Linapokuja suala la IMANI, Waafrika wanampigania Mungu. Likija suala la Haki zao za msingi, wanamwachia Mungu awapiganie!

Amekuambia wapi? Lini? Mwaka gani? Mwezi upi? Tarehe ipi? Siku ipi? Na muda gani exactly aliokwambia?
Mimi niliwahi kukata uwepo wake, lakini yeye alinitafuta na alinithibitishia kupitia ndoto, kile nilichomwomba alinijibu, nilipohitaji zungumza nae alizungumza nami kupitiia neno lake na kupitia watu mbalimbali.

Moja kubwa kuliko ni kunipa familia ambayo imenikuza kufikia hapa. Sikuwahi wafahamu wazazi wangu mpaka Leo na mara nyingi niliwahi mlaumu Mungu. Lakini nilikuja kugundua binadamu sisi tunapoanguka Mungu anatutetea na kutuinua, amenitengeneza mpaka nafikia umri huu nimeoa amenifanyia mengi. Nilipomwomba amefanya, nilipomuhitaji alikuwepo karibu.
 
Kabla ya uumbaji, Huyo Mungu alikuwa wapi?
Kabla ya magari wanadamu walikua wapi?

Kabla ya kuzaliwa wewe wazazi wako walikua wapi? God cannot die, kifo kipi Kwa sababu ya kutenganishwa na Mungu pale Eden but he gave us a second chance to live as God's maana tumeumbwa Kwa mfano wake na lengo lake lilikua kuishi milele. Hivyo Kwa wale waliobatizwa Kwa roho wataishi milele baada ya maisha ya hapa Duniani. Mwili unakufa lakini roho inaishi milele.
 
Mwanzo 1:1-3 BHN
[1] Hapo mwanzo (time), Mungu aliumba (Created maana yake something out of nothing) mbingu (space) na dunia. (matter) [2]
Aliye andika kitabu cha mwanzo ni nani?

Kabla ya hapo mwanzo, Huyo Mungu alikuwa wapi?

Huko alikokuwa ni wapi?

Na kuliumbwa na nani?
Haya ni maneno ya vitabuni tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.
 
Mimi niliwahi kukata uwepo wake, lakini yeye alinitafuta na alinithibitishia kupitia ndoto, kile nilichomwomba alinijibu, nilipohitaji zungumza nae alizungumza nami kupitiia neno lake na kupitia watu mbalimbali.
Alikutafuta lini? Mwaka gani? Mwezi upi? Tarehe ipi? Siku ipi? Na muda gani exactly aliokutafuta?
Huyo Mungu unayedai anatutetea na kutuinua, Anashindwaje kuwainua na kuwatetea maelfu ya wanawake na watoto wanaoteseka duniani kwa njaa, vita, magonjwa na majanga mbalimbali ya asili yanayotokea duniani?
 
Kabla ya magari wanadamu walikua wapi?
Wanadamu walikuwa hapahapa duniani.
Kabla ya kuzaliwa wewe wazazi wako walikua wapi?
Walikuwa kwa wazazi wao, Ambao ni bibi na babu zangu.
Binadamu Hawaumbwi.

Binadamu Wanazaliwa.

Ni wewe unajaribu kufosi kwamba binadamu wanaumbwa.

Binadamu Hawaumbwi na hatujaumbwa.

Binadamu tunazaliwa kutoka kwa wazazi wetu.
 
Mkuu unafikiri basi hata huko kwenye hizo dini zao cha mchongo wapo kihivyo basi 🤔 hawa tupo nao kila siku kidimbwi tukipanda juu ya meza na kushindania kuzipata UTI mbona🤔
Tuna unafiki wa kiwango cha lami. Juzi jumamosi kuna wamama walikuwa wanaenda jumuiya, ee bwana walikuwa wanamsengenya mwenzao hatari, nikajisemea eti wanaenda kusali hawa, si bora wangekaa nyumbani.
 
Imani sio kutokiwa na uhakika. Imani ni kuwa na uhakika na kitu ambacho bado hakijakuwa au hakijakuwepo.

Ndio maana mtu qnasema naimani notafika mwakani. Anauhakika na usadikisho binafsi kuwa atafika wakati uwezekano wa kufika hauko mikononi mwake. Hii ndio imani.
Hata wewe unayo ndio maana unapanga malengo ya mwakani, au unaupangia mshahara au faida matumizi hata kabla haujaupata. Maana kati yako na mwisho wa mwezi kunauwezekano mwingi tu wa kuukosa.
 
Naona umenijibu nje ya mstari
 
Kuhusu kuvuka barabara uhakika wa kutumia macho ni mdogo sana. Bado ndani yako kuna vitu usivyonauhakika navyo ambavyo vinaweza kukutokea katika mchakato wa kuvuka, mfano ukazimia au ukapata mshtuka.

Ili uwe na uhakika labda useme kabla hujavuka ukafanye full body chekup na uwe na uhakika ya precission ya vifaa na mtu atakayekupa majibu kama hawezi kutumiwa.

Sisi watu wa Biblia Imani ni kuwa na uhakika katikati ya mazingira yasiyoonyesha kabisa uhakika. Maana tunauhakika na unseen realm ambayo inaratibu kila kinachoendelea duniani.
Ufalme wa Mungu.


Kama dini hizihizi hasa Biblia ikifundishwa kwa usahihi inaweza kuwa catalyst kubwa ya maendeleo kuliko kumpinga Mungu. Maendeleo yote duniani yalianzia Ulaya. Na ulaya yalianza baada ya watu kusoma Biblia privatelu nje ya mifumo ya kitaasisi ambayo ilikuwa inaitumia Biblia kama chanzo cha kutawalia watu na kuwatumia kwa kuwafunga na sio kuwafungua akili wafanye yasiyowezekana.
 
Imani sio kutokiwa na uhakika. Imani ni kuwa na uhakika na kitu ambacho bado hakijakuwa au hakijakuwepo.
Unaona unavyo jichanganya mwenyewe, Kwenye hii post ulisema imani ni kutokuwa na uhakika. Na ukatoa mfano kabisa kwamba " Hata kusema kesho nitaenda kazini ni imani. Maana hauna uhakika"👇

Halafu tena sahivi unabadilika unasema imani ni kuwa na uhakika?

Hivi unazingatia unacho andika kweli?

Huoni kwamba una ji contradict mwenyewe hapa?
Ndio maana mtu qnasema naimani notafika mwakani. Anauhakika na usadikisho binafsi kuwa atafika wakati uwezekano wa kufika hauko mikononi mwake. Hii ndio imani.
Hana uhakika kwamba atafika mwakani, ndio maana anaweka imani.

Angekuwa na uhakika wa kufika mwakani, Asingeweka imani.

Una elewa?
Hata wewe unayo ndio maana unapanga malengo ya mwakani, au unaupangia mshahara au faida matumizi hata kabla haujaupata. Maana kati yako na mwisho wa mwezi kunauwezekano mwingi tu wa kuukosa.
Acha kujichanganya mwenyewe!!

Elewa unacho andika.
 
Acha kuleta ufafanuzi uchwara usio na logic.

Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu.
 
Kwa hiyo, hata kifo ni asili siyo? Then, why ask: why does the sun shine, or why does the rain fall and the wind blows?
 
Imqni ni kuwa na uhakika na mambo ambayo kikawaida hayana uhakika.

Ushahidi wa uhakika huo sio sayansi bali kauli za Mungu.

Hapo nilikuwa nakupa mfano wewe unayesema huna Imani wakati kunamambo mengi unayafanya kwa imani kwa sababu hayana uhakika na lazima uyafanye tu.

Sisi watu wa Mungu hayohayo ambayo hayana uhakika kibinadamu uhakika wetu au ushahidi wa uhak8ka wetu sio physical au scientific au biological au environmental bali ni kauli za Mungu au neno.

Naona kama wewe ndio unajijanganya nilipoongea kutokea upanxe wako na ninapoongea kwa kitokea upande wangu wa uhakika kwa yasiyokuwa na uhakika
 
Imani ni hali ya kukubali jambo bila uthibitisho / uhakika , ndio maana kila siku mnajaribu kuthibitisha uwepo wa Mungu bila kujua uwepo wa Mungu ni imani tu.
 
Imani ni hali ya kukubali jambo bila uthibitisho / uhakika .
Asilimia 90 ya mambo wanadamu wanayofanya hayana uthibitisho au uhakuka 100%. Kwa hiyo pasipo imani hakuna maisha.

Sisi watu wa Mungu, uthibitisho wetu ni kauli za Mungu juu ya jambo husika. Na kuna ushahidi ambao haupimiki au hauelezeki kisayansi au kimazingira ni ushahidi wa uzoefu ( evidence of experience).
Mfano upepo hatuuoni ila tunaexperience matokeo yake.

Kwa Mungu hatua ya awali kabisa ya imani ni kwa ushahidi wa uzoefu wa mtu kumuamini na matokeo yake.
 
Upepo unapimika kabisa labda wewe tu ndio haujui?
 
Mungu ni nadharia tu iliyotengenezwa vichwani mwa watu baada ya kukosa majibu ya maswali magumu waliyokuwa wanajiuliza , ndio maana dhana hiyo ipo tofauti miongoni kwa kila jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…