Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

Habari zenu

Leo nimeona ni vyema wana jikoni na wazazi tujadili na tubadilishane mawazo kuhusu lishe za watoto wetu kuanzia umri wa miezi 6 hadi mwaka.....

Nini madhumuni hasa

1)kwa wale watoto ambao hawapendi kula au hatujatambua bado nini wanapenda lakini kuna mzazi yeyote ameona chakula flani kime work kwake basi tu share nasi kujaribu kama kitapendwa pia....

2)tujuzane trick gani unatumia wakati wa kumlisha mtoto binafsi mimi huwa namfunga kwenye kiti chake alafu nampa kijiko au kipaja cha kuku sasa wakati anafungua mdomo kutafuna alichokikamata mie namuwahi kupitisha kijiko cha chakula hii inasaidia sana na tricks nyengine tutazidi kujuzana...

Karibuni wote tujadili au tupia recipe zako.

===============================

Lishe (1) - UJI WA OATS NA NDIZI/APPLE

Mahitaji

Oats kiasi

Apple 1 au ndizi ya kuwiva...

Maziwa...

Sukari (sio lazima)...

Namna ya kutaarisha

Chemsha maji

Weka oats acha zichemke hadi kuwiva

Ponda ponda ndizi vizuri weka maziwa kidogo ipondeke vizuri....

Mimina kwenye oats alafu weka na maziwa acha ichemke kidogo kwa dakika 3

Epua mlishe mtoto.....

Lishe (3) - WALI WA YAI

Mahitaji

Yai 1....tumia kiini tu

Siagi kidogo

Mchele....

Namna ya kutaarisha...

Pika wali kama wa kawaida ila weka maji mengi uwe laini bwabwa wengine wanaita bondo

Ukikaribia kuwiva weka yai ulolivunja koroga haraka haraka uchanganyike vizuri

Weka siagi na chumvi kidogo ukipenda....

Epua mlishe mtoto....

Lishe (3) - KAROTI NA KUKU

Mahitaji

Karoti

Kuku kiasi

Namna ya kutaarisha

Chemsha kuku hadi kuwiva iwe na supu kidogo

Weka karoti na subiria kuwiva...

Toa kuku pembeni alafu mchambue mifupa tupa

Weka katika blenda kuku na katoti na supu yako saga

Tayari kwa kumlisha mtoto

Ukipendeza waweza weka na viazi

Endelea kufuatilia mjadala kwa ushauri na lishe zaidi....

leo nitakesha kwenye hii sred.
 
Attachments

  • 20141213_211723.jpg
    20141213_211723.jpg
    271.2 KB · Views: 405
Habari zenu

Leo nimeona ni vyema wana jikoni na wazazi tujadili na tubadilishane mawazo kuhusu lishe za watoto wetu kuanzia umri wa miezi 6 hadi mwaka.....

Nini madhumuni hasa

1)kwa wale watoto ambao hawapendi kula au hatujatambua bado nini wanapenda lakini kuna mzazi yeyote ameona chakula flani kime work kwake basi tu share nasi kujaribu kama kitapendwa pia....

2)tujuzane trick gani unatumia wakati wa kumlisha mtoto binafsi mimi huwa namfunga kwenye kiti chake alafu nampa kijiko au kipaja cha kuku sasa wakati anafungua mdomo kutafuna alichokikamata mie namuwahi kupitisha kijiko cha chakula hii inasaidia sana na tricks nyengine tutazidi kujuzana...

Karibuni wote tujadili au tupia recipe zako.

===============================

Lishe (1) - UJI WA OATS NA NDIZI/APPLE

Mahitaji

Oats kiasi

Apple 1 au ndizi ya kuwiva...

Maziwa...

Sukari (sio lazima)...

Namna ya kutaarisha

Chemsha maji

Weka oats acha zichemke hadi kuwiva

Ponda ponda ndizi vizuri weka maziwa kidogo ipondeke vizuri....

Mimina kwenye oats alafu weka na maziwa acha ichemke kidogo kwa dakika 3

Epua mlishe mtoto.....

Lishe (3) - WALI WA YAI

Mahitaji

Yai 1....tumia kiini tu

Siagi kidogo

Mchele....

Namna ya kutaarisha...

Pika wali kama wa kawaida ila weka maji mengi uwe laini bwabwa wengine wanaita bondo

Ukikaribia kuwiva weka yai ulolivunja koroga haraka haraka uchanganyike vizuri

Weka siagi na chumvi kidogo ukipenda....

Epua mlishe mtoto....

Lishe (3) - KAROTI NA KUKU

Mahitaji

Karoti

Kuku kiasi

Namna ya kutaarisha

Chemsha kuku hadi kuwiva iwe na supu kidogo

Weka karoti na subiria kuwiva...

Toa kuku pembeni alafu mchambue mifupa tupa

Weka katika blenda kuku na katoti na supu yako saga

Tayari kwa kumlisha mtoto
R
Ukipendeza waweza weka a in viazi

Endelea mjadala kwa ushauri na lishe zaidi....
H
Reduced
 
Ngoja na mie nichangie kidogo maana mie dume, kuna mtoto wa dada yangu ametimiza mwaka mmoja sasa lakini kwa upande wa kumnywesha mtoto mfano uji anakuwa mgumu sana mtoto kunywa uji (anakataa).
Tumekuwa tukijiuliza hili tatizo linasabishwa na nini mpaka anakataa kunywa uji, ila kama ni maziwa ya mama yake anatumia kama kawaida.
Tujuzane jamani ili nimsaidie.
 
Watoto kukataa kula jamani kuna mtoto wa cousin yangu ana miezi 8 yeye hapendi kula nikagundua mama ake anampa chakula cha nyanya na maungo chakula hicho kina mkinai

Nimemwanzishia chakula chake tatizo ulitaka ale mpigie mluzi akicheka unamwekea kijiko

Uji wa karanga

Chambua karanga zako safisha
Zisage ziwe laini kabisa

Jinsi ya kutayarisha uji

Korogo unga wa karanga kwenye maji tia jikoni koroga mpaka ushike(uwe mzito) acha uchemke uive mpaka uone kama unaganda.

Utakuwa tayari kwa kunywa tia sukari kidogo ni uji mzuri kwa mtoto
Unachanganya karanga na nini au zenyewe?
 
Ngoja na mie nichangie kidogo maana mie dume, kuna mtoto wa dada yangu ametimiza mwaka mmoja sasa lakini kwa upande wa kumnywesha mtoto mfano uji anakuwa mgumu sana mtoto kunywa uji (anakataa).
Tumekuwa tukijiuliza hili tatizo linasabishwa na nini mpaka anakataa kunywa uji, ila kama ni maziwa ya mama yake anatumia kama kawaida.
Tujuzane jamani ili nimsaidie.
Kwenye huo uji anaiona sura ya WASSIRA ndiyo sababu.
 
Back
Top Bottom