Lini ilikuwa mara ya mwisho Mshahara wako ulikutana na unaofuata?

Lini ilikuwa mara ya mwisho Mshahara wako ulikutana na unaofuata?

Mimi unaishaga Week ya kwanza, Pesa yote Inaenda sehemu flani hivi.
Baada ya hapo naishi kwa kutatua matatizo..

Yaani, nakunywa chai pesa yote napata nguvu.
Hivyo nakosa ya mchana, naaza kutatua tatizo la pesa ya chakula mchana,

Likiisha hilo linakuja la jioni...
Lazima kichwa kiwake mda wote nipo resi..
 
Kuna swali najiuliza hivi kadiri unavyoata fedha ndivyo majukumu yanaongezeka au ni akili tu inajiambia sasa hivi kipato kimeongezekana nawe ongeza matumizi?

Nasema hivyo kwa kuwa mara nyingi imetokea kwa watu wengi hasa sisi wa hali ya kawaida na hali ya chini imekuwa kawaida mishahara kutokutana, yaani ule wa mwezi huu uwepo angalau kidogo pindi wa mwezi unaofuatia unapoingia.

Je, lini mara ya mwisho wewe mishahara yako imekutana?
Binafsi nina rough expenditure tu ila wangu nikitaka kusev kila mwezi naeza sev 1mil
 
Back
Top Bottom