Uchaguzi 2020 Lissu ailipua TCRA na Idara ya Habari Maelezo kwa kunyanyasa Vyombo vya Habari vinavyoripoti habari zake, aahidi kuifutilia mbali

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Akizungumza kutoka Singida Mgombea huyo wa Urais wa CHADEMA, Mhe. Lissu amefichua njama za kishamba za TCRA na idara ya habari maelezo za kushughulikia vyombo vya habari vinavyoripoti habari zake.

Tayari BBC wamepigwa faini ya Tsh. mil. 15 kwa kurusha mahojiano na Tundu Lissu huku RFA ikiambiwa ijieleze kwanini isiadhibiwe kutokana na kurusha alichoongea Lissu na BBC.

Hata hivyo Mhe. Lissu ameahidi kufutilia mbali TCRA na idara ya habari maelezo iwapo Watanzania wataamua kumpatia Urais.

Lissu anadai malengo ya tume ya Nyalali ya kuondoa SHIHATA na kuleta TCRA yalilenga kuondoa ukiritimba baada ya Shihata kuonekana kuipendelea serikali, jambo ambalo bado halijatimia kwa vile TCRA wameendelea kutumika .

Binafsi naunga mkono TCRA Kufutiliwa mbali.
 
Naunga mkono hoja, nchi inaendeshwa kidikiteta, lakini udikiteta wenyewe ni udikiteta wa kizalendo, a benevolent dictatorship, anafanya udikiteta kwa lengo la kuleta maendeleo kwa manufaa ya taifa.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

P
Mkuu maendeleo bila kutenda haki.
Kiongozi wa kweli ni yule atakaebadilisha uchumi wa watu wake na kuwapa Uhuru wa kujieleza ni hii huleta maendeleo endelevu.
 
Tena kufutilia mbali kabisa na wafanyakazi wake wote kuwafuta kazi wamevitesa Sana vyombo vya habari ndani ya hi miaka 5 na pia wamekuwa na ukilitimba wa kuwapa waru leseni

Jf ilizimwa kwa muda baada ya kupiga kelele wakalipishwa pesa ndefu Sana wakarudi hewani

TCRA ni janga la Taifa.
 
Anaedai hana uhuru wa kusema, yuko Tanzania; hapo alipo kasema na kupitia YouTube kasikika.

Nadhani Tundu Lissu atupe vision yake anataka kutupeleka wapi Tanzania na sio kulalamika kila siku.

Watu kwa sasa wako huru kupata habari Nadhani kuliko nyakati zote.

Kama mainstream inaogopa, kuna various networks ambazo hata hao wanaolalama uhuru wa kusema kubinywa, wanatumia na kupata followers au ujumbe wao kufika.

So far kwa majigambo haya toka katika akidai katiba mpya siojaona jipya.

Kenya ambao tunawasifu kupata katiba mpya, ufisadi na kupiga hela kumeongezeka sana ukiwamo upigwaji wa hela zs Covid19.

Bila shaka JPM akashinda kwa kura nyingi ajabu. Na kama TL hatabadili ujumbe wake; akipata kura nyingi kuzidi za Mrema 1995; basi huu utakuwa muujiza.
 
Akizungumza kutoka Singida Mgombea huyo wa Urais wa CHADEMA, Mhe. Lissu amefichua njama za kishamba za TCRA na idara ya habari maelezo za kushughulikia vyombo vya habari vinavyoripoti habari zake.

Tayari BBC wamepigwa faini ya Tsh. mil. 15 kwa kurusha mahojiano na Tundu Lissu huku RFA ikiambiwa ijieleze kwanini isiadhibiwe kutokana na kurusha alichoongea Lissu na BBC.

Hata hivyo Mhe. Lissu ameahidi kufutilia mbali TCRA na idara ya habari maelezo iwapo Watanzania wataamua kumpatia Urais.

Lissu anadai malengo ya tume ya Nyalali ya kuondoa SHIHATA na kuleta TCRA yalilenga kuondoa ukiritimba baada ya Shihata kuonekana kuipendelea serikali, jambo ambalo bado halijatimia kwa vile TCRA wameendelea kutumika .

Binafsi naunga mkono TCRA Kufutiliwa mbali.

Jamaa yako ni domokaya hana jipya ati atafuta TCRA anaanzaje ?!!
aendelee kupiga domo John Pombe anamgaragaza mapema mno, ata akifika Oct 28 lijamaa pumzi itakuwa imekata.
 
Anaedai hana uhuru wa kusema, yukp Tanzania; hapo alipo kasema na kupitia YouTube kasikika.

Nadhani Tundu Lissu atupe vision yake anataka kutupeleka wapi Tanzania na sio kulalamika kila siku.

Watu kwa sasa wako huru kupata habari Nadhani kuliko nyakati zote.

Kama mainstream inaogopa, kuna various networks ambazo hata hao wanaolalama uhuru wa kusema kubinywa, wanatumia na kupata followers au ujumbe wao kufika.

So far kwa majigambo haya toka katika akidai katiba mpya siojaona jipya.

Kenya ambao tunawasifu kupata katiba mpya, ufisadi na kupiga hela kumeongezeka sana ukiwamo upigwaji wa hela zs Covid19.

Bila shaka JPM akashinda kwa kura nyingi ajabu. Na kama TL hatabadili ujumbe wake; akipata kura nyingi kuzidi za Mrema 1995; basi huu utakuwa muujiza.
Mnaogopa nini kumpa airtime kwenye television za ndani ya Tanzania?
 
Back
Top Bottom