Linapokuja suala la IMANI, Waafrika wanampigania Mungu. Likija suala la Haki zao za msingi, wanamwachia Mungu awapiganie!

Linapokuja suala la IMANI, Waafrika wanampigania Mungu. Likija suala la Haki zao za msingi, wanamwachia Mungu awapiganie!

Umepewa ubongo,macho,miguu,mikono na kadhalika ilivikusaidie kutafuta.Aliyekuumba alijua utaishi ktk ulimwengu wa kutafuta
Sijaumbwa na Mungu.

Binadamu Hawaumbwi.

Binadamu Wanazaliwa.

Huyo Mungu ni wewe umemtunga huko kichwani mwako, Halafu unaanza kufosi kwamba ndio ameniumba.

Hakuna Mungu Aliyeumba kitu chochote kile.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Mungu ni dhana ya kufikirika mliyo jitungia vichwani mwenu tu haipo katika uhalisia, Na wala huwezi kuthibitisha uwepo wake.
Kama uko makini ukiangalia viumbe vilivyo Kaa Kwa mpangilio utajua Kuna mpangaji,hebu Kwa MFA angalia jicho lako lilivo umbwa kwa ustadi
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na mpangiliaji wake, Hata mpangiliaji wa kila kitu lazima awe na mpangiliaji wake mwingine.

Huyo mpangaji na yeye lazima awe na mpangaji wake mwingine. Mpangaji huyo hawezi ku exist tu mwenyewe from nowhere.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina mpangiliaji wake, Hata Ulimwengu na vitu vyote vilivyomo except man-made things, Havina Muumbaji.
Jicho la binadamu ni ogani ya hisi inayohusika na kuona. Linaundwa na sehemu mbalimbali ambazo kila moja ina jukumu maalum. Hizi ndizo sehemu kuu za jicho na kazi zake:

1. Konia (Cornea)

Kazi: Ni tabaka la uwazi la mbele ya jicho linalolinda sehemu za ndani na kusaidia kupinda mwanga kuelekea kwenye lenzi.

2. Konjunktiva (Conjunctiva)

Kazi: Ni utando mwembamba unaofunika sehemu ya mbele ya jicho na sehemu ya ndani ya kope ili kulinda jicho dhidi ya vumbi na vijidudu.

3. Ncha ya Jicho (Pupil)

Kazi: Ni tundu katikati ya iris linalodhibiti kiasi cha mwanga kinachoingia ndani ya jicho.

4. Iris

Kazi: Hutoa rangi ya jicho na kudhibiti ukubwa wa ncha ya jicho kwa kupanua au kupunguza ili kurekebisha mwanga unaoingia.

5. Lenzi ya Jicho (Lens)

Kazi: Inapinda ili kulenga mwanga na picha kwenye retina kulingana na umbali wa kitu.

6. Retina

Kazi: Tabaka la seli zinazohisi mwanga (photoreceptors). Inabadilisha mwanga kuwa ishara za umeme zinazopelekwa kwenye ubongo.

7. Kiwango cha Maji ya Jicho (Aqueous Humor)

Kazi: Ni giligili inayosaidia kudumisha umbo la mbele ya jicho na kutoa virutubisho kwa konia na lenzi.

8. Giligili ya Jicho (Vitreous Humor)

Kazi: Giligili yenye uwazi inayojaza sehemu ya ndani ya jicho na kusaidia kudumisha umbo lake.

9. Choroid

Kazi: Tabaka lililojaa mishipa ya damu linalosambaza oksijeni na virutubisho kwa retina na sehemu nyingine za jicho.

10. Sclera

Kazi: Tabaka la nje jeupe linalotoa umbo na kulinda sehemu za ndani za jicho.

11. Mishipa ya Fahamu ya Macho (Optic Nerve)

Kazi: Inabeba ishara za umeme kutoka kwenye retina kwenda kwenye ubongo ili kufasiri picha.

12. Misuli ya Jicho (Extrinsic Muscles)

Kazi: Hudhibiti harakati za jicho ili liweze kutazama pande zote.

13. Fovia (Fovea)

Kazi: Eneo maalum la retina lenye msongamano mkubwa wa seli za photoreceptors zinazohusika na kuona kwa uwazi mkubwa.

14. Kope (Eyelids)

Kazi: Husaidia kulinda jicho dhidi ya vumbi na mwanga mkali, pamoja na kusambaza machozi juu ya uso wa jicho.

15. Tezi za Machozi (Lacrimal Glands)

Kazi: Huzalisha machozi ambayo husaidia kulainisha na kulinda jicho dhidi ya vijidudu.

Sehemu zote hizi hufanya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha mchakato wa kuona unafanikiwa.
Jicho halijaumbwa.

Binadamu anazaliwa akiwa na macho automatically.
 
U
Waafrika dini zimewapumbaza sana. Waafrika wanamuachia kila kitu Mungu wa Israel awapiganie wakati waisrael wao wanapigana kwa makombora na wanalindwa na mifumo bora ya ulinzi, hawajamuachia Mungu wao awalinde kwa sababu wanajua Mungu ni hadithi za sungura na fisi na huyo Mungu hayupo na wala uwezo wa kuwalinda hana.
Unachokisema sijuii kama unakielewa ELEWA sasa MUNGU yupo na ataendelea kuwapo milele
 
Kwa nini ulizaliwa bila kupenda, unakua bila kupenda, na unakufa bila kupenda?
Hiyo ni asili jinsi ilivyo.

Ili viumbe vingine viweze kupata nafasi ya kuishi lazima viumbe vingine vife, vipungue. Vitoe nafasi kwa viumbe vipya.

Sasa kama tungekuwa hatufi, Dunia ingetosheleza kumudu ongezeko la binadamu na viumbe hai wote kwa miaka yote?

Pia jiulize kama huyo Mungu yupo, Kwa nini alikuumba bila ruhusa(idhini) yako kwanza?
Lini ulijipigania kuzaliwa? Lini ulijipigania kukua (to develop)? Lini ulijipigania kufa?
Hatujipiganii kuzaliwa, kukua wala kufa.

Process zote hizi hutokea automatically pasipo kufanywa na yoyote.
 
Moja ya uzi bora kabisa kwa miaka yote.

Lakini cha kushangaza likija suala la kutetea na kupigania haki zao za msingi katika jamii wanamwachia Mungu awapiganie! Na huyo Mungu hajawahi kuwapigania kwa lolote.
 
Hii ni imani yako, mkuu
Mimi sina imani. Sihitaji kuamini Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.
ila hawa ni watu halisi na hadi kuna archeological findings nyingi zinazoonyesha usahihi wa biblical stories.
Leta utafiti au evidence ya archeological findings ya hao kina Musa na Bible characters wengine.
Dini ikifundishwa kwa usahihi, biblia ndio kitabu pekee duniani chenye principles za kufanya palipo dumqq pqendelee.
Biblia ni hadithi za kutungwa tu.

Sawa na hekaya za Abunuwasi.
 
Moja ya uzi bora kabisa kwa miaka yote.

Lakini cha kushangaza likija suala la kutetea na kupigania haki zao za msingi katika jamii wanamwachia Mungu awapiganie! Na huyo Mungu hajawahi kuwapigania kwa lolote.
Hata hapa kwenye huu uzi, Unaona wazi wanavyo kazana kumpigania huyo Mungu wao wa kufikirika.

Binadamu ni kiumbe mpumbavu sana kwenye maswala ya Imani.

Badala ya kujipigania na kujitetea mwenyewe, Anatetea kiumbe cha kufikirika kiitwacho Mungu!!
 
Moja ya uzi bora kabisa kwa miaka yote.

Lakini cha kushangaza likija suala la kutetea na kupigania haki zao za msingi katika jamii wanamwachia Mungu awapiganie! Na huyo Mungu hajawahi kuwapigania kwa lolote.
Iyo Moyo kifuanu mwako nani anafanya udunde?

Yani hewa unavuta ndio uhai tu?

Nani anakuamsha asubuhi, nani analileta jua Kila baada ya masaa kumi na mbili? Nani kafanya dunia izunguke, nani aliweka utumbo na hormones, na miahipa midogo kabisa kwenye mwili wako? Kwa kweli watu kama nyie hata wazazi mnaweza kuwaambia mitaa imenilea
 
sijasoma yote uliyoandika ñakubaliana na wewe 100% kwa hili
Huu ndio uhalisia mkuu.

Haijalishi mtu anakubali au anakataa.

That's the reality.

You can avoid the reality, But you can never avoid the consequences of avoiding the reality.

Life will show you the reality by fire by force.
 
Iyo Moyo kifuanu mwako nani anafanya udunde?
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimefanywa na kiumbe kingine, Hata hicho kiumbe kinachofanya lazima kiwe kimefanywa.

You cannot exclude huyo Mungu kwenye hii Logic ya kufanywa.

Hata huyo Mungu lazima awe amefanywa.

Na ndio uanze kueleza na kuthibitisha huyo Mungu na yeye alifanywa na nani?

Usilazimishe "Moyo kudunda" kulifanywa na Mungu, ilhali bado hujathibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Thibitisha kwanza uwepo wa huyo Mungu na thibitisha huyo Mungu alifanywa na nani pia?
Yani hewa unavuta ndio uhai tu?

Nani anakuamsha asubuhi, nani analileta jua Kila baada ya masaa kumi na mbili? Nani kafanya dunia izunguke, nani aliweka utumbo na hormones, na miahipa midogo kabisa kwenye mwili wako? Kwa kweli watu kama nyie hata wazazi mnaweza kuwaambia mitaa imenilea
Nani alifanya huyo Mungu awepo?

Hili swali mbona hujiulizi?

Unarukia kwenye vitu vingine?

Anza kwanza kujiuliza na uthibitishe huyo Mungu alifanywa na nani?
 
Kama b
Sijaumbwa na Mungu.

Binadamu Hawaumbwi.

Binadamu Wanazaliwa.

Huyo Mungu ni wewe umemtunga huko kichwani mwako, Halafu unaanza kufosi kwamba ndio ameniumba.

Hakuna Mungu Aliyeumba kitu chochote kile.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Mungu ni dhana ya kufikirika mliyo jitungia vichwani mwenu tu haipo katika uhalisia, Na wala huwezi kuthibitisha uwepo wake.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na mpangiliaji wake, Hata mpangiliaji wa kila kitu lazima awe na mpangiliaji wake mwingine.

Huyo mpangaji na yeye lazima awe na mpangaji wake mwingine. Mpangaji huyo hawezi ku exist tu mwenyewe from nowhere.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina mpangiliaji wake, Hata Ulimwengu na vitu vyote vilivyomo except man-made things, Havina Muumbaji.

Jicho halijaumbwa.

Binadamu anazaliwa akiwa na macho automatically.
Kama binadamu ana zaliwa basi kwa vyovyote anamwanzo,Sasa nani alimzaa binadamu WA kwanza?
 
Imani za kidini barani Afrika ni zaidi ya madawa ya kulevya zimeharibu akili na mfumo mzima wa kufikiri wa waafrika.

Linapokuja suala la udini Waafrika wanampigania Mungu kwa nguvu zao zote wakitetea dhana ya kufikirika ambayo hawawezi hata kuithibitisha uwepo wake. Tena unakuta wanaipigania kwa nguvu zote na mabishano makali kabisa.

Lakini huyo Mungu wanaye mpigania miaka nenda rudi hajawahi kuonekana, kujitokeza, kujidhihirisha wala kuwasaidia chochote. Ni watu tu wanabaki kudai, kujifariji na kujipa matumaini uchwara kwamba wanasaidiwa na "Mungu" ilhali kiuhalisia ni wao wenyewe wanahenyeka na kukabiliana na matatizo yao.

Lakini cha kushangaza likija suala la kutetea na kupigania haki zao za msingi katika jamii wanamwachia Mungu awapiganie! Na huyo Mungu hajawahi kuwapigania kwa lolote.

Waafrika maskini wanazidi kuhujumiwa na viongozi wao wa kiserikali, Kodi zao zinaliwa, Haki zao zinaminywa, Mali na rasilimali zao zinaporwa na kutumiwa hovyo hovyo tu.

Halafu watu wanabaki kutulia na kusema tunamwachia Mungu, Mungu atatusaidia, Mungu atatulipia na kutupigania.

Sasa unajiuliza hizo nguvu za kumpigania huyo Mungu wa kufikirika kwenye dini,
Wakizielekeza na kuzitumia kwenye kupigania haki zao za msingi katika jamii zao si wataishi maisha safi kabisa?

Lakini kwa vile wengi wa waafrika wamesha pumbazwa na kuaminishwa utajiri na ufalme wa kufikirika mbinguni wala hawajihangaishi kupigania haki zao za msingi hapa duniani.

Watu wanaishi kwa kujipa matumaini uchwara ya maisha bora ya kufikirika mbinguni. Huku wakizidi kuteseka na umaskini wao, kuhujumiwa na kusulubishwa ipasavyo na viongozi wao wa serikali.

Katika maswala ya "Imani" binadamu ni kiumbe mpumbavu sana. Badala ya kujipigania yeye mwenyewe, Anapigania dhana ya kufikirika iitwayo Mungu ambayo kiuhalisia hata haijawahi kuwepo na haipo kujidhihirisha yenyewe.

No amount of prayers, faith, hope and grace can solve your problems in life for you.

No matter how strong you shout or scream the name of God in what you call praying, Your life will be miserable if you don't think, reason, plan and take productive actions to solve your own problems in life.

During those darkest moments in life when it feels like God has abandoned you, Remember that God was never with you in the first place. Because he doesn't exist in reality. He exists only in your head and in your imaginations.

The same God who has disappointed uncountable people in the world, Keep disappointing many people daily including you.

Any country waiting for God to come and help them will forever remain poor economically, medically, academically, technologically until such mental slavery religious faith is totally abolished.

Any person waiting for God to come and solve his or her problems in life will forever remain poor financially, Until such mental slavery religious faith is totally abolished.

In the jungle of life salvation is largely on your hands. No God, spiritual power or ritual can solve your problems.

If you are born into a poor financial foundation and you keep waiting for God to come and help you, You will suffer financially and die miserably.

Poverty strikes hard when laziness and ignorance is combined with prayers.

Take this bitter truth and let it sink deep in your mind.

I'm out.
Fakti.
 
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimefanywa na kiumbe kingine, Hata hicho kiumbe kinachofanya lazima kiwe kimefanywa.
Huyu ni mungu wako wewe wa kumuweka dirishani kama wahindi.

Ili awe Mungu lazima asiwe affected by time, space and matter. Na Mungu wetu anafit vizuri sana katika hayo.

He is alpha and Omega, ametuambia Jana ilikuaje na ametupa revelation of things to come meaning he knows tomorrow.

He cannot be fitted in his creation meaning he had to be outside his creation in able to make it, we know that kwenye genesis uumbaji alivyofanya. Matter, he is not affected by matter, he can be anywhere anytime.

Huyo mungu wako unaetaka kumdefine is artificial not the supreme God. Kama alifanya Kila kitu kwenye dunia na Bado the universe binadamu hatujahi hata kutoka nje ya solar system, imagine how great yey alivyo
You cannot exclude huyo Mungu kwenye hii Logic ya kufanywa.

Hata huyo Mungu lazima awe amefanywa.

Na ndio uanze kueleza na kuthibitisha huyo Mungu na yeye alifanywa na nani?

Usilazimishe "Moyo kudunda" kulifanywa na Mungu, ilhali bado hujathibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Thibitisha kwanza uwepo wa huyo Mungu na thibitisha huyo Mungu alifanywa na nani pia?

Nani alifanya huyo Mungu awepo?

Hili swali mbona hujiulizi?

Unarukia kwenye vitu vingine?

Anza kwanza kujiuliza na uthibitishe huyo Mungu alifanywa na nani?
 
Kama b

Kama binadamu ana zaliwa basi kwa vyovyote anamwanzo,Sasa nani alimzaa binadamu WA kwanza?
Binadamu wa kwanza kutokea wapi na kwa nani?

Huo "mwanzo" kabla ya kuwa mwanzo, ulikuwa wapi?

Huko ulikokuwa ni wapi na kulifanyikaje?
 
Mimi sina imani. Sihitaji kuamini Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Leta utafiti au evidence ya archeological findings ya hao kina Musa na Bible characters wengine.

Biblia ni hadithi za kutungwa tu.

Sawa na hekaya za Abunuwasi.
Hakuna mtu ambaye hana imani.
Sema mimi sina imani na Mungu na maandiko ya Biblia.

Hata kusema kesho ntaenda kazini ni imani. Maana hauna uhakika usiku nini kitakupata.

Hata kuvuka barabarq inahitaji imani kwamba ntavuka salama maana kuna factor nyingi ndani na nje ya uwezo wako zinazoweza kukusababisha ukaishia hapohapo barabarani.
 
Huyu ni mungu wako wewe wa kumuweka dirishani kama wahindi.

Ili awe Mungu lazima asiwe affected by time, space and matter. Na Mungu wetu anafit vizuri sana katika hayo.
Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu kabla ya kuanza kusema kwamba hawi affected na time, space and matter.

Kwanza thibitisha ulijuaje yupo?

Na unathibitisha vipi huyo Mungu wako hawi affected na time, space and matter?

Au ni mawazo yako tu ya kufikirika?
He is alpha and Omega, ametuambia Jana ilikuaje na ametupa revelation of things to come meaning he knows tomorrow.
Amekuambia wapi? Lini? Mwaka gani? Mwezi upi? Tarehe ipi? Siku ipi? Na muda gani exactly aliokwambia?
He cannot be fitted in his creation meaning he had to be outside his creation in able to make it, we know that kwenye genesis uumbaji alivyofanya. Matter, he is not affected by matter, he can be anywhere anytime.
Kabla ya uumbaji, Huyo Mungu alikuwa wapi?

Huko alikokuwa kulitoka wapi?

Na kuliumbwa na nani?

Maana uumbaji ulikuwa bado haujafanyika kabisa.

Sasa yeye huyo Mungu alikuwa wapi kabla ya uumbaji?

Huko alikokuwa kuliumbwa na nani?
Huyo mungu wako unaetaka kumdefine is artificial not the supreme God. Kama alifanya Kila kitu kwenye dunia na Bado the universe binadamu hatujahi hata kutoka nje ya solar system, imagine how great yey alivyo
Hakuna Supreme God, Kuna Fictional God.

Ambaye mpaka sasa umeshindwa kuthibitisha uwepo wake.
 
Hakuna mtu ambaye hana imani.
Sema mimi sina imani na Mungu na maandiko ya Biblia.
Imani ni kutokuwa na uhakika.

Ukishakuwa na uhakika, imani haihitajiki tena.
Hata kusema kesho ntaenda kazini ni imani. Maana hauna uhakika usiku nini kitakupata.
Huna uhakika nini kitakupata usiku, Ndio maana unaweka imani.

Hapa tayari umethibitisha msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.

Pia huna uhakika wa uwepo wa huyo Mungu, Ndio maana una imani.

Kwa hivyo huwezi kuhitimisha moja kwa moja kwamba Mungu yupo, Kwa sababu bado hauna uhakika wa uwepo wa Mungu.

Ni imani zako tu zisizo na uthibitisho wowote ule.
Hata kuvuka barabarq inahitaji imani kwamba ntavuka salama maana kuna factor nyingi ndani na nje ya uwezo wako zinazoweza kukusababisha ukaishia hapohapo barabarani.
Hatuvuki barabara kwa imani, Tunavuka barabara kwa uhakika.

Ndio maana kabla ya kuvuka barabara tunaangalia kulia na kushoto, kisha tena kulia na kushoto. Kufanya uhakiki wa je ni salama kuvuka kwa wakati huo?

Tukisha jiridhisha na kupata uhakika kwamba hakuna gari lolote lile na kwamba ni salama kuvuka, Ndipo tunavuka kwa uhakika kwamba ni salama.

Hivyo hatuvuki barabara kwa imani bali kwa uhakika.
 
U

Unachokisema sijuii kama unakielewa ELEWA sasa MUNGU yupo na ataendelea kuwapo milele
Kati ya wewe unaeamini Mungu wa Israel na Israel wenyewe ni nani anaemjua vizuri huyo Mungu? Kwa nini waisraeli wasiache huyo Mungu ambae wewe unaamini ana nguvu, ana uwezo, anajua kila kitu awalinde badala yake wanajilinda kwa mifumo bora ya ulinzi?

Kama yupo, yuko wapi mkuu?
 
Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu kabla ya kuanza kusema kwamba hawi affected na time, space and matter.
Mwanzo 1:1-3 BHN
[1] Hapo mwanzo (time), Mungu aliumba (Created maana yake something out of nothing) mbingu (space) na dunia. (matter) [2] Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji. [3] Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa.

Maneno kwenye kitabu Cha mwanzo vyote vinafit perfectly to explain God's nature of creating time, space and matter.
 
Back
Top Bottom