Tetesi: Lissu adaiwa kumponza Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji

Siku hizi ukiwa mshabiki wa Chadema akili unaziweka kando, mtu kupandishiwa cheo, alafu unasema kaponzwa na Lisu, kama sio ujinga wa mashabiki wa Chadema
 
Siku hizi ukiwa mshabiki wa Chadema akili unaziweka kando, mtu kupandishiwa cheo, alafu unasema kaponzwa na Lisu, kama sio ujinga wa mashabiki wa Chadema
Kumbe balozi wa marekani anaweza kuamrishwa jambo na naibu katibu mkuu wa ikulu na kufukuzwa?
 
Siku hizi ukiwa mshabiki wa Chadema akili unaziweka kando, mtu kupandishiwa cheo, alafu unasema kaponzwa na Lisu, kama sio ujinga wa mashabiki wa Chadema
Mkuu kutokana na baadhi ya vyeo kukosekana kwenye katiba yetu ya JMT imekua ni ngumu kudhibitisha moja kwa moja hiyo ni demotion au promotion, labda kama una vitu ambavyo vinaweza kudhibitisha kuwa hiyo ni promotion tusaidie ili tuweze kumaliza huu mjadala, vinginevyo hapa watu watabaki kubishana tu bila kujenga hoja na mwisho wa siku kudhihakiana.
 
Toka jana mkuu nakusoma post zako nashawishika kusema unawinda ukweli unafaa sana kuwepo jf hongera.
 
Hiyo nafasi huko Ubeligiji imeshajazwa au kuna nafasi "niombe"
 
Kumbe balozi wa marekani anaweza kuamrishwa jambo na naibu katibu mkuu wa ikulu na kufukuzwa?
Hilo la naibu katibu mkuu kumuamrisha balozi sidhani kama linawezekana na vivyo hivyo pia suala la balozi kumuamrisha naibu katibu mkuu haliwezekani, kwa hyo hoja yako hapo haidhibitishi nani ni mkubwa kwa mwingine, ila kuhusu Marekani (ambayo umeonekana kupenda kuitumia) hakuna ajuaye na kuna uwezekano mkubwa sana wa jambo moja likawa na tafsiri tofauti panapohusika nchi mbili hasa pale msingi wa jambo hilo linapokuwa katiba, katiba ya Marekani ni tofauti na ya TZ na lingine ni kwamba USA haipo jumuiya ya madola ambapo tanzania imo na miongoni mwa taratibu za TZ zinaendana na nchi za jumuiya ya madola, hivyo masuala mengi ya kikatiba ungetumia ulinganisho wa TZ labda na mataifa yaliyo jumuiya ya madola kwani ndo kidogo zinaendana.
 
Nnachojua balozi wa angola akiwa hapa kwetu hawezi kusumbuliwa na hicho cheo ambacho kapewa mtoto wa sokoine au katibu mkuu ikulu isipokuwa wao watamwambia raisi mwenenendo wake kama sio mzuri ndipo raisi atachukua jukumu la kuwaambia angola mtu wao sio ndipo angola watamchukua mtu wao ila katibu mkuu anaweza kukamatwa hata akiwa angola bila kizuizi chochote

Hope utakuwa uneona madaraka ya cheo cha ubalozi
 
hali ngumu bado mmeng'ang'ana maofisi ya umma... si muache kazi wangine waingie... wenye kusubutu kukinga kifua... au kupelekwa pelekwa yote sawa tu...
 
Amepandishwa cheo naibu katibu mkuu Ni cheo kikubwa kuliko balozi.
watanzania tuache ulimbukeni nyumbani Kuna fursa nyingi na nzuri kuliko nje ya nchi.
kama Ni hivyo mtoa mada nikuulize mh mahiga alikuwa new York balozi amerudi nyumbani kuwa waziri je amepandishwa cheo au ameshushwa?
habari yako hujaifanyia uchunguzi WA kutosha,ingekuwa vyema ungetuletea picha tu na utambulisho bila kuongeza maneno yoyote ya uongo
 
Amerudishwa nyumbani akajiandae kugombea ubunge 2020, ili baadaye awe mgombea rais, si unajua maandalizi mapema.
 
Kwa hiyo mabalozi wote wanao ondolewa kwenye vituo vyao vya kazi walienda kumjulia hali Tundu Lissu,au Tundu Lissu sio Mtanzania ?akili za Ufipa hizi kujifanya kila kitu mnajua na huu ni umbeya.
 
Mbona rais yeye huwa anakwenda kuwajulia hali wapinzani wakilazwa hapo Muhimbili?
 
Hizi sio tetesi tu bali ni uzushi, tulimwona Makamu wa Rais akimtembelea Lisu huko Hospitali nairobi, tatizo lenu, kila kitu mnahisi tu na kutaka kutupotosha, kila jambo ni hisia na mihemko. sijui lini mtajifunza kuwa watu wa hoja badala ya hisia.
 
Hizo ni tetesi...weka nyama kwa kuniambia mafanikio na madhaifu ya balozi huyo hapo belgium
Siyo lazima tuongelee "mafanikio na madhaifu" ya balozi huyo. unataka kuwa kama mganga wa jadi anayekuambia kaniletee jasho la nyoka ili nikutibu, au kamkamue Tembo anayenyonyesha ulete maziwa fresh, ukishindwa umeshindwa wewe? Kama wewe unayajua tuambie. lakini kuna "circumstantial evidence hapa" - ushahidi wa kimazingira - kuhusu tabia ya Magufuli kuwachukia wapinzani kwa chuki ya wazi, na kuzuia wengine kuhusiana nao
1. Hiyo la wabunge wa CCM kuzuiwa kwenda kumuona Lema mahabusu nalo ni uwongo?
2. Ni wabunge wangapi wa CCM walimtembelea Lissu alipolazwa Nairobi? Nyalandu aliyefanya hivyo aliishia kujiuzulu na kujiondoa CCM.
3. Kitendo cha wabunge wa CCM na wa Upinzani kuungana kuwatetea wakulima wa Korosho kilimkera sana Magufuli, kiasi cha kutishia kuwatimua wabunge wa CCM walioshiriki, hata kama hana mamlaka ya kufanya hivyo.
Hiyo ya Ubelgiji ni tetesi, lakini ina uzito mkubwa sana na uwezekano mkubwa wa kuwa ni kweli.
 
Hizi sio tetesi tu bali ni uzushi, tulimwona Makamu wa Rais akimtembelea Lisu huko Hospitali nairobi, tatizo lenu, kila kitu mnahisi tu na kutaka kutupotosha, kila jambo ni hisia na mihemko. sijui lini mtajifunza kuwa watu wa hoja badala ya hisia.
Kumbuka safari aliyokwenda Makamu ilikuwa aende Magufuli mwenyewe. shida hapo ilikuwa ni kwamba atakwendaje Nairobi halafu akwepe kumtembelea Lissu? kidiplomasia ingekuwa na utata. sitashangaa kwamba hiyo ilikuwa sababu ya kumtuma Samia Nairobi. na pia Samia alilazimika kwenda kumuona Lissu kutokana na sababu za kidiplomasia. ni tofauti na ya balozi wa ubelgiji. ukitaka kulinganisha, linganisha na balozi wetu wa Kenya, Pindi Chana.
 
Ni promotion
 
hizi nafasi za uteuzi kwa sasa ni sawa na kuishi kama digidigi kwenye msitu wenye simba wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…