Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Emmanuel Manase, Mtumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) alimtolea sime dereva wa lori akimtaka ampe leseni yake.
Tukio hilo limeonekana kuwa na ugomvi mkubwa na baadae mtumishi huyo aliamuru dereva aandikiwe faini ya Tsh. 500,000 ili kumkomoa.
Umoja wa Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) wamelaani tukio hilo kwa kuwa kama asingekuwa afisa wa polisi katika tukio lile wanasema yangetokea madhara makubwa.