Pre GE2025 Lissu aishangaa CHADEMA ilimpokeaje Nyalandu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndio maana nilishasema kutegemea wanasiasa pekee ili ndio watuhabarishe au wafanye kilicho chema wakati wana maslahi yao binafsi ni kama kutegemea kupe akupe blood donation ukipata ajali....

 
"Walikuja kuleta" mkuu kumbe na wewe ni kamanda kindakindaki
Kiswahili kigumu.

Nikisema kuwa Kenyatta alikuja kuwa rais wa Kenya ina maana mimi lazima niwe Mkenya au nipo Kenya.

Mimi kamanda kabla ya CHADEMA haijazaliwa. Nimevaa khaki suit na Cocoa Tea.

Unamjua Cocoa Tea wewe?
 
This is neither here nor there...., Nyalandu anaweza akawa mtu mwema sana, tena anaweza akawa rafiki yake kipenzi na Lissu na mtenda wema asiye na doa lakini haimaanishi ni perfect fit kwa CHADEMA / CHAMA kwahio sio kweli kwamba wote waliomtendea Lissu wema au kesho Samia akitaka apewe cheo CHADEMA basi apewe sababu tu alikwenda kumuangalia Lissu na Lissue asiseme kitu sababu alitendewa wema.... Tukishaanza siasa za Scratch my back I will Scratch yours wanufaika watakuwa wanasiasa kugawana Keki na sio Mwananchi Kitaa
 
Mbowe alifanya maamuzi ya tamaa za kuangalia muda mfupi ambayo yame ki cost sana chama.
 
Lisu anajipa umalaika ambao hana.
 
Lisu anajipa umalaika ambao hana.
Ni kweli Lissu msema hovyo na binafsi sidhani kama anaweza kuwa kiongozi mzuri Lissu ni mwanaharakati unamuhitaji ukiwa unagombania kitu / unapigania kitu kama mtu wa kuleta amsha amsha..... Ila ndio hivyo wanasiasa sio wa kuwaamini wana maslahi binafsi na wamekuwa flip floppers ni ngumu hata kujua wanasimamia nini (ingawa matumbo yao nadhani ndio kipaumbele)
 
Reactions: Tui
M
Lissu anatakiwa awe makini sana asijikute yupo kwenye Kundi la Msema hovyo Kama kina Zitto na Mrema.

Ngoma ikilia sana hupasuka.
True, mengine unayaacha. La Abdul sijalipenda kuliwka hadharani. asingelitaja jina
 
Hongera kwa msimamo wako, sijawahi kuwa kiongozi wa chama chochote Cha siasa, na sijawahi kutoa kura yangu kwa mwanaccm yoyote ni sintokaa niipe ccm kura yangu, iwapo kura kweli ina maana, kwani naamini kwenye mabadiliko ambayo Mbowe kafeli vibaya.

Ni hivi Magufuli hakuwa anafanya siasa ndio maana akawapiga Ban cdm kwasababu alijua mvuto wa cdm utampoteza. Inshort sijawahi kuwa muumini wa madubwasha ya aina ya magu.
 
Lissu kwa hili amekosea
Sijui mkuu 'Benjamini Neta', kama Lissu kakosea au la kuhusu Nyalandu. Huenda kuna mambo mengi ndani ya CHADEMA yanachangia kuhusu mikanganyiko yote hii.
Inawezekana Nyalandu alikwenda CHADEMA kwa kutopenda yaliyokuwa yanatokea ndani ya chama chake CCM wakati huo. Alipofika CHADEMA kagundua kuwa mambo hayakuwa kama alivyotegemea ndani ya chama hicho.
 
Mbowe aache family business?
 
Reactions: Tui
M

True, mengine unayaacha. La Abdul sijalipenda kuliwka hadharani. asingelitaja jina
Ni katika mwendelezo wa yale ya mabilioni kwa Magufuli, kumsema Mwalimu Nyerere kuwa mdanganyifu, n.k.,
Haya ni mambo yasiyomletea heshima hata kidogo.
Kama ushahidi upo kuhusu tuhuma husika, atumie hadhara maalum na kwa wakati mahsusi kuibua maswala ya aina hii. Siyo katika mikutano ya kuwaelimisha wananchi wajue wajibu na haki zao.
Anaivuruga kazi yake nzuri aliyolenga kuifanya.
 
Nyalandu aliacha ubunge na posho zake kujiunga Cdm Haina hata posho sidhani Kama ni maslahi

Ila hao wengine ni sawa walifuata maslahi
Aliacha kwa kuzira maana ya Magufuli kumtukuna kwa kwenda kumtembelea Lisu, lakini hakuwahi kuishi kama mwanacdm, bali mwanaccm aliye ukimbizini.
 
Mbowe alifanya maamuzi ya tamaa za kuangalia muda mfupi ambayo yame ki cost sana chama.
Kabisa, ni kama alitaka mafanikio bila kujali athari za muda mrefu. Pale ndio nilijua Mbowe hastahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama kama cdm.
 
Ni vigumu kujua kama uchaguzi ule Lowassa kweli alishinda, inawezekana.
Lakini naamini kwa dhati kabisa, Lowassa mwenye nguvu na siha kama yule aliyejiuzuru u-waziri mkuu wakati ule angekuwepo wakati wa kampeni ile iliyofanyika, sina shaka yoyote ile kwamba Magufuli na CCM wasingefurukuta.
Hali na mwonekano wa Lowassa kwenye kampeni iliondoa matumaini kwake kuwa rais.
Kuhusu uhalali wa kuwapokea ndani ya chama wakati ule...; hakika madhumuni na lengo la chama chochote cha siasa ni kushika madaraka, na CHADEMA iliiona fursa hiyo ndani ya Lowassa, bila kujali mengine yote yaliyopita. Matarajio yakiwa kwamba chama kikiwa na madaraka kitaweza kutimiza baadhi ya yale kinayoyapigania. Mtu anayekuja ndani ya chama, hata awe na nguvu kiasi gani, itamlazimu atimize baadhi ya matakwa ya chama.
Bila shaka matarajio ya CHADEMA yalikuwa kwa upande huo.
Sasa nimalize kwa kuchokonoa: endapo CHADEMA italenga kujishikiza kwa Samia kuingia madarakani; hiyo ni hali tofauti kabisa na ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…