Linapokuja suala la IMANI, Waafrika wanampigania Mungu. Likija suala la Haki zao za msingi, wanamwachia Mungu awapiganie!

Katika yote unamlaumu Munguz wewe umefanya Nini kuwasaidia wale maskini waliopo mtaani kwako?

Lini umexchukua nguo ukamvisha kichaa au mtu mtaani? Mateso, kifo, magonjwa, njaa yote ni matokeo ya Mwanadamu kujitenga na Mungu.

Kwa Mungu Kuna ukamilifu, pasipo uwepo wa Mungu Kuna maafa. Angalia Nchi ambazo si za kikristo mateso yanavyo wapata watu huko
 
Kwa hiyo unataka tuwe tunamkubali nani kati ya mwanasayansi au mtu aliyesoma historia ya sayansi ?
 
Vita vya kiimani ni nini? Vikoje? Fafanua.
Ni vita watu hufanya kutetea presence ya Imani Yao katika eneo au ukanda na mara nyingi hufanyika Kwa Kuua au kuwateketeza wale wenye Imani tofauti na Yako.

Mfano: Kusambaa Kwa Uislam au Middle east na North Africa
 
Kwa hiyo unataka tuwe tunamkubali nani kati ya mwanasayansi au mtu aliyesoma historia ya sayansi ?
Jikubali wewe mwenyewe na mawazo yako.

Kisha yafanyie kazi.

Hata hao wanasayansi walianza kujikubali wao Kwanza na mawazo yao. Kisha wakayafanyia kazi.
 
Katika yote unamlaumu Munguz wewe umefanya Nini kuwasaidia wale maskini waliopo mtaani kwako?
Nimeshatoa michango mingi sana kusaidia wahitaji.

Na nimeshuhudia wahitaji wengi wakisaidiwa na binadamu sio Mungu.

Huyo Mungu ni dhana uchwara tu mliyo jitungia vichwani mwenu na kuipa sifa isizo zistahili.

Hakuna Mungu aliyewahi kusaidia kitu chochote kile

Binadamu ndio tunasaidiana sisi wenyewe kwa wenyewe.
Lini umexchukua nguo ukamvisha kichaa au mtu mtaani? Mateso, kifo, magonjwa, njaa yote ni matokeo ya Mwanadamu kujitenga na Mungu.
Thibitisha ni lini huyo Mungu alishawahi kusaidia watu?

Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wasio na hatia yeyote ile wana teseka na wanaendelea kuteseka duniani kwa njaa, vita, magonjwa na majanga mbalimbali ya asili.
Licha ya kusali sana, kuomba sana, kufunga sana na kumlilia huyo Mungu awasaidie shida zao, Lakini hakuna kinacho tokea.

Wengi wanazidi kuumia, kuteseka na kufa. Halafu huyo Mungu anayedaiwa yupo, Haonekani kusaidia kitu chochote kile!!
Kwa Mungu Kuna ukamilifu, pasipo uwepo wa Mungu Kuna maafa. Angalia Nchi ambazo si za kikristo mateso yanavyo wapata watu huko
Hata hapa Tanzania tu kwenye ukristo kuna watu wanateseka sana licha ya kumtumainia huyo Mungu.

Na si kweli kwamba nchi zenye ukristo watu hawateseki.

Wanateseka sana.

Hakuna uhusiano wowote ule wa uwepo wa ukristo na watu kutokuteseka.
 
Unakataa hakuna Mungu, mwezi unaghaa angani nani ameweka hapo? Nani alifungua fuzu la kichwa na kupachika ubongo? Nani alimweka mtoto ndani ya tumbo la mama na kuishi kwenye maji? Nani alitengeneza ngozi na kumba wanyama na samaki majini.

Mungu yupo na Mimi nimemshuhudia kwenye mambo mengi kwenye maisha yangu? Usiku ukilala, njozi unaoyoota nani amekuwekea kichwani mwako? Think vizuri Kaka.

Kama haujajiumba basi, usimdharau muumba wako, mtafute, muombe atajidhiririsha kwako.
 
Biblia inasema tafuteni nanyi mtaona,huezi achia haki Yako burebure ni akili pungufu tunaitafuta kwa bidii zote ikishindika kwa juu ya uwezo ndo tunamwachia muumbaji wa ulimwengu
Sasa kama Lazima utafute, Kuna haja gani ya kumtegemea huyo Mungu?
We kama huamini uwapo wa Mungu nakuuona huu uumbaji tata ni matokeo ya ajali hiyo ni akili Yako TU mkuu
Hakuna kitu chochote kile kilicho umbwa na Mungu.

Vitu vyote vilivyomo except man-made things, Havijaumbwa. Vimekuwepo, vipo na vitaendelea kuwepo milele.

Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.

Ni nyie tu watu wa imani, mnajaribu kufosi kwamba Ulimwengu uliumbwa.
 
Unakataa hakuna Mungu, mwezi unaghaa angani nani ameweka hapo?
Huyo Mungu na yeye kawekwa na nani?

Unalazimisha mwezi uwe umewekwa, ila una amini huyo Mungu alijiweka tu?

Kwa nini hujiulizi na huyo Mungu aliwekwa na nani?
Nani alifungua fuzu la kichwa na kupachika ubongo?
Hakuna.
Nani alimweka mtoto ndani ya tumbo la mama na kuishi kwenye maji?
Hakuna.
Nani alitengeneza ngozi na kumba wanyama na samaki majini.
Hakuna
Mungu yupo
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
na Mimi nimemshuhudia kwenye mambo mengi kwenye maisha yangu?
Thibitisha na ueleze ulimshuhudia wapi huyo Mungu kwenye maisha yako?
Usiku ukilala, njozi unaoyoota nani amekuwekea kichwani mwako? Think vizuri Kaka.
Hakuna.
Kama haujajiumba basi, usimdharau muumba wako, mtafute, muombe atajidhiririsha kwako.
Mimi sijaumbwa.

Binadamu Hawaumbwi.

Binadamu Wanazaliwa.

Una elewa hilo?
 
Jikubali wewe mwenyewe na mawazo yako.

Kisha yafanyie kazi.

Hata hao wanasayansi walianza kujikubali wao Kwanza na mawazo yao. Kisha wakayafanyia kazi.
Ni vizuri kujikubali .

Ila mambo mengine unaisingizia dini . Mfano Tanzania kila kinachofanyika wasomi wanasema ni mama ndiye ametoa hela zake lakini wasomi haohao hawajui kuwa wananchi huwa wanalipa kodi na wao huwa wanakatwa kodi kwenye mishahara yao . Aina ya elimu inayotolewa Africa ndiyo inawafanya watu kuwa wajinga na waoga , dini haihusiki .
 
Dini inahusika sana.

Maelfu ya wachungaji wana waaminisha waumini wao maisha bora ya kufikirika kwa kutegemea miujiza badala ya kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Waumini wa Mwamposa ni mfano tosha.

Hii ni mojawapo ya impact ya dini.
 
Faida yake ni kujifariji tu na kuwa na tumaini la kuishi , shida inakuja pale watu wanaposema hilo jambo ndio kweli na kufikia hatua hata ya kuuana kwa sababu ya hizo imani.
Ukiona mtu yoyote anatumia dini yake kuwa hukumu wengine hukumu za dini yake huyo ni MUHALIFU MOJA KWA MOJA bali dini ni kujihukumu wewe mwenyewe juu ya nafsi yako sawa sawa na dini yako...hukumu yoyote iliyo nje ya nafsi yako inatakiwa kuzingatia HAKI TU siyo dini yako.mfano zanzibar wanazuia watu wasile chakula mwezi wa Ramadhan huko ni kutumia dini kuhukumu nafsi za wengine ni uhalifu...na ushahidi wa hili hupo hata kwenye msahafu na biblia
 
Wale wanaopigana kwa ajili ya Allah njooni, au bado hamjafika Syria. 🤠🤠
Mwalimu nyerere angetulia tu kwa Imani, una uhakika leo hii Kagera ingekua Tanzania.

Ukraine wangetulia tu kwa Imani leo hii wangekua wapi?

Ndio mana hua nawaambia dini ni chanzo cha umasikini.
 
Umepewa ubongo,macho,miguu,mikono na kadhalika ilivikusaidie kutafuta.Aliyekuumba alijua utaishi ktk ulimwengu wa kutafuta


Kama uko makini ukiangalia viumbe vilivyo Kaa Kwa mpangilio utajua Kuna mpangaji,hebu Kwa MFA angalia jicho lako lilivo umbwa kwa ustadi

Jicho la binadamu ni ogani ya hisi inayohusika na kuona. Linaundwa na sehemu mbalimbali ambazo kila moja ina jukumu maalum. Hizi ndizo sehemu kuu za jicho na kazi zake:

1. Konia (Cornea)

Kazi: Ni tabaka la uwazi la mbele ya jicho linalolinda sehemu za ndani na kusaidia kupinda mwanga kuelekea kwenye lenzi.


2. Konjunktiva (Conjunctiva)

Kazi: Ni utando mwembamba unaofunika sehemu ya mbele ya jicho na sehemu ya ndani ya kope ili kulinda jicho dhidi ya vumbi na vijidudu.


3. Ncha ya Jicho (Pupil)

Kazi: Ni tundu katikati ya iris linalodhibiti kiasi cha mwanga kinachoingia ndani ya jicho.


4. Iris

Kazi: Hutoa rangi ya jicho na kudhibiti ukubwa wa ncha ya jicho kwa kupanua au kupunguza ili kurekebisha mwanga unaoingia.


5. Lenzi ya Jicho (Lens)

Kazi: Inapinda ili kulenga mwanga na picha kwenye retina kulingana na umbali wa kitu.


6. Retina

Kazi: Tabaka la seli zinazohisi mwanga (photoreceptors). Inabadilisha mwanga kuwa ishara za umeme zinazopelekwa kwenye ubongo.


7. Kiwango cha Maji ya Jicho (Aqueous Humor)

Kazi: Ni giligili inayosaidia kudumisha umbo la mbele ya jicho na kutoa virutubisho kwa konia na lenzi.


8. Giligili ya Jicho (Vitreous Humor)

Kazi: Giligili yenye uwazi inayojaza sehemu ya ndani ya jicho na kusaidia kudumisha umbo lake.


9. Choroid

Kazi: Tabaka lililojaa mishipa ya damu linalosambaza oksijeni na virutubisho kwa retina na sehemu nyingine za jicho.


10. Sclera

Kazi: Tabaka la nje jeupe linalotoa umbo na kulinda sehemu za ndani za jicho.


11. Mishipa ya Fahamu ya Macho (Optic Nerve)

Kazi: Inabeba ishara za umeme kutoka kwenye retina kwenda kwenye ubongo ili kufasiri picha.


12. Misuli ya Jicho (Extrinsic Muscles)

Kazi: Hudhibiti harakati za jicho ili liweze kutazama pande zote.


13. Fovia (Fovea)

Kazi: Eneo maalum la retina lenye msongamano mkubwa wa seli za photoreceptors zinazohusika na kuona kwa uwazi mkubwa.


14. Kope (Eyelids)

Kazi: Husaidia kulinda jicho dhidi ya vumbi na mwanga mkali, pamoja na kusambaza machozi juu ya uso wa jicho.


15. Tezi za Machozi (Lacrimal Glands)

Kazi: Huzalisha machozi ambayo husaidia kulainisha na kulinda jicho dhidi ya vijidudu.


Sehemu zote hizi hufanya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha mchakato wa kuona unafanikiwa.
 
Kwa nini ulizaliwa bila kupenda, unakua bila kupenda, na unakufa bila kupenda? Lini ulijipigania kuzaliwa? Lini ulijipigania kukua (to develop)? Lini ulijipigania kufa?
 
Wote ulio wataja hapa ni fictional characters. Wana exist vitabuni tu kwenye hadithi na masimulizi ya kale.

Hakuna uthibitisho wowote ule wa uwepo wao.

Hawana tofauti na Abunuwasi wa kwenye Hekaya za kutungwa tu.
Hii ni imani yako, mkuu ila hawa ni watu halisi na hadi kuna archeological findings nyingi zinazoonyesha usahihi wa biblical stories.

Dini ikifundishwa kwa usahihi, biblia ndio kitabu pekee duniani chenye principles za kufanya palipo dumqq pqendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…