Kwani kuliendaje? Uchaguzi wa 2013, tume mpya na huru ya uchaguzi, IEBC, ilifanya kazi nzuri na uchaguzi uliisha bila malumbano. 2017 wapinzani wakapinga matokeo, wakawasilisha kesi yao mahakamani, uchaguzi wa urais ukabatilishwa. Ukarudiwa tena, upinzani wakapinga matokeo tena, mgombea wa upinzani akajiapisha. Baadaye wakafanya handshake na rais na sasa hivi bado yupo Kenya, bila tundu hata moja la risasi, wakiketi pamoja kupanga na kujadili masuala ya taifa la Kenya. Sasa tuna nini cha kujifunza kutoka kwenu, wakati bunge lenu sasa hivi ni la chama kimoja? Huku aliyekuwa mgombea wenu wa urais kutoka chama cha upinzani akiwa ukimbizini kule Ubelgiji?