Tetesi: Lissu adaiwa kumponza Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji

Tetesi: Lissu adaiwa kumponza Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji

Pamoja na kwamba anayejua ukweli wa huo uamuzi wa kumrudisha nchini ni Mh.rais, tungejiuliza kwanza hivi kutoka kuwa balozi mpaka kuwa naibu katibu mkuu ikulu ni Demotion (kushushwa cheo) au promotion (kupandishwa cheo) both interms of opportunity and exposure, labda kuanzia hapo ndo tuanze kuunganisha dot.
Siku hizi ukiwa mshabiki wa Chadema akili unaziweka kando, mtu kupandishiwa cheo, alafu unasema kaponzwa na Lisu, kama sio ujinga wa mashabiki wa Chadema
 
Siku hizi ukiwa mshabiki wa Chadema akili unaziweka kando, mtu kupandishiwa cheo, alafu unasema kaponzwa na Lisu, kama sio ujinga wa mashabiki wa Chadema
Kumbe balozi wa marekani anaweza kuamrishwa jambo na naibu katibu mkuu wa ikulu na kufukuzwa?
 
Siku hizi ukiwa mshabiki wa Chadema akili unaziweka kando, mtu kupandishiwa cheo, alafu unasema kaponzwa na Lisu, kama sio ujinga wa mashabiki wa Chadema
Mkuu kutokana na baadhi ya vyeo kukosekana kwenye katiba yetu ya JMT imekua ni ngumu kudhibitisha moja kwa moja hiyo ni demotion au promotion, labda kama una vitu ambavyo vinaweza kudhibitisha kuwa hiyo ni promotion tusaidie ili tuweze kumaliza huu mjadala, vinginevyo hapa watu watabaki kubishana tu bila kujenga hoja na mwisho wa siku kudhihakiana.
 
Toka jana mkuu nakusoma post zako nashawishika kusema unawinda ukweli unafaa sana kuwepo jf hongera.
 
Kumbe balozi wa marekani anaweza kuamrishwa jambo na naibu katibu mkuu wa ikulu na kufukuzwa?
Hilo la naibu katibu mkuu kumuamrisha balozi sidhani kama linawezekana na vivyo hivyo pia suala la balozi kumuamrisha naibu katibu mkuu haliwezekani, kwa hyo hoja yako hapo haidhibitishi nani ni mkubwa kwa mwingine, ila kuhusu Marekani (ambayo umeonekana kupenda kuitumia) hakuna ajuaye na kuna uwezekano mkubwa sana wa jambo moja likawa na tafsiri tofauti panapohusika nchi mbili hasa pale msingi wa jambo hilo linapokuwa katiba, katiba ya Marekani ni tofauti na ya TZ na lingine ni kwamba USA haipo jumuiya ya madola ambapo tanzania imo na miongoni mwa taratibu za TZ zinaendana na nchi za jumuiya ya madola, hivyo masuala mengi ya kikatiba ungetumia ulinganisho wa TZ labda na mataifa yaliyo jumuiya ya madola kwani ndo kidogo zinaendana.
 
Nnachojua balozi wa angola akiwa hapa kwetu hawezi kusumbuliwa na hicho cheo ambacho kapewa mtoto wa sokoine au katibu mkuu ikulu isipokuwa wao watamwambia raisi mwenenendo wake kama sio mzuri ndipo raisi atachukua jukumu la kuwaambia angola mtu wao sio ndipo angola watamchukua mtu wao ila katibu mkuu anaweza kukamatwa hata akiwa angola bila kizuizi chochote

Hope utakuwa uneona madaraka ya cheo cha ubalozi
 
hali ngumu bado mmeng'ang'ana maofisi ya umma... si muache kazi wangine waingie... wenye kusubutu kukinga kifua... au kupelekwa pelekwa yote sawa tu...
 
Hilo la sijui Marekani na Angola limetoka wapi Mkuu, lakini mada uliyoleta inamzungumzia mtoto wa Sokoine ambaye alikuwa balozi wa Tanzania umoja wa Ulaya ila kupitia mabadiliko madogo yaliyofanyika juzi akahamishiwa ikulu kuwa naibu katibu mkuu, swali langu ni kutaka kujua huko ni kupandishwa cheo ama kushushwa cheo? Naomba unijibu kama ikikupendeza
Amepandishwa cheo naibu katibu mkuu Ni cheo kikubwa kuliko balozi.
watanzania tuache ulimbukeni nyumbani Kuna fursa nyingi na nzuri kuliko nje ya nchi.
kama Ni hivyo mtoa mada nikuulize mh mahiga alikuwa new York balozi amerudi nyumbani kuwa waziri je amepandishwa cheo au ameshushwa?
habari yako hujaifanyia uchunguzi WA kutosha,ingekuwa vyema ungetuletea picha tu na utambulisho bila kuongeza maneno yoyote ya uongo
 
Amerudishwa nyumbani akajiandae kugombea ubunge 2020, ili baadaye awe mgombea rais, si unajua maandalizi mapema.
 
Toka chanzo changu nyeti cha habari kimedadavua habari hii kwa uhakika kabisa kwamba kisa cha kutolewa ubalozi mtoto wa sokoine nchini ubelgiji na kurudishwa nchini ni kile kitendo cha yeye kwenda kumjulia hali mheshimiwa Tundu lissu.

Inasemekana bwana mkubwa hakufarahishwa na kitendo cha balozi wetu kwenda kumuona ndugu lissu na kumuona ni msaliti akaenda mbali zaidi na kusema hali kama hiyo aliipitia ndugu Lazaro Nyalundu alipokwenda kumuona lissu kwani wabunge wa ccm walizuiwa kwenda na ndicho chanzo kikuu cha Nyalandu kuamua kuachia ubunge wake na kujitoa ndani ya chama cha mapinduzi ( ccm) kwa kuwa hakuridhishwa na namna ya hilo jambo lilivyokuwa likiendeshwa na mwenyekiti wao.

Kahitimisha kwa kusema kwamba wanachama wao kwa sasa wanahali ngumu mno katika vipindi vyote ambayo wapo ndani ya chama hicho kikongwe.

My take:

Kwa upande wangu naona hili jambo si zuri hasa kwa sisi Watanzania tulishazoea kuishi kwa upendo kwani siasa sio uadui lakini inashangaza bwana mkubwa anapogeuza siasa ni uadui hasa kwa yale majibu yake ya kuomba aachwe afanye atakavyo aje kuulizwa mbele hii kitu inatia shaka mno,

Inakuwaje mtu anasema siasa nazifungia kwa kuwa natukanwa huku nikiwajengea barabara je hizo pesa ni za hisani toka mfukoni kwake? Nakumbuka wanafunzi wa udom waliitwa vilaza sijui kama anakumbuka hizi kauli za kuudhi.

Ukipenda kusifiwa kubali kunakukosolewa hata shilingi ina pande mbili.
Kwa hiyo mabalozi wote wanao ondolewa kwenye vituo vyao vya kazi walienda kumjulia hali Tundu Lissu,au Tundu Lissu sio Mtanzania ?akili za Ufipa hizi kujifanya kila kitu mnajua na huu ni umbeya.
 
Mbona rais yeye huwa anakwenda kuwajulia hali wapinzani wakilazwa hapo Muhimbili?
 
Hizi sio tetesi tu bali ni uzushi, tulimwona Makamu wa Rais akimtembelea Lisu huko Hospitali nairobi, tatizo lenu, kila kitu mnahisi tu na kutaka kutupotosha, kila jambo ni hisia na mihemko. sijui lini mtajifunza kuwa watu wa hoja badala ya hisia.
 
Hizo ni tetesi...weka nyama kwa kuniambia mafanikio na madhaifu ya balozi huyo hapo belgium
Siyo lazima tuongelee "mafanikio na madhaifu" ya balozi huyo. unataka kuwa kama mganga wa jadi anayekuambia kaniletee jasho la nyoka ili nikutibu, au kamkamue Tembo anayenyonyesha ulete maziwa fresh, ukishindwa umeshindwa wewe? Kama wewe unayajua tuambie. lakini kuna "circumstantial evidence hapa" - ushahidi wa kimazingira - kuhusu tabia ya Magufuli kuwachukia wapinzani kwa chuki ya wazi, na kuzuia wengine kuhusiana nao
1. Hiyo la wabunge wa CCM kuzuiwa kwenda kumuona Lema mahabusu nalo ni uwongo?
2. Ni wabunge wangapi wa CCM walimtembelea Lissu alipolazwa Nairobi? Nyalandu aliyefanya hivyo aliishia kujiuzulu na kujiondoa CCM.
3. Kitendo cha wabunge wa CCM na wa Upinzani kuungana kuwatetea wakulima wa Korosho kilimkera sana Magufuli, kiasi cha kutishia kuwatimua wabunge wa CCM walioshiriki, hata kama hana mamlaka ya kufanya hivyo.
Hiyo ya Ubelgiji ni tetesi, lakini ina uzito mkubwa sana na uwezekano mkubwa wa kuwa ni kweli.
 
Hizi sio tetesi tu bali ni uzushi, tulimwona Makamu wa Rais akimtembelea Lisu huko Hospitali nairobi, tatizo lenu, kila kitu mnahisi tu na kutaka kutupotosha, kila jambo ni hisia na mihemko. sijui lini mtajifunza kuwa watu wa hoja badala ya hisia.
Kumbuka safari aliyokwenda Makamu ilikuwa aende Magufuli mwenyewe. shida hapo ilikuwa ni kwamba atakwendaje Nairobi halafu akwepe kumtembelea Lissu? kidiplomasia ingekuwa na utata. sitashangaa kwamba hiyo ilikuwa sababu ya kumtuma Samia Nairobi. na pia Samia alilazimika kwenda kumuona Lissu kutokana na sababu za kidiplomasia. ni tofauti na ya balozi wa ubelgiji. ukitaka kulinganisha, linganisha na balozi wetu wa Kenya, Pindi Chana.
 
Pamoja na kwamba anayejua ukweli wa huo uamuzi wa kumrudisha nchini ni Mh.rais, tungejiuliza kwanza hivi kutoka kuwa balozi mpaka kuwa naibu katibu mkuu ikulu ni Demotion (kushushwa cheo) au promotion (kupandishwa cheo) both interms of opportunity and exposure, labda kuanzia hapo ndo tuanze kuunganisha dot.
Ni promotion
 
hizi nafasi za uteuzi kwa sasa ni sawa na kuishi kama digidigi kwenye msitu wenye simba wengi.
 
Back
Top Bottom