Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Mjadala wa mungu katika mambo mbalimbali kama kuwepo au kutokuwepo kwake, kusaidia masikini kuwa matajiri, kuponya wagonjwa n.k utaendelea kwa muda mrefu sana au wakati wote dunia itakapokuwepo lakini jambo moja lenye uhakika kabisa ni kwamba kwenye siasa na masuala ya haki hakuna ushahidi wowote wa Mungu kusaidia, kuhusika au kubadilisha mambo popote duniani.
Tofauti na story za kwenye Biblia na Quran hakuna miujiza ya Mungu iliyowahi kushuhudiwa na kujadiliwa hata kwa kubishaniwa kwamba aliwasaidia watu fulani dhidi ya mfumo fulani wa siasa kandamizi, ukoloni, unyonyaji au kuweza kupata haki zao dhidi ya madhalimu, madikteta na wakandamizaji.
Zaidi sana kote duniani watu wanaofanya haya mabaya na maovu katika tawala karibia zote kasoro zile za Kikomunist nao huwa wanasema ni watu wa mungu na wamewekwa na mungu kufanya hayo au kutawala hivyo.