Tanzania ya enzi za Nyerere ikiheshimika kila pembe ya dunia haipo tena. Tanzania hiyo ilikuwa na misimamo yake iliyojulikana na isiyotetereka.
Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote bila Afrika yote kuwa huru. Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote kama kulikuwa na ukiukwaji haki popote duniani Ukweli huo ulifahamika hivyo na kila rafiki na hata kila adui.
Kama taifa tulikuwa wamoja na nchi ilikuwa yetu sote. Nguvu ya hoja ilitamalaki na uthubutu wa kuhoji ulisisitizwa katika nyanja zote kutokea shule za misingi.
Leo baadhi ya watu kwa nafasi na ubinafsi wao wametumia nguvu kuuuwa uthubutu wa kuhoji. Yote hiyo ikiwa kwa nia ya kujimilikisha nchi wao na familia zao. Wasijue kuwa nchi wanaiuwa pia
Leo hatushindani kwa hoja. Hoja hazijibiwi kwa hoja, bali kejeli au kwa marungu. Watu wenye hoja tofauti wanatakiwa kuufyata. Tumelazimishwa kuwa taifa la makondoo.
Matokeo yake yamekuwa watu kulia lia yanapowakuta bila kuwa na uthubutu wa kuchukua hatua. Watu wamelazimika kuwa wenye kuangalia maslahi yao binafsi yanayowagusa wao moja kwa moja. Kwa maana jitihada za kuhoji lolote zimegeuzwa kuwa ni kujichumia majanga.
Uwezo wa kujenga, kutetea au kupinga hoja haupo tena. Utanzania wetu tuliojulikana nao umeparaganyika. Kila mtu imekuwa yupo yupo tu. Leo bila aibu tunajinasibu kama mashabiki wa Man U au Arsenal.
Ni muhimu kwa Kila mmoja kujihoji amefanya nini kuifikisha hii nchi hapa.
Anasema Prof Shivji:
“Pasipo mijadala au ubunifu huwezi kuendeleza fikra, na hii inakwenda moja kwa moja kuathiri usomaji na ufundishaji.”
Kwanini kuwaziba watu midomo? Kwanini hoja kupigwa marungu? Kwanini kuitana majina? Kwanini kujikita kupambana na mleta hoja badala ya kupambana na hoja? Nk, nk.
Kwanini JF hupiga wajumbe ban, kufuta au kufunga nyuzi bila kutoa sababu zikajulikana hadharani?
"Kwanini," huhitaji majibu si marungu.