Lipi bora kati ya kununua nyumba iliyojengwa au kujenga yako mwenyewe?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Je, ipi ni sahihi ukiwa na hela yako kama Tsh. Milioni 40, ununue nyumba mbalimbali zinazotangazwa mitandaoni na magazetini au kwa hiyo hiyo Tsh. Milioni 40 uliyonayo umtafute fundi na akujengee nyumba yako katika uwanja ambao tayari unao siku nyingi?

Leo GENTAMYCINE nitakuwa ni msomaji zaidi wa comments zenu hapa ili basi siku moja huko mbeleni kama Mwenyezi Mungu atanibariki na kimaajabu nikaipata hii pesa (Tsh. Milioni 40) niweze kuwa na nyumba kutokana na ushauri wenu na maelekezo yenu ya kitaalam ambayo mtayatoa hapa.
 
Kuna mtu alinunua nyumba kwa tsh mil100+ kwa nje imepigwa rangi imefanyiwa pimping moja matata kumbe ilijengwa kwa matofali ya udongo ambapo kiuhalisia ile nyumba thamani yake ilikuwa haifiki hata mil30.
Madalali kwa kweli mbingu hawataiona!
 
Bora ujenge mwenyewe, kwa kahela Kako hako hako inatoka vizuri kabisa. Lakini ukinunua pahali, unaweza kukutana na matatizo lukuki Yani, kama si majini, mauza uza ya hivyo usiku au asubuhi basi utakuta matofali aliyotumia ni hovyo kabisa. Nyumba nzuri ni Ile ambayo umetayarisha kiwanja chako mwenyewe na umejipangia muundo wa nyumba uutakao.
 
Asante kwa Ushauri wako wa Kitaalam Mkuu. Nina Kajiswali kadogo tena hapa hivi kwa Kiasi hicho hicho cha Pesa ipi bora Kununua Nyumba iliyoko maeneo ya Mjini na Kulikochangamka au uende Ukajenge zako mbali huko mfano wa Vikindu au Mapinga ambako kuja Mjini ni lazima uwe na Tsh 10,000?
Nasimamia pale pale kua ni bora kujenga haijarishi ni maeneo gani(sababu maendeleo yatakuja tu no matter what),nyumba za kununua zinamengi mabaya, ya kiroho(mshana jr aje kusema chochote),hata watu wabaya wanaweza kukusumbua pia maana pengine wanaijua vizuri ramani ya nyumba ulio nunua.naomba niishie hapa
 
Mikocheni mpaka masaki watu wana nunua mijengo leo kesho!

Bado kariakoo watu wana nunua wana shusha maghorofa

Kama una pesa mwenge hapa kuna fremu tuna taka kuziua tushushe ghorofa, njoo uwe mbia
 
Je, ipi ni sahihi ukiwa na hela yako kama Tsh. Milioni 40, ununue nyumba mbalimbali zinazotangazwa mitandaoni na magazetini au kwa hiyo hiyo Tsh. Milioni 40 uliyonayo umtafute fundi na akujengee nyumba yako katika uwanja ambao tayari unao siku nyingi?

Leo GENTAMYCINE nitakuwa ni msomaji zaidi wa comments zenu hapa ili basi siku moja huko mbeleni kama Mwenyezi Mungu atanibariki na kimaajabu nikaipata hii pesa (Tsh. Milioni 40) niweze kuwa na nyumba kutokana na ushauri wenu na maelekezo yenu ya kitaalam ambayo mtayatoa hapa.
Jenga mpya usinunue

Kuna nyumba zimejengwa na katika ardhi husika Kuna maagano ya kiroho yaliyofanyika kupitia mmiliki wa awali wa nyumba yanaweza kukutesa na kuisambaratisha familia
 
Jenga Mkuu usije ukayakanyaga ya "JENGA UZA".

Ukijenga yako utazingatia ubora ,ukinunua tayari unaweza ukavagaa mkenge wa JENGA UZA ,Jenga uza matofali yao biscuit ,ila decoration yao ya kufa mtu ila NYUMBA ni MABUA ,mvua mbili tu inaenda na MMA.
 
Je, ipi ni sahihi ukiwa na hela yako kama Tsh. Milioni 40, ununue nyumba mbalimbali zinazotangazwa mitandaoni na magazetini au kwa hiyo hiyo Tsh. Milioni 40 uliyonayo umtafute fundi na akujengee nyumba yako katika uwanja ambao tayari unao siku nyingi?

Leo GENTAMYCINE nitakuwa ni msomaji zaidi wa comments zenu hapa ili basi siku moja huko mbeleni kama Mwenyezi Mungu atanibariki na kimaajabu nikaipata hii pesa (Tsh. Milioni 40) niweze kuwa na nyumba kutokana na ushauri wenu na maelekezo yenu ya kitaalam ambayo mtayatoa hapa.
kula bata.. kula bata.. duniani tunapita
 
yani bongo kuendelea bado sana, eti ardhi ina mizimu na maagano dah🤣
ukiipenda ya kununua nunua na ukitaka kujenga jenga tu
 
Back
Top Bottom