Uchaguzi 2020 Lissu akamilisha ujazaji wa fomu za Urais Tanzania

Uchaguzi 2020 Lissu akamilisha ujazaji wa fomu za Urais Tanzania

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,903
TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, amekamilisha hatua za mwisho za ujazaji fomu za uteuzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Leo Ijumaa tarehe 21 Agosti 2020, Lissu akiambatana na mgombea mwenza, Salum Mwalimu, wamefika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kisheria ya ujazaji wa fomu zao za kugombea.

Akizungumza baada ya kukamilisha hatua hiyo, Lissu amesema wamefika katika mahakama hiyo kula kiapo cha ujazaji wa fomu hizo.

“Mimi ni mteule wa CHADEMA kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Salum anagombea makamo wa rais, taratibu ya sheria ya uchaguzi baada ya kutafuta wadhamini.”

“Kinachofuata ule kiapo mbele ya Jaji Mkuu, ukija kula kiapo kama sehemu ya kukamilisha ujazaji fomu ya uteuzi wa kugombea kinachofuata ni safari ya Dodoma kuwasiliha fomu za uteuzi siku ya Jumanne,” amesema Lissu.

Uteuzi wa wagombea urais itafanyika tarehe 25 Agosti 2020 Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma.

Baada ya uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi huo zitafanyika kuanzia tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.
 
Hivi nimakundi gani hasa yenye ushawishi ktk jamii yanayomuunga mkono Lissu.
Anaota kwenda ikulu kwa kura zipi hasa, maana idadi ya watu waliohamia ccm ndani ya miaka mitano si ya kubezwa.
 
Congratulations Tundu Lissu...

Hakuna cha kukuzuia kaka Lissu....

Kila hatua, Bwana Mungu Yehova ameisafisha na kuongoza njia yako...
å Uponyaji wako
å Safari back home from Kenya & Belgian after 3 yrs of Magufuli's bullets healings
å Kuteuliwa na Chama chako
å Kupokea fomu ya uteuzi NEC
å Kutafuta wadhamini

Na Leo utakula kiapo bila shaka yoyote maana alipo Mungu muumba (siyo ile miungu yao), hakuna kinachoshindikana....

Kisha nenda hatua zinazofuata;
å Kurudisha fomu ya uteuzi wa kuuendea Urais wa nchi hii, NEC - Dodoma
å Anza kampeni rasmi
å Shinda uchaguzi
å Tangazwa na kuwa Rais Mteule
å Apishwa kuwa Rais wa nchi hii.
å Ondoa kinga za kutoshitakiwa za waliojiwekea wahalifu wote wa nchi hii ili waanze kuonja matokeo ya dhambi zao..

KARIBU SANA MH. RAIS TUNDU A.M. LISSU...!!
 
Hivi nimakundi gani hasa yenye ushawishi ktk jamii yanayomuunga mkono Lissu.
Anaota kwenda ikulu kwa kura zipi hasa, maana idadi ya watu waliohamia ccm ndani ya miaka mitano si ya kubezwa.
Ccm inaushawishi kwa kundi lipi hao wapiga mitama ambao tulishawazarau na nyimbo zao au viongoz wa din uchwara
 
Back
Top Bottom