Nchi Tanzania imeshapasuka,imegawanywa katika misingi ya DINI,Mbaya zaidi hakuna ana/aliyeweza ku address hii ISSUE kwa uzuri wake na kuweka bayana namna ya kupata ya suluhu kabla halijakuchwa na kuingia kiza kinene.
Obama aliweza ku address issue ya ubaguzi wa rangi akaeleweka pamoja na kwamba alieleza ukweli unaouma kwa baadhi ya watu,lakini walikubali uhalisia na kusonga mbele,na ndio utaona sasa hivi racial melting point in US imekuwa high,ingawa still kuna vijimambo vya hapa na pale but the issue was well addressed.
Akiwa Rais Muislam kama ilivyo sasa hivi,waislam wanapunguza kelele dhidi ya CCM na kuona si tatizo sana. Kinyume chake,wakristo wanapiga kelele na kufanya mikakati kadha wa kadha ili kulinda kile kinachoonekana ni maslahi yao.
Akiwa Rais ni Mkristo,the same applies,kelele zinapungua kabisa,na inakuwa ni zamu ya Waislam kulalamikia serikali na CCM kwamba ina sura ya ubaguzi na kutafuta mikakati ya kutetea kile wanachodai ni haki zao.
Kumekuwa hakuna kuaminiana kabisa kutokana na kutofautiana katika itikadi ya dini,na hii hali inaelekea kubaya,kama hatua madhubuti ambazo zina balance pande zote hazitachukuliwa,basi kuna dark future.
Tupo tayari kutothamini potential figures kwa sababu ya dini zetu,tupo tayari kutetea maovu kwa sababu dini yetu inapata maslahi nayo.