DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
HILI NDILO JIBU LINALOTAKIWA....
 
Mkuu, mambo ya ujenzi hayapimwi kwa macho, embu jiongeze kidogo.
Mkuu, naona unabishana ili mradi ubishane tu.
Mambo mengine ni macho na busara zako tu zinatosha kabla hata ya vipimo kaka.
Yaani unaona tofali la block likinyeshewa na manyunyu kidogo linaanza kupukutika, macho na busara yako haviwezi kujua kuwa hili mchanga ni mwingi kuliko simenti...hadi ulete vipimo?
Na utaendelea kujengea nyumba yako kweli kwa vile hujalifanyia vipimo na mtu wa kawaida tu amekuambia kuwa tofali hili ni mchanga mtu halifai....we utandelea tu kulitumia kwa vile aliyesema hakutumia vipimo?? [emoji35][emoji35]
 

Kila jambo ni Fursa kwa wengine. Acha lijengwe hivyo hivyo Kinyume na Viwango ili baadae litakaposababisha Msiba mkubwa wa Wapangaji hapo na Wapita Njia kwa nchini na Jirani basi Wauza Majeneza, Sanda na hadi Wamiliki wa Gari za Kubebea Maiti nao waweze Kufanya Biashara na Kujipatia Vipato. Siku zingine usirudie tena Kutoa Angalizo kama hili Kiongozi kwani unaharibu Biashara za wengine sawa? Naziomba Mamlaka husika ziliache hilo Jengo liende hata ghorofa 200 juu huku Nguzo zake zikiwa hivyo hivyo kama Chelewa na Mifyagio ya Mashuleni ili baadae Maafa yakitokea na wengine waneemeke.
 
Ni kihere here cha waswahili hana lolote huyu unaweza ukakuta kama alibahatika kusoma advance alisoma HKL eti nguzo nyembamba.....hajawahi kuona mtu bonge ana miguu kama tubelight kwani wanaanguka wanapo simama......kajenge ya kwake yenye beem nene
 
Hizo si nguzo za msingi ni nguzo za nje ya balcony je nguzo zinazibeba na kuishikilia hilo jengo zipo hvyo hvyo
 
Ki muonekano linatia shaka sana, inaonekana mwenye jengo anabana matumizi sana, hii inaweza kuwa hata kwenye ubora pia, wahusika wafanye structural analysis na stability ya hilo jengo. Pia watu wa OSHA wako lazy sana, hilo jengo linavunja taratibu nyingi za usalama mahali pa kazi, na linaweza kuleta madhara muda wowote.
 
Sasa unaweza kuta michoro ya structural engineer imespecify mwisho ghorafa 10, lakini mwenye jengo anaamua tu kuongeza zaidi kwa tamaa ya pesa. Maana zile nguzo ni nyembamba sana na jengo lenyewe ni jembamba kama mlingoti.
Mkuu una hata ka diploma ka civil engineering twende sawa
Ni physics tena form three O level,mambo ya centre of gravity
The higher the structre,the lower the centre of gravity
Kwa hiyo mjengo unapokwenda juu uzito inabidi upungue,halafu wabongo mnapenda sana zege,siku hizi ni steel fixing,unaweza kuunga gorofa 100 kwa mwezi tu halafu unapanga tofali
 
naomba kujua level yako ya elimu kwanza....maana ulicho kifanya niz aidi ya umbea tu..! kuna vitu vingi sana vinazingatiwa kwenye ujenzi...pengine huvijui...hujasoma hesabu...?
 
The higher the structure the lower the center of gravity?!! Umedata au???! " The lower the centre of gravity the more stable a structure is", nadhani hiki ndicho ulichomaanisha, sio?
 
Mmmhh! Ulichozungumza uko sahihi mkuu, lakini sicho kinachofanyika mtaani practically kabisa.
Taaluma yangu ni Civil Engineer, na hapo mjini kama kariakoo nimeshiriki kuanzia IPT(nikiwa chuoni) na hata baada ya chuo. Kuna majengo kama 4 hivi yalikuwa chini ya kampuni flani(jina kapuni) yamejengwa bila uwepo wa technician wana site foreman ni mafundi wazoefu tu. Engineer sijawahi kumuona mpaka nilipoondoka.
Michoro wanapewa kazi wanafunzi wa Ardhi University, anagonga mpaka mihuri ya structural engineer wenye mihuri fake. Na maisha yanaenda....
Kifupi maisha ni blaa blaa tupu yaani. Ulishawahi kuona kampuni imefungiwa kufanya kazi lakini nyumba ya pazia inafanya kwa kutumia bango la kampuni nyingine!?
Hebu kwa leo niishie tu hapa
Haya mambo hayafanywi kienyeji enyeji tu. Lazima mtu awe na permit na authorization kutoka kwa mamlaka husika; na engineer anakuwa ame approve michoro ya hilo jengo kuwa ujenzi huo ni salama. Kama hujui kitu unauliza ufahamishwe...

Mchana mwema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…