Afisa wa LATRA ni mla rushwa mkubwa, hiyo gari bei yake ni mil 35 (Harrier), kwa mshahara wake sidhani kama anaweza nunua, wachunguzi waanzie kwenye akaunti yake etc. Ni bora afukuzwe kazi mara moja liwe fundisho. Pia kuna traffic wa hivyo, unakuta anaibuka tu kusema umemdharau ilihali unaonesha kumheshimu
Gari amenunua kabla hajaajiriwa latra.. hana hata miaka miwili latra.. ameshafanya kazi kampuni binafsi kubwa nyingi.. amefanya huawei kama logistics manager, bandari kavu ami amefanya, amefanya kazi za mshahara milion 4.. why asijenge au kununua magari?
Watu wanaenda serikalini kupumzika baada ta kuchoka presha za sekta binafsi..ila hela wameshavuna sana sekta binafsi.. manase miaka zaidi ya 8 amefanya private sector..
Ameshashika cheo cha logistics manager nabaki africa, huawei,Alistair.. sasa hela zote huko ashindwe kujenga au kununua magari
Tena ukiona nyumba yake kimara ndipo utasema afungwe kabisa kwa ufisadi