The useful idiot
JF-Expert Member
- Jul 14, 2024
- 1,019
- 2,670
Kama sio bikra usioe!Habarini za JIONI wakuu?
Mimi ni kijana wa miaka 32 mnamo mwaka 2019 nilibahatika kupata mwanamke kutoka Kanda ya ziwa{Tabora}..,nilimpenda sana na nahisi nae alinipenda japo siwezi semea nafsi ya mtu.
Ilipofika 2020 alihitaji sana kukaa NAMI nyumba moja kama mume na mke..,kweli KUTOKANA na Mimi nilikuwa nimepanga sehemu na kwa bahat mbaya sehemu niloyopanga kulikuwa na shida na baba Mwenye nyumba kuwa na visilani basi aliniomba nitoe vitu nihamie anapokaa yeye japo n kwenye nyumba ya kupanga pia.
Kweli nilimkubalia kwa upendo ila nikawa nawaza nawezaje kuingia kwenye nyumba ambayo sijui ni nani analipa Kodi?n.k nikaamuomba nikapange mitaa ambayo s mbali na anapokaa ili tu nizidi kujifunza na kujua mambo yake japo kipindi ambacho sijahamia makazi mapya tulikuwa tunakutana lodge.
Kwenye kuzidi kujuana nilikuwa namuuliza kama ana mtoto au laah,alinijibu kweli ana mtoto wa miaka mi 4 kasoro na anakaa nae japo alisem wameachana na mzazi mwenzie..,nikasema hakuna shida kama mtoto unae tutapambana MAISHA yataenda tu..,muda huo mm sina mtoto nae hata mmoja na muda huo mm sina mtoto kabisa.
Basi nilikaa pale nilipopanga nilikuwa naenda kule kwakwe kupata chakula Cha usiku nikitoka mishe zangu then nakuja kulala nilipopanga japo muda mwingine alikuwa anakuja niliponga MAISHA yanaenda,ikiwa weekend naenda nashinda pale kwakwe na mwanangu wa kufikia tunafurah mambo yanaenda..,tuliishi hayo MAISHA kwa miezi kadhaa hivi tukifurahia MAISHA.
Sasa basi katika hayo maisha tuliyokuwa tunaishi mwenzangu akapata ujauzito tukiwa kwenye MAISHA yale ya kulea ujauzito na mambo mengine Kuna mambo nikawa siyaelew especially kwenye mambo ya mawasiliano yake na mtu ambaye anasema n kaka yake wa hiyali maana nikimuuliza anasema HUYU n kaka hata kijijin kwetu walipo ndugu zangu wanamjua kwa Hiyo usiogope maana hata nilipofika hapa mjini yeye alinipokea na nilipatwaga na matatzo yeye ndo mtu wa kwanza kuniwahisha hospital kabla hata ya ndugu zangu kufika...,mm nikasema sawa hakuna shida.
Kweli tulienda na hayo MAISHA tulibahatika kupata mtoto wa kiume na kwa bahat nzuri kafanana na Mimi mpaka watu wanashangaa,baada ya kumpata huyo mwanangu wa kwanza kwangu na mtoto wa pili kwakwe tulifurah wazee walipata taarifa na ndugu kiujumla..,nilipatwa Hadi nguvu ya kumsimamia mwanangu wa kufikia nilianzisha SHULE ya nasali na kila kitu kinachohusu yule mtoto wa kufikia nilisimamia kuanzia,mavaz,maladhi,SHULE n.k
Sasa basi KUTOKANA na filosofi ya MAISHA yangu huwa Nina Mila yangu ya kutokunfuatilia mke wangu kuhusu simu yake yangu., tumeanze mahsiano ni miaka mi 5 kasoro Hadi sasa nilikuwa sijawahi shika simu yake kusema kuanza kumfuatilia HUYU nani?kwann anapiga simu?au kusoma sms yake nilifanya hvyo ili awe huru na MAISHA yake..,japo yangu alikuwa anaipekua na kwasababu Mimi ni mtaalamu wa program hizi za simu nikawa najua mtu akishika simu yangu...,sikutaka kumsema kwasababu najua kila mtu ana moyo wake.
KUTOKANA na yule mtu ambaye anasema n kaka yake kuzidi kuwasiliana na mawasiliano yakawa mengi sana nikapatwa na shaka nilikuwa namuuliza huyo n nani akajibu vile vile yule ni kaka..,na Kuna wengineo pia wawili yeye akasema n kaka zake mmoja yupo nzega na mwingine yupo kijijini kwao hapa mkoani tulipo.
Nikamjibu sawa...,KUTOKANA na majibu yake ambayo hayakuwa na uzito Wala umaana kwangu nkasema ntalichunguza hili kwa MIFUMO yangu nayoijua Mimi.
Japo najua n kosa kumfuatilia mtu mawasiliano yake lakini nilifanya hvyo..,nilimhack nilichokuja kukiona n kwamba wale sio kaka zake Tena wanadiliki kumuita mke nae anajibu mume,huku akawa mpaka ananunuliwa nguo analeta ndani s kwamba Hana nguo hapana,mbaya zaidi anaomba pesa kwa mahawala ovyo labda kama Mimi simpatii,pili anamambo ya chini chini sana yenye usili ndani yake...,nilimfuata nikamuuliza swali au maswali kama yale yale alijibu kuwa wale n kaka zake akiwa hajui sasa kama
Mimi najua ukweli wote...,nilimuonyesha ukweli akastua na kuanza kutafuta makosa yangu ili wote tuonekane sio..,nikasema hapana HUYU ni mtoto wa watu nisije nikapatwa na hasira nikaja mfanya vibaya nikampeleka kwenye kikao kwa ndugu zake ili wamuhoji kwann anafanya vile?akawa Hana la kujibu akawa anasema mbona nam Nina makosa,basi wazee wakasuluhuhisha tukaombana msamaha na kuahidi kwa mungu kwamba hatorudia na akirudia nifanyie kitu chochote.
Basi tulirud nyumbani MAISHA yakaendelea,tumeshinda siku ya kwanza,ya pili na ya 3,siku ya nne nilitoka kazini kama mida ya saa 12 JIONI nilipofika tu akaniambia baba flani Kuna net mbili nimenunua nakuomba nenda kzibadili,nikasema sawa
Nikachukua neti moja nikaenda kuanza kubadili chumbani kwa watoto,sasa wakat nabadili nikakiona kisimu kidogo kipo dirishani wakat naendelea kutoa net akanyanyuka ALIPOKUWA anapika akakifuata kile kisimu akatoka nacho nje...,
sasa basi mungu nae alivyo wa ajabu Kuna sehemu Kuna kamba ilikuwa imefungwa sehemu ambayo Ina kiza nikaamuomba kile kisimu nimulikie pale,nkachukua nikamulika nkamaliza sasa wakat nahangaika kutafuta mahal pa kuzimia tochi s nikabofya kwenye sms nikakuta wale wale watu ambao tulisuruhisha kwa ndugu zake ndiyo anachat nao aisee nilipatwa na mshituko sana na kujiuliza HUYU mtu au Jini?
Embu naomba mnishauli jambo..
Nimfanyaje HUYU mtu au nifanyie Nini?
Maamuzi yangu nilihtaji nibebe nguo zangu tu nisepe nikakae kwingine,watu wazima wanasema nibaki nisifanye lolote kwakwe kwa ajili ya watoto...,lakini najihisi kama ntazidi kumchukia jaman.
Singo maza ni pigo la roho