Shibuda alikuja kabla ya ule upuuzi wa 2015, maana yeye aliingia 2010. Nilidhani cdm walijifunza kutokana na mwenendo wa Shibuda ndani ya cdm, maana Shibuda alikuwa mbunge kwa ticket ya cdm, lakini akabaki mwanaccm mtiifu. Ilifikia hatua hadi cdm wakamtenga Shibuda. Lakini 2015 wakafanya maamuzi ya kipuuzi kabisa kuliko ya huyo Shibuda.
Hata ukitazama kundi kubwa la viongozi wa cdm waliorejea ccm wakati wa dhalimu magu kwenye kampeni ya kuunga mkononi juhudi, ni wale waluokuja muda mfupi Kabla ya uchaguzi wa 2015, na kupewa nafasi kama Lowassa. Na mmoja kati ya waliorejea ccm ni huyo Lowassa. Nilisangaa sana Mbowe kupata ujasiri wa kugombea uenyekiti tena baada ya ile political blunder ya 2015! Mbowe alitakiwa kujiuzulu muda mrefu baada ya kete ya Lowassa kushindwa kuchukua urais.