Mimi kweli katika kuwaza kwangu ninashawishika kuamini kwamba JPM aliuziwa mbuzi kwenye gunia na akina Kikwete. CCM ilikuwa ikabidhi madaraka kwa wapinzani toka 2015 bahati nzuri Kikwete akachomoa. Tunachokiona sasa ni muendelezo wa wimbi la 2015. Kama isingekuwa mkono wa chuma wa JPM kuzima shughuli za siasa huenda kingeisha eleweka zamani.
Kosa alilolifanya JPM hakutumia tafiti kubuni mbinu ya kisiasa ya kuzima wimbi hilo, akaamua kutumia nguvu ya dola tu kudhibiti viongozi wa vyama vya upinzani, akasahau kuwa upinzani uko katika mioyo ya watu.
Kosa lingine la JPM ni kupenda kuzungukwa na wanaomuabudu, wasio na maono, akina Polepole. Na pia kuamini kuwa vyombo vya dola vikikaa sawa tatizo la kuishi ikulu limekwisha. Akafungia magazeti ambayo yangempa mrejedho wa kinachoendelea mtaani. Bunge huru nalo lingempa mwongo wa nini kifanyike mapema, huenda hata miaka 2 kabla ya uchaguzi. Akapendezwa na mbwembwe za Spika na naibu wake,
Polepole na Bashiru wakajikita katika siasa za kipolisi, kumbuka kwa watanzania, raia na polisi ni mbalimbali, kwanini? Kesi za kubambikizia, kunyima dhamana, kuziba midomo, kununua wapinzani, kukejeli, kujitweza, na kunyima watu haki zao hasa za uwakilishi.
Watu kimyaaa! Hawakujiuliza maana ya kimya kingi, wakadhani ni kukubalika, kumbe watanzania wanalao jambo. Wakaeleza macho yao katika tarehe ya uchaguzi mkuu. Wamesubiri tarehe hiyo toka miaka minne iliyopita na sasa zimebaki siku 26 watoe majibu kwa Polepole na Bashiru na ukomunist wao.!