figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Kijana mmoja aliefahamika kwa jina la Ally Chinga mkazi wa kata ya Msinjaili manispaa ya Lindi amefungiwa ndani na kupuliziwa dawa ya Mbu baada ya kupigwa na mtu aliyemtuhumu kuiba betri ya gari leo Disemba 28, 2021.
Imeelezwa kuwa, Mtuhumiwa huyo ambaye ni kondakta, alipewa gari hiyo kwenda kujaza mafuta na dereva wake Mussa Mshamu na baadae ndipo ikasemekana aliiba betri hiyo jambo ambalo mtuhumiwa huyo amelikana.
Mjumbe wa mtaa huo Bi. Rehema Omary amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, dereva huyo sio mara yake ya kwanza kufanya hivyo jambo ambalo limekuwa kero mtaani hapo huku akikemea vikali matukio ya kujichukulia sheria mkononi.
Chanzo: Mashujaa FM