Uchaguzi 2020 Lissu adai kucheleweshwa KIA makusudi na TCAA

Uchaguzi 2020 Lissu adai kucheleweshwa KIA makusudi na TCAA

mulwanaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
5,262
Reaction score
12,855
ANAANDIKA MH.TUNDU LISSU

-------

Waheshimiwa viongozi salaam. Mimi na timu yangu ya kampeni tuko Kilimanjaro International Airport tangu saa nne asubuhi. Tulikuja kuweka mafuta kwenye chopper yetu ili tuweze kwenda Dar kwa ajili ya mkutano wetu wa kufunga kampeni unaotakiwa kuanzia Kawe saa tisa mchana.

Hata hivyo tumeshindwa kuondoka KIA kwa sababu hatujapatiwa kibali cha kutua Dar na Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA).

Huu ndio umekuwa utamaduni wa TCAA katika kampeni hizi tangu tuanze kutumia chopper. Wanatumiwa na CCM ili kuhujumu kampeni zetu na ndivyo walivyofanya wiki iliyopita Lindi na Mtwara.

Sasa itatulazimu tuondoke KIA kuelekea Dar bila kibali cha TCAA; wafanye lolote wanalotaka kufanya. Mimi na wenzangu hatutakubali kunyanyaswa namna hii tena. Dar jiandaeni, tuko njiani tunakuja!
 
CCM na idara zake mwaka huu wanapata tabu sana, haiwezekani mtu asubiri kibali muda wote huo wasikitoe, huu ni mchezo mchafu unaofanywa na mamlaka ya anga Tanzania.

Wakati wa tension kama huu mambo ya kijinga kama haya hayatakiwi kuwepo, ndio yanazidisha chuki na hasira, halafu mwishowe watu wakidai haki zao wanapigwa risasi bila sababu huku mkiimba wimbo wenu wa amani...amani!.

Idara za serikali hata kama zinatumika na CCM ziache uzembe usiokuwa na sababu za msingi kuepusha maafa, msisubiri mpaka mtu alalamike ndio mchukue hatua, timizeni wajibu wenu.
 
Hatuwezi kuishi kwenye nchi ya kipuuzi namna hii. Yaaani binadamu mwenzetu anaonewa kiasi hiki tena waziwazi na wala tusichukue hatua.

Walimpiga risasi wakitaka kumuua, akapona mauti ila wakamnyima matibabu, akapona kabis wakamvua ubunge na kukataa kumlipa hata kiinua mgongo kwa kipindi alichotumikia.

Sasa amegombea uraisi hawaachi figisu, mikoa ya kusini wamemzuia kufanya mikutano zaidi ya 10, na Mkoa wa Pwani pia, kisa magufuli ameshindwa kufanya kampeni kusini.

Sasa leo anakuja kufunga kampeni Dar wanamletea figisu tena kwa makusudi. Sasa tunasema imetosha!!!!

Kesho kwa hasira tunaenda kupiga kura nyingi kwa Lissu na tutalizilinda hakika kwa gharama ya damu zetu. Hata tukifa ila historia itatukumbuka.
 
Kwanini hamkuoversee hii possibility,,?,ndo maana nasemaga hamjawa tayari kuongoza,hii ilitakiwa muione kabla na muweke plan B,C,D
Kwa akili yako unadhani plan B ni ipi? Kama kutumia gari unajua umbali wa Dar-Moshi wewe?

Tatizo ccm mmejazana vilaza sana na Ndo mana miaka nenda rudi nchi yetu chini yenu itazidi kuwa masikini sana. Ccm hamna akili sana na lazima tuwatoe mwaka huu
 
Kwanini hamkuoversee hii possibility,,?,ndo maana nasemaga hamjawa tayari kuongoza,hii ilitakiwa muione kabla na muweke plan B,C,D
Kwa kuaanza ku over see kila possibility ya kukwamisha huwezi kufanya kampaini, kumzuia lissu kutofika Dar kwenye mkutano huo wahamisho kwa vikwanzo vya TCAA ni faida kubwa kwake katika kampeini kuliko kuhudhuria hicho kikao
 
Back
Top Bottom