6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Niaje waungwana,
Waungwana najua wengi humu mnashauku kubwa sana ya kutaka kujua ni kwanini Israel mpaka leo tar 10/10 haijaishambulia Iran, licha ya kusema na kuapa kuwa itaishambulia na kuiangamiza Iran from day one ya shambulizi lile la pili la Iran nchini Israel ambalo lililenga shabaha iliyokusudiwa na washambuliaji (Iran), kwa kulenga tu kambi za jeshi na ofisi za mosad (sio nyumba za raia) hata kama wanajua kuwa kina Netanyahu na genge lake wana utaratibu ule ule wa kujificha katika nyumba za watu wa kawaida ili kukwepa angamizo ambalo linaweza kusababishwa na shambulizi lolote la Iran (kivita hilo linafahamika).
Sasa kinyume na matarajio ya wengi kuhusu kauli zilizotolewa na kina Netanyahu, mpaka leo hii hakuna kilichofanyika. Sio kwamba Israel haitaki kuishambulia Iran ili angalau kulipiza kisasi cha shambulio lile, bali kwanza ili wakamilishe hilo ni lazima wapate backup kubwa kutoka Marekani, UK, EU na baadhi ya nchi za NATO kama vile Canada nk. Bila nchi hizo kuwa nyuma ya Israel kimipango, silaha na fedha kiukweli Israel haiwezi kufanya chochote kwa Iran NEVER, NEVER and NEVER again. Ndiomaana mara usikie Netanyahu kaongea na Biden kwenye sim, mara usikie Biden kamwambia asishambulie vinu vya nyuklia na visima vya mafuta, mara sijui mkuu wa jeshi la Marekani kaenda Israel kukutana na mkuu wa jeshi la Israel nk. Huku kote ni katika kuhaha, kuhenya henya na kuhangaika, maana wanajua fika kwamba Israel yenyewe haiwezi kujibizana na Iran kijeshi, hivyo ni lazima wakae chini wajadili madhara yatakayotokea endapo Israel itapewa tafu na mabeberu wake kuishambulia Iran alaf Iran ijibu kwa nguvu hali itakuaje!!
Iran ikitaka kufanya shambulizi huwa haihitaji kwenda kuomba msaada au ruhusa yoyote. Wao wanatwanga tu halaf wanasubiri mpumbavu ajibu wamuoneshe.
Lengo la Iran sio kushambulia raia, bali jeshi na mifumo mingine ya serikali. Ila ikitokea Israel ikashambulia makazi ya raia wa Iran kama afanyavyo huko Lebanon na Gaza, basi bila shaka na yeye hatokuwa na njia nyingine zaidi ya kulipiza kisasi ili na wao waone uchungu waupatao wenzao. Sasa hilo ndio linalowaumiza kichwa maadui wote wanaopanga kumsaidia Israel kupambana na Iran.
Wanajua kwamba mifumo ya Israel huwa haina shabaha katika vita, ndomaana mara usikie wamekosea wakalipua mpaka ofisi za UN, mara wameuwa waandishi wa habari, mara raia nk. Sasa wakikosea na shabaha ya huko Iran wakapiga raia, kisasi chake kitakuaje. Unaweza kutumia kichwa chako kutafakari vizuri kwamba kama mifumo ya ulinzi wa anga na wa jeshi Iron dome imeshindwa kuzuia makombora kupenya, vipi nyumba za kawaida za raia zilizojengwa kiholela kama vibanda vya wamachinga pale Karume Complex. Maafa yake si yataishangaza dunia.
Hivyo basi ili kuepusha hayo yasitokee ni lazima kuangalia strategy fulan itayoisadia Israel na Marekani zifute aibu yao. Sasa wameshaona kuwa shambulizi lao linaweza kusababisha hasara zaidi kwa Israel, maana kina Netanyahu wote makazi yao yanajulikana hata wakimbilie chini ya udongo watafuatwa tu na kombora. So ili kuepusha majanga hayo kutokea ni kutafuta tukio lolote ili liunganishwe na shambulizi kwa njia ya imani au kawaida. Mfano ikitokea soko au au uwanja hata wa mpira umepata hitilafu ya umeme na kuungua moto, basi tukio hilo haraka kupitia vyombo vya habari vya magharibi litatangazwa kama ni shambulizi la kimya kimya lililofanywa na Israel katika nchi hiyo yenye nguvu kubwa katika mashariki ya kati. Hili litaenda sambamba na kauli ya Biden kwamba alikuwa ameikataza Israel kufanya mashambulizi Iran, ila yenyewe imeamua kushambulia 😂😂😂
Nafikiri kila mtu anakumbuka lile shambulio la kwanza lilivyotengenezewa tukio. Kimya kilikuwa kingi kama hivi. Siku ambayo radi ilipiga ili mvua inyeshe, wazee wa kazi wakaliunganisha lile tukio ghafla na kisasi cha Israel. So na hili shambulizi litalipwa kwa njia ya tukio au kuvizia viongozi wa hezbullah wataoenda Iran kutembea, ila Netanyahu kufanya shambulizi kama anavyofanya huko Lebanon, Syria, Yemen na Gaza hana uwezo huo.