Mtu umeoa bado unakaa kwenye nyumba ya baba yako, baba yako ndiye anayekununulia chakula, nakukupa posho, anakununulia wewe, mkeo na watoto wako nguo, anawasomesha watoto wako, anakulipia umeme na maji na akiugua yeyote katika familia yako, yeye ndiye anayelipa. Wewe na mkeo hamfanyi kazi bali mnajisifia kuwa mzee wenu tajiri. Hivi siku baba akikuambia kuwa uache kulewa ovyo, usiwachape bila sababu watoto wako na usimpige mkeo utatanua kifua na kumwambia kuwa asikuiingilie katika himaya yako? Himaya gani hiyo!
Sisi tunapitisha kibakuli hata kuomba vyandarua, madawati, kuchimbiwa vyoo na visima n.k. Sisi tunapigiwa muziki ili hao mnaowaita wakoloni watusamehe madeni ambayo kweli tulikopa na tumeshindwa kurudisha ( ati.. we will pay them!)! Leo, miaka 50 baada ya uhuru, sehemu kubwa ya bajeti yetu wanaibeba hao tunaowaita wakoloni! Sasa hizo responsibility mnazojivunia ziko wapi? Mtu ambae ni responsible hata siku moja hataki kuwa tegemezi maana anajua athari zake. Utasemaje unapoenda kuomba misaada ( na sio mikopo) ati si kwa sababu mnataka kuwa watumwa! Mngejua hivyo basi mngehakikisha mnajitegemea na mnaweka mazingira ambayo wenyewe watawabembeleza kuwekeza. Hapo watawaheshimu. Hakuna mtu anayemheshimu mtembeza kibakuli! Tukubali makosa yetu na tujifunze kutokana nao. Tusipofanya hivyo tutabaki watu wakuonewa huruma na kudharauliwa.
Amandla.....