Wapenda ngono na wachawi siyo kwenu tu, hata kwetu wapo."
Kama taifa tuna agenda ipi?
Hii ndiyo akili nyingine mbaya ya average Tanzanians...Kwanini udhani kwamba mtu hatakiwi kuongea akiwa na nafasi ya ki uongozi? Collective responsibility ni kwa yale tu ambayo yana maslahi kwa nchi nje ya hapo hiyo ni state capture, any person anaye default ni mzalendoSema ukipewa fursa ya kuiba mali za umma utaongea?
Bashiru, Kabudi, Slaa, Mkumbo wako wapi? tunaolalamika ni wale ambao tupo mbali na huu mfumo ovu wa kuiba pesa umma, hata wewe leo ukiteuliwa utaanza kuiba mapambio pekee.Hii ndiyo akili nyingine mbaya ya average Tanzanians...Kwanini udhani kwamba mtu hatakiwi kuongea akiwa na nafasi ya ki uongozi? Collective responsibility ni kwa yale tu ambayo yana maslahi kwa nchi nje ya hapo hiyo ni state capture, any person anaye default ni mzalendo
Sema ukipewa fursa ya kuiba mali za umma utaongea?