Lililokuwa taifa la kupigiwa Mfano halipo tena

Unaikumbuka hoja ya Abdul Jumbe aliekuwa Rais wa Zanzibar nini kilimkuta?
 
Ndugu yangu umemaliza kila kitu nakumbuka mwaka 1983 niliwakimbia polisi wasinikamate kwa kosa la kuuza vipande vya dawa ya mbu yalikuwa maisha mabovu sijapata kuona!!!

Kipindi hicho tulikuwa tukiliona trekta tunalikimbilia tukidhani limebeba chakula inafikia tunakimbilia mpaka gari zilizobeba maiti usitishwe na hizo nukuu lakini uhalisia Nyerere aliongoza Nchi hii kwa mkono wa chuma
 
Mbona wamejitokeza mara nyingi? What have they gained zaidi ya kuwa branded negatively na hao ambao wame consolidate power na wealth?
Ili kufupisha mjadala huu kati yetu, ingependeza sana kama ungetaja majina ya hao unaowafikiria kuwa "wamejitokeza mara nyingi,"
Itarahisisha sana mjadala huu ukiweka mifano ya hawa watu.
 
Unaikumbuka hoja ya Abdul Jumbe aliekuwa Rais wa Zanzibar nini kilimkuta?
Kwa hiyo kwa maoni yako wewe unajuwa ulikuwa ni uamzi wa Mwalimu Nyerere kuhusu yaliyompata Jumbe?
 
Kwenye kuwajengea wananchi uthubutu uko chaka
Heshima mkuu 'Yoda'.

Hebu fafanua unacholenga hapa, na kama unaweza utoe na mfano au mifano kwa nini unadhani "Kwenye kuwajengea wananchi uthubutu" huyo uliyemjibu yuko "chaka".

Pointi hii ni muhimu sana, kwa sababu watu wanafikra potofu kabisa kwamba waTanzania walinyamazishwa wakati wa Mwalimu Nyerere jambo ambalo siyo kweli.
 
Nyerere alimuuwa nani tena Zanzibar mkuu mbona sikuelewi?
Aliwauaje uwaje? Una ushahidi wa hiki ulichoandika hapa?
Soma kitabu kwaheri ukoloni kwaheri uhuru humo utaelewa kuwa Nyerere alikuwa adui wa Zanzibar hata kabla uhuru na yeye ndiye alikuwa kinara wa mavamizi yaliyouwa maelfu ya watu Zanzibar na mipango yake inaendelea kuitesa Zanzibar mpaka hii leo
 
Umeandika maneno matupu yasiweza kuvunja mfupa. Jikite kwenye Imani hii utwambie palipo na tatizo:

View attachment 2390863
basi wewe bado mtoto hujui yaliyokuwepo wakati wa nyerere. You have only been brainwashed kuamini kuwa nyerere was a perfect demi god. Huwa sijadiliani na toddlers
 
basi wewe bado mtoto hujui yaliyokuwepo wakati wa nyerere. You have only been brainwashed kuamini kuwa nyerere was a perfect demi god. Huwa sijadiliani na toddlers

Mada inahusu uthubutu wa kuhoji. Zingatia kuwa haujadili hilo uko way ward. Kama wewe mmetajwa kwenye mada. Hamna hoja wala stamina ya kujadili lolote.

Bure kabisa.
 

Nimesoma posts zako mbalimbali ukiruka ruka huku hadi kule. Ni wazi kuwa hukutambua msingi wa mada? Unaonekana kuwa uko kiimani zaidi mkuu.

Hoja Iko kwenye uthubutu wa kuhoji ndiyo maana hata kina BAK wameangaziwa. Kwanini - huhitaji majibu taslimu!

Umejitahidi hata kupotosha nadharia ya huruma. Ukasahau takwimu za walionyongwa kipindi cha Nyerere kulinganisha na Mwinyi zinasema je.

Umejitahidi kuiandika historia upya kuhusu struggle za wanafunzi UDSM katika kipindi cha Mwinyi.

Nimechukua muda kujiridhisha. Ukweli uko wazi:

"hakuna mwanafunzi yeyote aliyekamatwa kwenye sekeseke la matusi dhidi ya Mzee Mwinyi yakiendeshwa na Mzee Punch."

Mzee Punch aliendelea kuwa omnipotent na incognito muda wa uhai wake.

Badala yake kwenye mgomo uliozaa aliyoita Mwinyi kutukanwa matusi ya nguoni wanafunzi 10 wakiwamo James Mbatia walifukuzwa forth with jwa kilichoitwa kufutiwa udhamini.

Mkuu check facts zako historia si rahisi sana kuiandika upya.

Kama kawaida ya makondoo hudhani kisemwacho kitachukuliwa kama kilivyo.

Panapo uthubutu wa kuhoji fact checks hubeba sehemu yake.

Zingatia: mada ni kuuhusu misingi wa kuhoji. Mada si Nyerere wala Mwinyi bali kuparaganyika kwa misingi ya elimu.
 
Kwanza umekosea sana unaposema kuwa mimi nazungumzia hili swala kiimani zaidi.
Kitu unachotakiwa kujua ni kwamba mimi na Mwinyi hatuchangii imani wala kabila.
Ninaochangia nao imani unaweza kuona ndio walio wengi kwenye avatar yangu, so mpaka hapo bila shaka umeshaona imani yangu ni ipi.

Lakini pia hata hao wa kwenye avatar yangu sikuwaweka kwa sababu ya imani zetu kuwa moja, bali kwa mchango mkubwa waliofanya kwa taifa letu.
Nimekupa sifa za Nyerere kama baba wa taifa letu alietuunganisha watanzania na kutufanya tuwe kitu kimoja, pengine bila yeye leo hii tungekuwa kama Kenya, watu wanabaguana kutokana na utofauti wa lugha, kabila nk.

Picha za Magufuli na Samia sintoziongelea maana sio mahala pake. Hata hivyo mimi nimesimama katika ukweli na nitaendelea kusimama katika ukweli kuwa Mwinyi ndio baba wa demokrasia ya kweli hapa Tanzania. Nyerere hakuwa baba wa demokrasia ndomaana aliwafunga, aliwahenyesha na wengine walikimbia wenyewe kukwepa mkono wa chuma chini ya uongozi wake. Chini ya uongozi wake kuna mengi tu mabaya yalifanyika kama alivyokiri mwenyewe baada ya kutoka madarakani, lkn hakukuwa na mtu wa kuweza kuthubutu kuyazungumza hadharan au hata kuyaandika. Ndio maana kuna siku Lisu alisema jambo Zito kuhusu Nyerere, wengi waliokuwa hawamfahamu vizuri Nyerere walimshangaa Lisu na kulaani alichoongea, lkn wale waliokuwa wanamfahamu Nyerere hawakumshangaa Lisu maana walijua ameongea ukweli, japo kwa mila zetu waafrika sio vizuri kumsema marehem kwa mabaya so wale waliomfahamu Nyerere badala ya kumuunga mkono Lisu kwa alichokisema wao waliamua kukaa kimya ili kulinda mila yetu ile ya kutomsema vibaya marehem.

Nikiwa mdogo nishawahi kutoka magomeni hadi mw/nyamala nyuma ya hospital kufuata chakula, mitaa ile kulikuwa na kanisa moja lilikuwa linagawa dawa ya mswaki, sabuni, unga wa ngano, dengu, sukari na kadhalika kilo moja moja.

Lile kanisa sijui kama bado lipo mpaka leo.

Mwinyi alivyoingia kwa huruma wake aliamua kuwaondolea watanzania mateso ya kuishi kama Mogadisho kwa kuwasogezea huduma zote muhimu karibu. Maduka yalifunguliwa, vyakula viliruhusiwa kuingia nchini, zahanati zikafunguliwa mitaani, madawa yakaruhusiwa kuuzwa, barabara zikajengwa, mabasi yakaletwa ili watu wasichelewe makazini, shule zikaongezwa, walimu ambao baadhi walikuwa washaanza kugoma kufundisha kwa kukosa mishahara wakarudi mashuleni, hela mtaani ikaanza kuonekana.

Angeamua watu waendelee kuishi kama mashetan basi angewaacha na wala yeye na familia yake wasingekuwa na hasara yoyote maana wangekula, kunywa na kuishi kama walivyoishi viongozi wengine enzi za Nyerere.

Kuhusu uhuru wa hapa JF, nimeshakujibu kwenye post namb #9
 
Weeh dogo ujamaa umeshaisha
 

Imani haina maana ya dini peke yake. Imani. Pata kamusi kujiridhisha.

Jambo la msingi hukukanusha idadi kubwa ya walionyongwa kipindi cha Mwinyi kuliko Nyerere.

Hukukanusha pia ya Mzee punch wala ya matusi ya nguoni wala wanafunzi 10 waliofukuzwa milele na Mwinyi.

Mada ni uthubutu wa kuhoji ambayo ndiyo njia pekee ya kuumaliza u Mungu wa watu.

Miungu watu huchomoza popote uthubutu wa kuhoji unapokuwa haupo. Ya JF yalikuwa ni mfano katika uendelezo huo.

NInakazia mada haimhusu awaye yote bali misingi ya elimu iliyo paraganyika. Aliyeiparaganyisha hawezi kukwepa lawama.

Nukuu ya Prof Shivji inaishi:

'Pasipo mijadala au ubunifu huwezi kuendeleza fikra, na hii inakwenda moja kwa moja kuathiri usomaji na ufundishaji.”
 
Mada inahusu uthubutu wa kuhoji. Zingatia kuwa haujadili hilo uko way ward. Kama wewe mmetajwa kwenye mada. Hamna hoja wala stamina ya kujadili lolote.

Bure kabisa.
mjadili hoja hata kupanga maneno huwezi...bladifekeni
 
Acha kudanganya Nyerere hakuwa mtu wa kuruhusu upinzani
Jiulize kwanin Nyerere hajawahi shindanishwa na mtu kwenye nafasi yake ?

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Kuna vitu vingi vimefichwa sana katika taifa kuvielewa ni ngumu sana,, kwani vyama vingi vilianza lini na Mwalimu alistafu lini na ile iliyokuwa USSR ilivunjika lini? Ukivijua hivi hatasumbuka kabisa,,,, Alikuwa raisi lakini naye alikuwa na mapungufu yake Mwalimu,,,
Katika Africa nazani ni mmoja tu alikuwepo naye NELSON MANDELA tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…