Je, ipi ni sahihi ukiwa na hela yako kama Tsh. Milioni 40, ununue nyumba mbalimbali zinazotangazwa mitandaoni na magazetini au kwa hiyo hiyo Tsh. Milioni 40 uliyonayo umtafute fundi na akujengee nyumba yako katika uwanja ambao tayari unao siku nyingi?
Leo GENTAMYCINE nitakuwa ni msomaji zaidi wa comments zenu hapa ili basi siku moja huko mbeleni kama Mwenyezi Mungu atanibariki na kimaajabu nikaipata hii pesa (Tsh. Milioni 40) niweze kuwa na nyumba kutokana na ushauri wenu na maelekezo yenu ya kitaalam ambayo mtayatoa hapa.
Hili swali lako majibu yake sio rahisi au sio majibu ya direct kwamba kujenga ni Bora kuliko kununua au kinyume chake.
Mfano Kuna nyumba zimejengwa na kampuni au taasisi au mtu binafsi na zinauzwa , pengine zipo kwenye maeneo unayoyapenda na zimesimamiwa under professional consults like civili engineers nk(zimejengwa kweny standard). Hapo nitakushauri ununue kwa sababu gharama za ujenzi kwa hiyo standard ni gharama na pia Kama sio mzoefu kweny secta ya ujenzi itakusaidia.
Pia ukitaka kununua nyumba ulizia ramani yake, consultant aliesimamia nyumba, Kama unanunua nyumba kwa mtu binafsi pata mda wa kufanya tafiti kwa majirani, relax husiwe na haraka kufanya maamuzi. Kwa nini ufanye maamuzi ndani ya masaa mawili kwenye nyumba ambayo utaishi zaidi ya miaka 50? So take time , husipelekeshwe na madalari.
Kwa upande mwingne, Kama una fundi mzuri/ una uwezo wa kutumia kampuni , umepata mtalamu wa ramani na una mda wa kutosha kufanya follow up au una mtu unaemuamini wa kusimamia ujenzi basi Jenga.
Kwa kuhitimisha.
kwenyw swala la kiuchumi/economical factor.
_kununua ni Bora kuliko kujenga, here time also has been considered.
Kwenye ufahari wa kumiliki/ ownership factor.
_kujenga ni Bora kuliko kununua, maana utakuwa na authority ya kumodel nyumba utakavyo.