Tetesi: Lissu adaiwa kumponza Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji

Tetesi: Lissu adaiwa kumponza Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji

Lakini hebu tulifikirie jambo hili la mbaazi kiundani zaidi, mbona katika masoko ya Dar na kwengineko nchini bei ya mbaazi ipo juu ya shilingi 1500?! Kwanini wakulima wa huko kusini wasiuzie katika soko la ndani? Au kuna nini hasa kinachoendelea?
mkuu bei ya mbaazi shambani ni mbovu sana hata hivyo huyo wa sokoni anauza ili kufidia gharama zake za usafirishaji + ununuzi
 
hahahahaha tangia lini balozi akawa mkubwa kuzidi naibu katibu mkuu ikulu labda kama unaongelea ukubwa wa kukaa nje ya nchi hahahaha....unajua mshahara wa balozi? hahaha bawacha bhana mtu kapandishwa cheo ninyi mnafikiri ameshushwa
Huyo kufurumushwa ulaya baada ya kujichanganya kwa heshima ya baba kawekwa hapo kusoma magazeti mifupi kamuuzi sana jiwe kwa sasa hali ni mbaya taarifa zishavuja.
 
Sasa mbona cheo kapandishwa? au unafikiri kuwa nje ya nchi na kurudishwa nchini ni kushushwa cheo? Balozi anaweza kuwa mkubwa zaidi ya Naibu katibu mkuu ikulu? hahahaha
Unaangalia kigezo gani Rutta? mshahara,status au eneo la utawala? Binafsi sioni tofauti ya nafasi kati ya naibu katibu mkuu na mawaziri vivuli bungeni.Yaani kutoka kuiwakilisha nchi katika masuala ya kidiplomasia na kuwa msaidizi wa katibu vifanane kweli? Huu ni utani wa kiwango cha SGR.
Cheo cha balozi kinatambulika duniani kote huu unaibu sidhani hata hazina kama wanaweza kumkabidhi fungu la wizara.
 
Kama kweli katolewa Ubalozini nadhani hiyo sio sababu, serikali ingelikuwa na shida hata Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassani asingelikwenda kumuona Lissu alipokuwa Hospitalini Nairobi na hata kutoa salamu za Rais, nadhani hizi ni hisia negative ambazo wengi wetu tuzijenga kwenye fikra zetu.

Ni mtizamo wangu tu
Sasa wewe unadhani Samia anaweza kuchukuliwa hatua gani na huyo mwenye chuki? au hujui kuwa Samia ni mgombea mwenza na katiba inasemaje kuhusu cheo chake?
 
Sasa mbona cheo kapandishwa? au unafikiri kuwa nje ya nchi na kurudishwa nchini ni kushushwa cheo? Balozi anaweza kuwa mkubwa zaidi ya Naibu katibu mkuu ikulu? hahahaha
Usitudanganywe bwana! ingekuwa ni hivyo Balozi Costa Mahalu akiwa Italy asingeweza kumvimbia Waziri wa mambo ya nje Kikwete wakati ule. Balozi anayo hadhi tofauti sana na sio Naibu Katibu mkuu tuu bali hata katibu mkuu
 
Hadhi ya ubalozi unaishi nayo mpaka siku ya kuondoka duniani wakati ukatibu ama unaibu unaishia siku unapotenguliwa tu.
 
Hizo ni tetesi...weka nyama kwa kuniambia mafanikio na madhaifu ya balozi huyo hapo belgium
1. Kajenga barabara
2. Kanunua pampu ya kijiji
3. Kahamasisha wananchi kuchangia mbio za mwenge
4. Anatembea na ilani ya 'chuma twawala'
5. Anahamasisha uzalendo
 
Mpumbavu!
Huu uzi ulikuwa na zaidi ya comment za aina yako kama 300 lakin mods wamefuta zote zimebaki zile zenye mantiki na za kiume nnachoweza kukusaidia ni kukupuuza tu
 
Usitudanganywe bwana! ingekuwa ni hivyo Balozi Costa Mahalu akiwa Italy asingeweza kumvimbia Waziri wa mambo ya nje Kikwete wakati ule. Balozi anayo hadhi tofauti sana na sio Naibu Katibu mkuu tuu bali hata katibu mkuu
ikulu ndo inatoa maagizo ndani na nje ya nchi,km aliteuliwa na mamlaka hiyo kwa vigezo vyao je akibadilishiw kazi kuna tabu,inawezekana alilotumwa kamaliza kulifanikisha sasa anatumwa mwingine kufanikisha lingine,kwani anapaswa kuwa balozi nje mpaka astafuu,inawezekana anaekwenda kule ana vigezo na uwezo tofauti na pia anaenda kutekeleza jambo jingine
 
Mbona makamu wake hajambadilisha si alienda msalimia
 
ikulu ndo inatoa maagizo ndani na nje ya nchi,km aliteuliwa na mamlaka hiyo kwa vigezo vyao je akibadilishiw kazi kuna tabu,inawezekana alilotumwa kamaliza kulifanikisha sasa anatumwa mwingine kufanikisha lingine,kwani anapaswa kuwa balozi nje mpaka astafuu,inawezekana anaekwenda kule ana vigezo na uwezo tofauti na pia anaenda kutekeleza jambo jingine
That is for the sake of malumbano tuu. Kubadilishwa jambo ni kawaida lakini kupo kwingine ni kwa sababu zilizotokea.
Kama Kumbadili Mwigulu na Kangi, huwezi sema ni mabadiliko tuu ila sababu ipo.
 
Usitudanganywe bwana! ingekuwa ni hivyo Balozi Costa Mahalu akiwa Italy asingeweza kumvimbia Waziri wa mambo ya nje Kikwete wakati ule. Balozi anayo hadhi tofauti sana na sio Naibu Katibu mkuu tuu bali hata katibu mkuu
katibu mkuu ni mtendaji na mara nyingi anapaswa kuzingatia mwongozo rasmi na ndio msimamizi wa bajeti ya wizara yake,balozi anapswa kutekeleza majukumu kupitia njia rasmi ya wizara yake au majukum yasiyo rasmi kupitia ikulu,na balozi akishindwa kutekeleza majukumu yake km anavyo agizwa inaangaliwa mamlaka yaliyomuagiza anashtakiwa huko au km mamalaka mbili zinakinzana inaangaliwa mamlaka ya juu zaidi ya uteuzi na nidhamu
 
Tetesi hizi hazina ukweli wowote,haina uthibitisho na maelezo ya kutosha, ni kama imetungwa kwa madhumini fulani hivi,infact kwa nionavyo ona mimi amepewa promotion ya kuja kuwa karibu na Raisi kumtembelea Tundu haiwezi kuwa chanzo cha kuteuliwa kufanya kazi Ikulu
 
Hata chadema huko hali tete..Kama unabisha ngoja siku mnyika aende ikulu uone..Au asifie chochote..Sema tu nyie mkifanyiwa ndio mnajifanya kuleta utaifa
Ikulu kuna mgonjwa au mfiwa? Kujuliana hali ni jadi yetu, soma vizuri, elewa mada kisha toa mfano.
 
Back
Top Bottom