Lindi: Zitto Kabwe na Sulemani Bungara (Bwege) wakamatwa na Polisi

Wamwachie mara moja bila masharti yeyote.
Vikao vya ndani vya chama mnamkamata mtu?
Hivi hawa polisi wetu na wale wa wakoloni tofauti yao ni nini? Yaani inauma sana kuona jamii ikisukumwa kutafuta uhuru na kujikomboa mikononi mwa wakoloni weusi karne ya 21.
 
Libya iliyokombolewa kutoka kwa Ghadafi sahivi ipo wapi?
Bado inapitia mchakato wa kusimama .


Sasa kipi bora, kuendelea kupigana na kua huru.

Kuendelea kujitia ujinga na kua mtumwa ndani ya nchi yako??


Tatizo ni Viongozi wa Afrika, tunao viongozi wa ovyo ovyo sana .
 
Ni hasira tu mkuu maana wajinga hawaishi katika ulimwengu na ndio mtaji wa SISIEMU.
Haya mambo yakupigana kisa uchaguzi na mavyama wenzetu wakenya washavuka naona sisi ndo kama tunaelekea huko.Unampigania mwanasiasa yeye anamaliza kuhojiwa anatoka wewe ushapambana na polisi ushaumizwa na huyo unayempigania hatakupa hata mia ya matibabu! Zaidi mtu anajizidishia umasikini tu!
 
Sawa ila nakwambia ipo siku atatokea kichaa atawafanyia mbaya sana hao Policcm na ndio itakuja kuwa fundisho kuvamia mikutano hovyo hovyo!!! Sio kwamba wanampigania mwanasiasa wanareact kwasababu hao wapoliccm wanavamia wanavuruga mkutano wao,hao walioreact ni part ya uongozi wa ACT na ni moja ya kazi zao hizo wanazojadili kwenye huo mkutano ,kitendo cha policcm kuvuruga taratibu za kazi zao na kureact sio kwamba ndio wanampigania zitto na bwege,wanapigania haki yao kunajisiwa.
 
Bado inapitia mchakato wa kusimama .


Sasa kipi bora, kuendelea kupigana na kua huru.

Kuendelea kujitia ujinga na kua mtumwa ndani ya nchi yako??


Tatizo ni Viongozi wa Afrika, tunao viongozi wa ovyo ovyo sana .
Itakuwa huifahamu Libya ya sahivi wewe. Hata dalili za kuinuka hazipo.Ndo kwanza majeshi ya Egypt, Turkey, na ya nchi nyingine yametia kambi kulinda maslahi yao.Ile Libya iliyomuumiza kichwa U.S haitarudi.Uchumi graph imeshuka kwa kasi ya ajabu.Hayo ndo matokeo ya Violence. Kama upo tayari na sisi tufike huko sawa.
Ila elewa hakuna mwanasiasa atakutoa wewe kwenye lindi la umasikini!
 
Kama hawakuwa na kosa lolote basi hapo wameonewa
 
CCM wakiona hata wapinzani wakifanya kikao haja kubwa inaanza kuwagonga chu..pi
 
Huyo zitto kutwa kujipendekeza kwa mabalozi kuichafua Nchi yetu

Akamatwe akae huko ajifunze
Umenikimbusha wafuasi wa makaburu walivyokua wakishangilia waafrika wenzao wanavyo nyanyaswa hovyo huko Afrika kabla ya Uhuru lakini ata baada ya Uhuru mambo niyale yale.
 
Hao polisi wanatumwa tu mkuu, tatizo ni wanaowatuma.
 
June 21, 2020
Mkuranga, Pwani

UVCCM MKURANGA, WAMPITISHA JOSEPH POMBE MAGUFULI BILA KUPINGWA/ MHE. ULEGA "MIRADI MIKUBWA IMEKAMILIKA"


source : ikema tv
 
2015 NEC ilitangaza Pombe imeshinda na 2020 wananchi wenye nchi yetu tunamwaga Pombe.

Mwaga Pombe ya NEC chagua Raisi wa wananchi.
 
Mbona mapema sana kuanza hayo mambo? Hama kweli kuna watu wanaogopa upinzani kuliko maelezo.
 
Wazuie hata vikao vya harusi na sendoff pamoja na misafara yake. Ni kwamba hakuna uhuru wa kukusanyika lakini tunaona wengine wakifanya yao kila siku pasipo vibari wala kuzuiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…