YA NINI SASA? NI UPUUZI. NI KUSOMA AU KUKARIRI? MI SIJAONA WAKISOMA. NIMEONA WAKIKARIRI.
Kukariri/kuhifadhi ni njia ya kwanza muhimu sana ktk kujifunza kitu chochote duniani, ingawa pekee haijitoshelezi ktk mchakato wa kujifunza. Kuna vitu kama mantiki(logic) kudadisi(curiosity) kulinganisha/kuhusianisha
na ndio maana mara nyingi kama sio mara zote utaona haya mashindano yanahusisha watoto . Na ndio maana watoto wengi wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi wakipata access wanakuja kuwa wasomi wazuri ukubwani
Tatizo la biblia kutohifadhika;
1. Biblia ni kubwa takriban mara 5 ya Quran ukihesabu mistari utaona Biblia Ina mistari takriban 30,000 wakati Quran Ina mistari takriban 6,000 Ingawa kiimani ni jambo lisiloshindikana
2, Biblia haina sole/single universal text ambayo wakristo wote duniani wa madhehebu yote wanaweza wakakutana kuitumia word to word kama ilivyo Quran kwa waislamu
3. Meaningful Poetry
Ukiangalia Quran yote kwa ukaribu utaona mtiririko wa maneno yenye vina na mizani ambao haujapoteza maana iliyokusudiwa. Ni kitu kigumu sana kwa wandashi kubalansi matakwa ya kishairi bila kupoteza kusudio la unachotaka kukisistiza, kwenye Quran hicho kimewezekana. Kwa ushairi uliyopo kwenye Quran umeifanya iweze kuhifadhika ki urahisi ingawa Biblia nayo Ina baadhi ya sura (Hesabu/Psalms)ambazo zina vionjo vya mashairi ila sidhani kama Inafika hata robo ya Biblia
4. Lugha ya kutatamausha ( isiyo muruwa) kwa kadamnasi
Biblia imesheheni mistari yenye kuogofya kusomwa mbele ya watu wengi hususan watoto wadogo
Kwa mfano pale Daud anapohitaji mahari ya magovi na mistari mwingine kama hiyo
5. Uislam kwa nguvu zote unasistiza usomaji na uhifadhi wa Quran wakati wakristo hawana muamko huo au wako NEUTRAL ktk kuhifadhi
6. Frequency & Consistency
Kama kwa uchache unasoma au unasikiliza somo moja Kila siku mara 5 Hivyo ndivyo kwa Waislamu maana wao huswali mara tano kwa siku na Kila wanaposali lazima wasome Quran
Hapo huyo kijana bado hajatenga muda wa kuhifadhi Quran