Uchaguzi 2020 Lissu ailipua TCRA na Idara ya Habari Maelezo kwa kunyanyasa Vyombo vya Habari vinavyoripoti habari zake, aahidi kuifutilia mbali

Naam anashinda na malaika mkuu, siyo? Siyo vizuri kushindana na malaika mkuu.
Sio malaika chaliii ni level mbili tofauti huyo Lissu ni kamanda Magu ni Rais ni sawa na ardhi na mbingu.
 
Pale TCRA Mh amewajaza watiifu wake sana adi mwanae..chunguzeni hapo TCRA.
 
We ulipata kula ngapi ndugu??? Kweli msomi kama wewe?? Upate kura mbili?? Ina maana wanakuona huna akili??
Wajumbe wamedhihirisha kiwa hata mijadara yako humu ndani ina kura mbili
 
Kwani vyombo vya habari vina muda wa kutoa habari mbona wewe kama huwahi kufuta ujinga ni wapi huko ambako vyombo vinasubiri muda wa kutoa habari
Kwani wanalazimika kutoa habari?!
 
TCRA ni janga. Futilia mbali.
 

Hakuna uduktetea wa kizalendo Pascali. dikteta ni dikteta tu. watu kupotea, ktk mazingira ya kutekwa, watu kuuwawa na wengine kuokotwa ktk visandarusi ndio sehemu ya udikteta wa maendeleo ? Hapan ndugu yngu Pascali. jiwe liite jiwe sio mpapai.
 
Pasi-kali(pascal) ulikosa maneno/majina ya kumpamba kiongoz wako mpaka umuite dikiteta?
Ubaya ni ubaya tu,hamna ubaya mzuri.Mfano ungesema tumempata kiongozi mkali,mfuatiliaji au makini ingetosha kuliko kusema tulimuhitaj na tumempata kiongozi dikiteta,kama utukuzaj wenyewe n huu basi nina mashaka na taalum yako!
 
Kwani kila mtanzania anaona YouTube au umejitoa ufahamu hivo unaona sawa vyombo vya habari kutozwa faini sababu ya kumuhoji mgombea urais wa Tanzania. Nchi hii inakwamishwa na watu wenye mawazo kama yakwako.
Malim Seif ni mwanasiasa mkubwa sana mwenye kuungwa mkono na Block karibu yote ambayo ni Pemba toka 1995 akiwa mgombea Urais kwa CUF na media hazijawahi kumkimbia au kutozwa faini kwa kumhoji.

Bila shaka huyo anaekimbiwa na vyombo vya habari ni either hana content ya ku-offer, to the extent ya kukimbiwa au kupotezewa.

By the way, mtu mwongo TL mwenye hadaa kama mwenye statement hizi hapa chini; tunawezaje kumwanini
https://www.facebook.com/
Akipata kura kama za Mrema 1995; utakuwa muujiza mkubwa sana.
 
Udikteta wa kuzuia vyombo vya habari unakupa faida gani wewe Mayala? Tukikubali mambo ya kijinga namna hii, kuna siku kiongozi atawaua raia halafu tutasifia kuwa mauaji ya kizalendo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…