Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Akizungumza kutoka Singida Mgombea huyo wa Urais wa CHADEMA, Mhe. Lissu amefichua njama za kishamba za TCRA na idara ya habari maelezo za kushughulikia vyombo vya habari vinavyoripoti habari zake.
Tayari BBC wamepigwa faini ya Tsh. mil. 15 kwa kurusha mahojiano na Tundu Lissu huku RFA ikiambiwa ijieleze kwanini isiadhibiwe kutokana na kurusha alichoongea Lissu na BBC.
Hata hivyo Mhe. Lissu ameahidi kufutilia mbali TCRA na idara ya habari maelezo iwapo Watanzania wataamua kumpatia Urais.
Lissu anadai malengo ya tume ya Nyalali ya kuondoa SHIHATA na kuleta TCRA yalilenga kuondoa ukiritimba baada ya Shihata kuonekana kuipendelea serikali, jambo ambalo bado halijatimia kwa vile TCRA wameendelea kutumika .
Binafsi naunga mkono TCRA Kufutiliwa mbali.