Lililokuwa taifa la kupigiwa Mfano halipo tena

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Tanzania ya enzi za Nyerere ikiheshimika kila pembe ya dunia haipo tena. Tanzania hiyo ilikuwa na misimamo yake iliyojulikana na isiyotetereka.

Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote bila Afrika yote kuwa huru. Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote kama kulikuwa na ukiukwaji haki popote duniani Ukweli huo ulifahamika hivyo na kila rafiki na hata kila adui.

Kama taifa tulikuwa wamoja na nchi ilikuwa yetu sote. Nguvu ya hoja ilitamalaki na uthubutu wa kuhoji ulisisitizwa katika nyanja zote kutokea shule za misingi.

Leo baadhi ya watu kwa nafasi na ubinafsi wao wametumia nguvu kuuuwa uthubutu wa kuhoji. Yote hiyo ikiwa kwa nia ya kujimilikisha nchi wao na familia zao. Wasijue kuwa nchi wanaiuwa pia

Leo hatushindani kwa hoja. Hoja hazijibiwi kwa hoja, bali kejeli au kwa marungu. Watu wenye hoja tofauti wanatakiwa kuufyata. Tumelazimishwa kuwa taifa la makondoo.

Matokeo yake yamekuwa watu kulia lia yanapowakuta bila kuwa na uthubutu wa kuchukua hatua. Watu wamelazimika kuwa wenye kuangalia maslahi yao binafsi yanayowagusa wao moja kwa moja. Kwa maana jitihada za kuhoji lolote zimegeuzwa kuwa ni kujichumia majanga.

Uwezo wa kujenga, kutetea au kupinga hoja haupo tena. Utanzania wetu tuliojulikana nao umeparaganyika. Kila mtu imekuwa yupo yupo tu. Leo bila aibu tunajinasibu kama mashabiki wa Man U au Arsenal.

Ni muhimu kwa Kila mmoja kujihoji amefanya nini kuifikisha hii nchi hapa.

Anasema Prof Shivji:

“Pasipo mijadala au ubunifu huwezi kuendeleza fikra, na hii inakwenda moja kwa moja kuathiri usomaji na ufundishaji.”

Kwanini kuwaziba watu midomo? Kwanini hoja kupigwa marungu? Kwanini kuitana majina? Kwanini kujikita kupambana na mleta hoja badala ya kupambana na hoja? Nk, nk.

Kwanini JF hupiga wajumbe ban, kufuta au kufunga nyuzi bila kutoa sababu zikajulikana hadharani?

"Kwanini," huhitaji majibu si marungu.
 
Kila nabii na kitabu chake. Ukitaka kujua namaanisha nini kuhusu msemo huo, basi muulize Oscar Kambona, bibi Titi Mohammed na viongozi wengine walioonja joto la jiwe la mwl Nyerere. Labda uniambie Mwinyi ndo hakutumia nguvu kubwa kuwaadhibu waliompinga.

Kuna kijana (jina simtaji) huko chuo kikuu fulan aliwahi kumchora raisi Mwinyi picha ya kudhalilisha, kijana akashukiwa na wanausalama ili wakamuadabishe, kama walivyokuwa wanawaadabisha vijana wa aina hii enzi za Nyerere.

Mwinyi alipopata taarifa aliwapigia sim fasta wana usalama na kuwaamrisha wamuachie kijana huyo haraka iwezekanavyo aendelee na masomo yake bila kujali matusi na kejeli zake alizozionesha kwake, kwa familia yake na nafasi yake kama raisi wa nchi.

Huyu kijana angefanya hivyo enzi za Nyerere pengine leo tusingekuwa nae tena.
 
Kila nabii na kitabu chake. Ukitaka kujua namaanisha nini kuhusu msemo huo, basi muulize Oscar Kambona na viongozi wengine walioonja joto la jiwe la mwl Nyerere. Kidogo uniambie Mwinyi ndo hakutumia nguvu kubwa kuwaadhibu waliompinga.

Hoja ya Kambona ilikuwa nini kumfikisha alikofikishwa? Labda tuanzie hapo.

Kuna mengine huku yaliyo ndani ya 18 zetu:

"Kwanini JF hupiga wajumbe ban, kufuta au kufunga nyuzi bila kutoa sababu zikajulikana hadharani?"
 
Wewe umelishwa propaganda na kusikiliza hoja za upande mmoja wa Nyerere na kuacha kusikiliza za upande mungine wa Kambona. Kifupi nyerere aliongoza Tanzania kwa mkono wa chuma ndio maana hakutaka upinzani wowote wa kichama au wa kimawazo.

Jiulize ni kwanini kwenye utawala wake alifuta vyama vya upinzani? Aliogopa nini kukosolewa na wapinzani? Kwanini alisababisha watu wamchoke kwa aina ya utawala wake na kutaka kumpindua mara 2?
Mtu yeyote aliefuta upinzani kwa wakati ule au huu anakuwa hana tofauti na dikteta kama kina Omar Bashiri, Museven, Mobutu nk.

Mfano wako huo ungeuelekeza kwa Mwinyi ungeeleweka maana ndio raisi wa kwanza alieruhusu kukosolewa bila kuwaadhibu wakosoaji wake. Hata hao kina hayati Mrema, Malima nk waliondoka wenyewe chamani bila kufukuzwa. Maana Mwinyi, hakumfunga mtu wala kumfukuza chama mtu kwa kigezo cha kukosolewa. Rejea waziri alierudisha mabati kwa Mwinyi baada ya kujifanya kumnyanganya hapo nyuma kabla ya kuwa raisi.
 
Kila nabii na kitabu chake. Ukitaka kujua namaanisha nini kuhusu msemo huo, basi muulize Oscar Kambona, bibi Titi Mohammed na viongozi wengine walioonja joto la jiwe la mwl Nyerere. Kidogo uniambie Mwinyi ndo hakutumia nguvu kubwa kuwaadhibu waliompinga.

Kuna kijana (jina simtaji) huko chuo kikuu fulan aliwahi kumchora raisi Mwinyi picha ya kudhalilisha, kijana akashukiwa na wanausalama ili wakamuadabishe, lkn Mwinyi akawapigia sim fasta wana usalama na kuamrisha wamuachie kijana huyo haraka iwezekanavyo aendelee na masomo yake bila kujali matusi na kejeli zake alizozionesha kwake, kwa familia yake na nafasi yake kama raisi wa nchi.

Huyu kijana angefanya hivyo enzi za Nyerere pengine leo tusingekuwa nae tena.
Mkuu Dudumizi ..Mwinyi ni Muungwana .Kuna vitu kiongozi akitilia maanani havina maana ..mambo mengine Ni madogo kiasi kwamba kiongozi akiyapuuza hayaathiri nafasi yake Wala heshima..

Hivi kiongozi kuagiza diwani auawe au kupotezwa ni Kuna faida gani ?? Ni mambo madogo tu ambayo kimamlaka hayana athari yoyote ndio maana Mwinyi hakutaka kusulubu watu.
 
Nimekusoma na ninakuhakikishia kuwa tupo watu tunasoma na kufuatilia ila watu hawasomi! Samia mdogo wangu hebu soma na ujue kuwa kuna watu vimbelembele wanatumia jina lako kujitukuza.

MimiT baada ya kuchoshwa na mambo ya CCM niliamua kukaa pembeni. Nilikuwa na TYL ya mwaka 1967 na ya TYL ya mwaka 1981, Tulipigana vita lakini hatukufanikiwa maana tulikuwa na wajuaji wengi kwenye chama. Tukaamua kukaa pembeni.

Samia okoa chama toka mikononi mwa watoto na wajukuu wa kusema waasisi. Sisi tulikuwepo ila tulitoka familia maskini au changa ndo maana tuliishia kuwekwa pembeni. Muda wetu umeisha ila usisikie wanaotaka kuzaliana. Mungu tunusuru kwa hili.
 
Wewe umelishwa propaganda na kusikiliza hoja za upande mmoja wa Nyerere na kuacha kusikiliza za upande mungine wa Kambona. Kifupi nyerere aliongoza Tanzania kwa mkono wa chuma ndio maana hakutaka upinzani wowote wa kichama au wa kimawazo.
Jiulize ni kwanini kwenye utawala wake alifuta vyama vya upinzani? Aliogopa nini kukosolewa na wapinzani? Kwanini alisababisha watu wamchoke kwa aina ya utawala wake na kutaka kumpindua mara 2?
Mtu yeyote aliefuta upinzani kwa wakati ule au huu anakuwa hana tofauti na dikteta kama kina Omar Bashiri, Museven, Mobutu nk.
Mfano wako huo ungeuelekeza kwa Mwinyi ungeeleweka maana ndio raisi wa kwanza alieruhusu kukosolewa bila kuwaadhibu wakosoaji wake. Hata hao kina hayati Mrema, Malima nk waliondoka wenyewe chamani bila kufukuzwa. Maana Mwinyi, hakumfunga mtu wala kumfukuza chama mtu kwa kigezo cha kukosolewa. Rejea waziri alierudisha mabati kwa Mwinyi baada ya kujifanya kumnyanganya hapo nyuma kabla ya kuwa raisi.

Nakuona unaruka kimanga. Hukujibu hata moja katika niliyokuuliza:

1. Hoja ya Kambona ilikuwa nini?
2. Kwenye 18 zetu kulikuwa na kwanini JF hupiga wajumbe ban, kufuta au kufunga nyuzi bila kutoa sababu zikajulikana hadharani?

Zingatia mchango wa Nyerere kwenye kuvirudisha vyama vingi na hasa alipokiri hadharani kuwa tulifanya makoss.

"Wacha maneno weka muziki."
 
Nakuona unaruka kimanga. Hukujibu hata moja katika niliyokuuliza:

1. Hoja ya Kambona ilikuwa nini?
2. Kwenye 18 zetu kulikuwa na kwanini JF hupiga wajumbe ban, kufuta au kufunga nyuzi bila kutoa sababu zikajulikana hadharani?

Zingatia mchango wa Nyerere kwenye kuvirudisha vyama vingi na hasa alipokiri hadharani kuwa tukifanya makaso.

"Wacha maneno weka muziki."
Oh kumbe hoja hapa ni swala la kupigwa ban na JF bila kupewa maelezo. Hili swala wengi wetu limeshatukuta na tukashauri hatua za kuchukuliwa kabla mtu hajapigwa ban. Mfano kumuonya mtu mara 1 au 2 kwa kosa au makosa anayofanya kabla ya kupigwa ban, pia kama muhusika aliandika au ku comment vitu visivyoeleweka basi wafute vile alivyoandika muhusika na kuzuiwa kuendelea kuchangia mada ya thread husika (sio azuiwe kuchangia mada zingine) mpaka pale atapoonekana kwamba ameendelea kukiuka onyo alilopewa ndo apewe sasa ban.
 
Wewe umelishwa propaganda na kusikiliza hoja za upande mmoja wa Nyerere na kuacha kusikiliza za upande mungine wa Kambona. Kifupi nyerere aliongoza Tanzania kwa mkono wa chuma ndio maana hakutaka upinzani wowote wa kichama au wa kimawazo.
Jiulize ni kwanini kwenye utawala wake alifuta vyama vya upinzani? Aliogopa nini kukosolewa na wapinzani? Kwanini alisababisha watu wamchoke kwa aina ya utawala wake na kutaka kumpindua mara 2?
Mtu yeyote aliefuta upinzani kwa wakati ule au huu anakuwa hana tofauti na dikteta kama kina Omar Bashiri, Museven, Mobutu nk.
Mfano wako huo ungeuelekeza kwa Mwinyi ungeeleweka maana ndio raisi wa kwanza alieruhusu kukosolewa bila kuwaadhibu wakosoaji wake. Hata hao kina hayati Mrema, Malima nk waliondoka wenyewe chamani bila kufukuzwa. Maana Mwinyi, hakumfunga mtu wala kumfukuza chama mtu kwa kigezo cha kukosolewa. Rejea waziri alierudisha mabati kwa Mwinyi baada ya kujifanya kumnyanganya hapo nyuma kabla ya kuwa raisi.
Nyerere alifuta vipi vyama vya upinzani wakati ni yeye ndie aliruhusu vianze kuwepo licha ya kupingwa na wengi kwenye chama chake?

Usichanganye Nyerere kuvifuta vyama vya upinzani wakati wa kupigania Uhuru na baada ya hapo, wakati wa kupigania Uhuru ilikuwa ni vyema kwake kufanya alivyofanya ili kuwaunganisha watanzania kwa muda mfupi, wawe na lengo moja, ili kufikia matarajio waliyojiwekea.

Kuruhusu vyama vya upinzani kabla ya uhuru kungekuwa ni kuvurugana wenyewe kwa wenyewe hapa ndani, hivyo mkoloni angetumia mvurugano wetu kuendelea kututawala kirahisi, mimi niko na Nyerere kwenye hilo.
 
Kwa mtazamo wangu vipo vitu vjngi vinavyoashiria kudumaa kwa fikra ikiwemo humu JF na hasa hili Jukwaa la Siasa.

Ukiachilia mbali hizo ban unazolalamikia mtu kupigwa bila kupewa haki ya kujieleza, japo hapa ningesisitiza watumiaji wa jukwaa wawe wanajikumbusha sheria na kanuni zinazotawala..

Lakini pia tatizo la kudumaa kifikra lina extend mpaka kwa watumiaji wa hili jukwaa.

Uwepo wa makundi yanayoshabikia vyama vya siasa ndio chanzo cha haya yote, hii imesababisha wengi toka pande tofauti kushindwa kuwa wakweli/wazi pale jambo baya linapotokea upande wao, huamua kulifumbia macho, wengi husubiri mpaka litokee upande wa pili ndio waseme.

Kwangu hili pia linasababisha kudumaza wengi kifikra, hatupati nafasi ya kujadili mambo kwa mapana yake kwa sababu ya mahaba na ushabiki kwa vyama tuvipendavyo.
 
Oh kumbe hoja hapa ni swala la kupigwa ban na JF bila kupewa maelezo. Hili swala wengi wetu limeshatukuta na tukashauri hatua za kuchukuliwa kabla mtu hajapigwa ban. Mfano kumuonya mtu mara 1 au 2 kwa kosa au makosa anayofanya kabla ya kupigwa ban, pia kama muhusika aliandika au ku comment vitu visivyoeleweka basi wafute vile alivyoandika muhusika na kuzuiwa kuendelea kuchangia mada ya thread husika (sio azuiwe kuchangia mada zingine) mpaka pale atapoonekana kwamba ameendelea kukiuka onyo alilopewa ndo apewe sasa ban.

Hoja si kupigwa ban mkuu. Kupigwa ban, kufutwa nyuzi au kufungwa nyuzi hiyo ni mifano tu.

"Hoja ni kuuwawa kwa uthubutu wa kuhoji."

Madhara yake ni makubwa kuliko faida. Leo kama taifa si kama tulivyokuwa.

Nyarere alifuta vyama vingi akiwa na sababu zake alizokuja kukiri zilikuwa fyongo. Alitofautiana na kina Kambona, hata watoto mapacha hutokea kugombana.

Bila ya dababu za kutofautiana kuwekwa wazi vipi kumnyooshea kidole Nyerere?

Nyerere alihimiza uthubutu wa kuhoji kwa nguvu zote na matokeo yake tulikuwa na taifa lenye nguvu.

Leo watoto wanabakwa na kulawitiwa mashuleni. Udumavu wa kuhoji umeshika Kila mahali. Madhara ya moja kwa moja ya kuuwawa kwa uthubutu wa kuhoji.

Tusiruke ruke kama bisi kwenye kikaangio. Hoja Iko wazi.
 
Tanzania ya enzi za Nyerere ikiheshimika kila pembe ya dunia haipo tena. Tanzania hiyo ilikuwa na misimamo yake iliojulikana na isiyotetereka.

Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote bila Afrika yote kuwa huru. Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana
Wakati wa nyerere nani alikuwa na nguvu ya kuhofi ikiwa salamu ya chama ilikuwa kudumisha fikra za mwenyekiti wa chama, kwa kuwa aliwaaminisha watz kuwa analosema ni sahihi daima?
 
Baada ya Nyerere, walau huyu alikuwa na misimamo inayoeleweka.
Eiav3EwXkAAVrju.jpeg
 
Kwa mtazamo wangu vipo vitu vjngi vinavyoashiria kudumaa kwa fikra ikiwemo humu JF na hasa hili Jukwaa la Siasa.

Ukiachilia mbali hizo ban unazolalamikia mtu kupigwa bila kupewa haki ya kujieleza, japo hapa ningesisitiza watumiaji wa jukwaa wawe wanajikumbusha sheria na kanuni zinazotawala..

Lakini pia tatizo la kudumaa kifikra lina extend mpaka kwa watumiaji wa hili jukwaa.

Uwepo wa makundi yanayoshabikia vyama vya siasa ndio chanzo cha haya yote, hii imesababisha wengi toka pande tofauti kushindwa kuwa wakweli/wazi pale jambo baya linapotokea upande wao, huamua kulifumbia macho, wengi husubiri mpaka litokee upande wa pili ndio waseme.

Kwangu hili pia linasababisha kudumaza wengj kifikra, hatupati nafasi ya kujadili mambo kwa mapana yake kwa sababu ya mahaba na ushabiki kwa vyama tuvipendavyo.

Suala la ban, kufuta na kufunga nyuzi ni mifano tu katika hoja iliyopo. Ni kweli kuwa kuna sheria na kanuni za matumizi ya JF. Kama ilivyo sheria na kanuni hutokea wakati zikakiukwa. Utaratibu wa kutoa hukumu za wazi zenye kuonyesha makosa na adhabu ungeleta tija zaidi.

Kukupa mfano. Kwa nini uzi huu kumhusu mjumbe BAK ulifungwa?

Nikiwarejea wajumbe chawa kudumaza jukwaa, tatizo linaanzia mbali kama anavyosema Prof. Shivji.

Tatizo ni elimu yetu ilikofikishwa. Tunayoyaona sasa hayo ni matokeo tu. Siyo tatizo lenyewe.
 
Sijakuelewa maana hakuna aliyekuzuia kutoa maoni yako Wala hoja zako hapa unazoona zinaweza kusaidia katika ujenzi wa Taifa letu, pili Tambua kuwa hakuna Uhuru usio na mipaka popote pale duniani hakuna Uhuru wa namna hiyo,

Unalalamika uongozi wa jf kufuta au kuwafungia baadhi ya watu kwa muda fulani, Napo Mimi kwa hapo nawatetea na kuwaunga mkono uongozi wa humu kwa kufanya hivyo, maana huwezi ukaamka na mawazo yako na hasira zako ukaja humu ukaanza kutukana watu matusi ya nguoni bila sababu halafu uachwe tu, hiyo haiwezekana hata kidogo, Uhuru wako haupaswi uutumie kuwatukana wengine na kuwavunjia heshima na utu wao, mbona watu wengine wanakosoa kwa lugha nzuri na kueleweka vizuri tu ujumbe wao, lakini wengine unakuta hawezi kuchangia maada bila kutukana , lazima tujifunze kuvumiliana na kuheshimiana hata pale tunapotofautiana mitizamo

Pili napenda kumwambia kuwa heshima ya Tanzania bado ipo Tena Sana tu katika siasa za kikanda na kimataifa, Bado Tanzania sauti yake inasikika na kuheshimika vizuri tu, Lakini pia lazima ufahamu kuwa siasa za miaka ya sitini haziwezi kuwa sawa na leo, tuliyoyapigania wakati huo siyo tunayoyapigania yote Leo hii, mfano wakati huo Tulikuwa mstari wa mbele kusaidia ukombozi wa nchi nyingi kusini mwa Afrika lakini Leo nchi zote Ni huru, hivyo huwezi ukaendelea na siasa zile zile za miaka ya ukombozi, lazima ubadilike kulingana na wakati, lazima ujuwe Dunia imebadilika na kila mtu anapigania maslahi ya Taifa lake na nchi yake

Kwa hiyo usitulazimishe tufanye siasa za miaka ya Uhuru, kwa Sasa viongozi wetu wakiongozwa na Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani wapo mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa Tanzania inavutia wawekezaji, watalii , wafanyabiashara wakubwa, wanamichezo na kila aina ya fursa yenye maslahi kwa Taifa letu unakuja Tanzania, Viongozi wetu wanafanya juhudi za kuhakikisha kuwa uchumi wetu unastawi na kumgusa mwananchi mnyonge, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa fursa za ajira kwaa vijana zinatengenezwa iwezekanavyo ili kuwakwamua na kuwawezesha vijana kiuchumi
 
Usichanganye Nyerere kuvifuta vyama vya upinzani wakati wa kupigania Uhuru na baada ya hapo, wakati wa kupigania Uhuru ilikuwa ni vyema kwake kufanya alivyofanya ili kuwaunganisha watanzania kwa muda mfupi, wawe na lengo moja, ili kufikia matarajio waliyojiwekea.

Kuruhusu vyama vya upinzani kabla ya uhuru kungekuwa ni kuvurugana wenyewe kwa wenyewe hapa ndani, hivyo mkoloni angetumia mvurugano wetu kuendelea kututawala kirahisi, mimi niko na Nyerere kwenye hilo.

Aliruhusu vyama vya upinzani baada ya USSR kusambaratika mwaka 1991 akajua Ujamaa wake utakosa mfadhili. Lakini alivyokuwa madarakani hakuwa na upinzani. Alitawala kidikteta

Wakati wa nyerere nani alikuwa na nguvu ya kuhofi ikiwa salamu ya chama ilikuwa kudumisha fikra za mwenyekiti wa chama kwa ni sahihi daima?

Wakati wa Nyerere msimamo ulikuwa huu:

IMG_20221017_103027_006.jpg

Mengi ya ukiukaji haki ya leo yasingekuwa na nafasi.

Kwa msimamo huu madaraka yalikuwa Kwa watu. Walinzi was maslahi yao walikuwa watu wenyewe.

Msome Nyerere kumwelewa, mwana halisi was nchi hili. Wametuulia uthubutu was kuhoji tumekuwa kama mifugo ya mtu.
 
Wakati wa Nyerere msimamo ulikuwa huu:

View attachment 2389885

Mengi ya ukiukaji haki ya leo yasingekuwa na nafasi.

Kwa msimamo huu madaraka yalikuwa Kwa watu. Walinzi was maslahi yao walikuwa watu wenyewe.

Msome Nyerere kumwelewa, mwana halisi was nchi hili. Wametuulia uthubutu was kuhoji tumekuwa kama mifugo ya mtu.

Walio thubutu kumhoji Nyerere walifia jela au walikimbia nchi. Alitawala kidikteta yule mchonga meno.
 
Sijakuelewa maana hakuna aliyekuzuia kutoa maoni yako Wala hoja zako hapa unazoona zinaweza kusaidia katika ujenzi wa Taifa letu, pili Tambua kuwa hakuna Uhuru usio na mipaka popote pale duniani hakuna Uhuru wa namna hiyo,

Unalalamika uongozi wa jf kufuta au kuwafungia baadhi ya watu kwa muda fulani, Napo Mimi kwa hapo nawatetea na kuwaunga mkono uongozi wa humu kwa kufanya hivyo, maana huwezi ukaamka na mawazo yako na hasira zako ukaja humu ukaanza kutukana watu matusi ya nguoni bila sababu halafu uachwe tu, hiyo haiwezekana hata kidogo, Uhuru wako haupaswi uutumie kuwatukana wengine na kuwavunjia heshima na utu wao, mbona watu wengine wanakosoa kwa lugha nzuri na kueleweka vizuri tu ujumbe wao, lakini wengine unakuta hawezi kuchangia maada bila kutukana , lazima tujifunze kuvumiliana na kuheshimiana hata pale tunapotofautiana mitizamo

Pili napenda kumwambia kuwa heshima ya Tanzania bado ipo Tena Sana tu katika siasa za kikanda na kimataifa, Bado Tanzania sauti yake inasikika na kuheshimika vizuri tu, Lakini pia lazima ufahamu kuwa siasa za miaka ya sitini haziwezi kuwa sawa na leo, tuliyoyapigania wakati huo siyo tunayoyapigania yote Leo hii, mfano wakati huo Tulikuwa mstari wa mbele kusaidia ukombozi wa nchi nyingi kusini mwa Afrika lakini Leo nchi zote Ni huru, hivyo huwezi ukaendelea na siasa zile zile za miaka ya ukombozi, lazima ubadilike kulingana na wakati, lazima ujuwe Dunia imebadilika na kila mtu anapigania maslahi ya Taifa lake na nchi yake

Kwa hiyo usitulazimishe tufanye siasa za miaka ya Uhuru, kwa Sasa viongozi wetu wakiongozwa na Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani wapo mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa Tanzania inavutia wawekezaji, watalii , wafanyabiashara wakubwa, wanamichezo na kila aina ya fursa yenye maslahi kwa Taifa letu unakuja Tanzania, Viongozi wetu wanafanya juhudi za kuhakikisha kuwa uchumi wetu unastawi na kumgusa mwananchi mnyonge, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa fursa za ajira kwaa vijana zinatengenezwa iwezekanavyo ili kuwakwamua na kuwawezesha vijana kiuchumi

Nikupe dokezo ya yaliyopo kwenye mada:

IMG_20221017_103027_006.jpg

Ninazungumzia uthubutu wa kuhoji uliouwawa ambao leo haupo tena. Mengine ni matokeo tu.

Hakuna mahali ninapopinga members JF kupigwa ban, nyuzi kufutwa au kufungwa lakini bila sababu kuwekwa hadharani?

Labda unifahamishe kwa nini Uzi huu kumwulizia member BAK ulifungwa?

Back
Top Bottom