Elections 2010 Lipumba atangaza kugombea urais 2010

Elections 2010 Lipumba atangaza kugombea urais 2010

Nadhani tuliyemchoka ni JK, utamchokaje mtu wakati hata hajaanza?
 
CUF bado haijapitisha mgombea wao, Prof. Lipumba anahaki kugombea, na huenda akashindwa katika kura za ndani au akabadili mawazo baadae. Hata hivyo hakuna kitu cha kumshushia haki ya kugombea. Lipumba ni bora x1,000,000 ya Kikwete.

Mkuu hapo kwenye red sijui
1 - wote ni wachumi
2 - jk hajui anything about economics development zaidi ya kusafiri hovyo
3 - Lipumba - kwake uchumi wa nchi ni kuchapisha noti kama alivyomshauri mzee mwinyi na si kutengeneza mifumo ya kukusanya kodi km mkapa alivyofanya.

Sasa sijui ubora wa jk na wa lipumba uko wapi. Mimi nadhani wote hawafai, the only thing they fit ni PUBLIC RELATIONS-JK awe msemaji wa serikali ya Rais mwingine wa TZ na lipumba msemaji wa CUF.

Chini ya uongozi wake CUF imeweza kuwa na kiti cha ubunge kimoja tu TZ bara-Bukoba. He is useless.
 
Jamani inakera ndio maana naona huu upinzani wizi mtupu na thaman kwako ukiwa ndani ya hicho chama ..naona lipumba kwenye tv ya tbc anawahadaa watu kuna rais alianza kugombea toka 1975 amepata urais 2000 na sasa anaongoza na kuhaidi kuleta serikal ya mseto........
Hivi hakuna wengine kila siku hawa hawa tu jamani...mi nishachoka na sias za tanzania kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Kila anapoulizwa swali kuhusu yeye kugombea kila chaguzi,anatoa mfano wa huyohuyo jamaa yake aliyegombea tangu mwaka 1975,ananiboa!
 
Kila anapoulizwa swali kuhusu yeye kugombea kila chaguzi,anatoa mfano wa huyohuyo jamaa yake aliyegombea tangu mwaka 1975,ananiboa!

And huu is this another plastic aliyegombea tangu 1975?
 
Hakuna wa kuchagua.....Yaani sijui itakuaje next five yrs...so far bado kuna wakina mama wanajifungua chini ya miti,,,,,,life linazidi kuwa gumu...so...MUNGU ATULINDE
 
Hakuna wa kuchagua.....Yaani sijui itakuaje next five yrs...so far bado kuna wakina mama wanajifungua chini ya miti,,,,,,life linazidi kuwa gumu...so...MUNGU ATULINDE

Get Rich or Die Tryn......
 
Lipumba%2816%29.jpg

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba



Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema ataviandikia vyama vingine vya upinzani barua rasmi, kuviomba visisimamishe wagombea urais, badala yake vimuunge mkono yeye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Profesa Lipumba alisema hayo wakati akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF, kwa kumpitisha kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho katika uchaguzi huo Alisema anakusudia kuwasilisha maombi hayo kwa vile haoni kama kuna mtu katika vyama hivyo mwenye uwezo wa kukabiliana na mgombea wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, kulingana na hali ya kisiasa ilivyo nchini.
Profesa Lipumba aligombea urais katika uchaguzi wa mwaka 1995, 2000 na 2005 na kushindwa huku baadhi ya watu wakivitaka vyama vya siasa kusimamisha mgombea mmoja, lakini viongozi wa upinzani mara zote kushindwa kukubaliana.
Profesa Lipumba ambaye alipitishwa kwa kupata asilimia 99.7 ya kura zote zilizopigwa, alisema iwapo chama chake kitafanikiwa kushinda katika uchaguzi huo, miongoni mwa mambo makuu yatakayotekelezwa, ni pamoja na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Jana CUF walitangaza kwamba Lipumba alikuwa amepata ushindi wa asilimia 98.97, lakini baadaye usiku wakasema kulikuwa na makosa katika ukokotoaji hivyo kubainika kwamba alikuwa amepata asilimia 99.7.
Kadhalika, chama hicho kilisema kuwa ukokotoaji wa ushindi wa Maalim Seif nao ulikuwa umekosewa kuwa asilimia 96.38 badala ya asilimia 98.88.
Alisema pia, ataboresha elimu kufikia viwango vya kimataifa na atahakikisha mafisadi wote wanashughulikiwa ipasavyo.
“Naamini kwa uwezo nilionao, ninaweza kutatua matatizo ya nchi hii, na nina hakika ya kupata tuzo ya utawala bora,” alisema Profesa Lipumba na kushangiliwa na karibu ukumbi mzima wa mkutano huo.



CHANZO: NIPASHE

Mimi binafsi yangu Nakubaliana na wewe waweza kushindana na CCM. Je Mnasemaje Wakuu wenzangu wa J.F?
 
Jamaa ili linaweza ila shida yangu ni kuwa kwenye mikutano ya siasa ya CUF baraghashea na ijabu ni nyingi sana!!!
 
Kweli anaweza kushindana na siyo kushinda sisi tunataka mshindi. Hii itakuwa ni mara ya ngapi vile?
 
Mie binafsi baada ya mgombea binafsi hoja kupigwa chini nafikiria sana huyu jamaa anaweza kufaa
 
Tatizo CUF ni wabinafsi wanataka wao ndiyo waungwe mkono siku zote, wao hawako tayari kuunga mkono vyama vingine. Hii inatia shaka kuwa huenda wana agenda ya siri, pia Profesa amegombea mara nyingi na kushindwa, ni vema CUF wangesimamisha mgombea mwaingine. All in all kama hakuna mgombea mwingine toka opposition, nitampa kura yangu kwa vile naichukia CCM na viongozi wao kama ninavyomchukia shetani.
 
Tatizo ni chama chake? we need a liberal party na si chama chenye mwonekano wa kidini kama CUF. Mikutano yao ni kama forum ya walimu na wanafunzi wa madrassa. Na ndiyo sababu ccm inashinda maana watu wanaona ni bora jini ulijualo kuliko usilolijua.

Hakuna kiongozi yeyote wa upinzani anayeweza kukubali kuiunga mkono CUF kwa sababu ya mwonekano wa Udini ilionao.
 
hakuna njia ya haki ambayo wananchi wanaweza kuhusishwa kumchagua mgombea wanae mtaka kutoka upinzani kuliko Lipumba kujipigia pande mwenyewe kwamba yeye ndio anafaa?
 
UDINI! UDINI! UDINI! Chama chake kimejaa udini na hii nchi haina dini, we unazani itakuaje? aendelee kupiga makelele jukwaani na kuikosoa serikali ili siku ziende lakini si yeye wala chama chake cha kuitawala nchi. afu mi nashangaa kama vile hawaoni wajirekebishe..
 
Jamaa ili linaweza ila shida yangu ni kuwa kwenye mikutano ya siasa ya CUF baraghashea na ijabu ni nyingi sana!!!

Inasemekana hao wanaovaa hivyo wakati wa mikutano yao ni mapandikizi ya CCM katika kwa lengo la kukipaka chama hicho label ya udini.
 
Tatizo CUF ni wabinafsi wanataka wao ndiyo waungwe mkono siku zote, wao hawako tayari kuunga mkono vyama vingine. Hii inatia shaka kuwa huenda wana agenda ya siri, pia Profesa amegombea mara nyingi na kushindwa, ni vema CUF wangesimamisha mgombea mwaingine. All in all kama hakuna mgombea mwingine toka opposition, nitampa kura yangu kwa vile naichukia CCM na viongozi wao kama ninavyomchukia shetani.

Sallu wewe ndio umeonge pointi wengine naona mipumba tu imewajaa unasema CUF wadini unaweza kuprove how CUF ni wadini? Au kwavile baadhi yao ni waislamu? Je tupatie definition ya udini? Vile vile waislamu wakisema Chadema ni wakristo je?? tutafika? Binafsi nadhani sasa hivi tuamke na tuwe moyo wa umapinduzi pasina kujali huyu nani au nani? Binafsi namuona Professa ni competent zaidi kuliko JK. Ingelikuwa wameruhusu mgombea binafsi nilikuwa na hamu jamaa mmoja agombee kama mgombea binafsi kwakuwa nilisikia tetesi atagombea but kama ujuavyo imepigwa nyundo back to the parliament ambapo wataiahirisha mpaka baada ya uchaguzi.

Sasa labda tujadili kiutendaji baina ya Lipumba na JK nani zaidi? Nadhani utakuwa mjadala wenye manufaa kuliko kukaa kusema hoja za kijinga eti udini!!!
 
Eh! Kwani chadema ni chama cha kikristo...? Nilikuwa sijui hayo.
 
Back
Top Bottom